Upungufu wa dola nchini: Je, haiwezekani sababu ni kupungua kwa fedha za wafadhili kama sio matumizi ya dola katika kulipa madeni ya nje ya nchi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,187
144,807
Japo mimi sio mtaalamu wa mambo ya kifedha, lakini napata wasiwasi kuwa sababu ya upungufu wa dola hapa nchini inaweza kusababishwa na ama kupungua kwa fedha za wahisani kama sio matumizi ya dola katika kuhudumia deni la taifa sababu ambazo zinaweza kuwa ni ngumu kuziweka hadharani iwapo kweli ndio msingi wa hili tatizo kama ambavyo mimi nahisi?

Binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi ndio chanzo na kama kuna hiyo hali, basi BOT wangekuwa wameshasema unless imesemwa na mimi ndio sijasikia.

Anaeweza kutuwekea takwimu sahihi za upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia mikopo kutoka nje pamoja na fedha za misaada kwa mwaka mmoja uliopita atuwekee hapa ili tulinganishe na miaka ya nyuma.

Pia, anaeweza kutuwekea hadharani takwimu za ulipaji wa deni la nje ya nchi kwa mwaka mmoja uliopita akilinganisha na miaka ya nyuma.

Halikadhalika, yoyote anaeweza kutuwekea taarifa ya serikali kwa umma juu ya mikopo na misaada ya fedha inayopokelewa hapa nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kulinganisha na miaka ya nyuma.

Nashangaa siku hizi Zitto yuko kmya kabisa tofauti na enzi za Mwendazake alipokuwa akitumia taarifa za BOT kueleza maswala mbalimbali ya uchumi wakati leo hii uhuru wa kufanya hivyo umeongezeka tofauti na enzi za Mwendazake.
 
Back
Top Bottom