Serikali iangalie upya suala la usajili wa meli za kigeni baada ya kusitishwa mwaka 2018

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,952
12,527
Usajili wa Meli (Ship registration) hiki ni kitendo Cha kuipa meli uraia katika nchi Fulani na kurusiwa kutumia bendera hiyo iwapo baharini. Meli iliyosajiliwa na Tanzania italazimika kufata Sheria na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfano endapo meli itakiuka jambo lolote itaadhibiwa Kwa Sheria zetu.

Aina ya Usajili wa Meli (Type of Ship Registration)
1. Closed Registry


Huu ni usajili was meli ambao raia au wazawa wa nchi husika ndio uruhusiwa kusajili meli. Hii faida kubwa kwa mmiliki ni kupata uangalizi wa karibu kutoka Kwenye nchi yake(Genuine link). Mfano nchi zenye closed registry ni USA, Germany,Canada,UK na Japan.

2. Open Registry (Flag of Convenience-FOC)
Huu ni usajili ambao Mtu yeyote anaruhusiwa kusajili meli katika nchi yenu bila kujali uraia wake. Baadhi ya nchi ni Panama, Liberia,Cayman Island na Marshalls Island.

Asilimia kubwa ya meli Duniani zimesajiwa kwenye Open Registry, sababu kubwa zinazowavutia wamiliki wa meli ni:-
I. Mtu kuwa huru kusajili meli nchi nyingine

II. Unafuu wa Kodi

III. Rahisi kufanyika, Kwa nchi kama Panama na Liberia wanafanya mpaka online registration

Tanzania tunafanya Usajili upi wa Meli?
Tanzania tunafanya aina zote mbili za Usajili wa Meli. Tanzania bara inafanyika Closed Registry na Zanzibar wanafanya Open registry. Suala la Bahari na Bandari si la muungano(Non-Union Matter). Tanzania Bara na msimamizi wa masuala ya meli ni TASAC na Zanzibar Wana Zanzibar Maritime Authority (ZMA). Kwakuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hata Zanzibar wakisajili meli hutumia jina la Tanzania Zanzibar na meli upeperusha bendera ya Tanzania. Na meli itakayo sajiliwa Tanzania Bara upeperusha bendera ya Tanzania.

Usajili wa Meli Zanzibar (Open Registry)
Zanzibar Usajili wa Meli unafanyika nchini kwao na Ofisi ndogo ilikuwapo Dubai ambapo meli nyingi za kigeni zilikuwa zikisajiliwa huko.

Sababu ya Meli Kusitishwa kwa Usajili wa Meli zilizo sajiliwa Zanzibar
Meli nyingi zinazosajiliwa na Open Registry Huwa wamiliki wanakimbia Kodi au kutafuta unafuu wa Sheria na vigezo vya Usajili. Kuanzia miaka ya 2014 meli zilizokuwa na bendera yetu zilionekana baadhi ya nchi au kukakamatwa zikiwa na madawa au silaha.

Mwaka 2018 mwanzoni Kuna meli yenye bendera na Usajili wa Tanzania ilikamatwa na madawa ya kulevya Pwani ya Ugiriki na Kupelekea Raisi wa Jamhuri ya Muungano Hayati Dr JPM kutoa tamko la Kusitishwa kusajili meli kwa kuwa jambo hilo lilikuwa likichafua taswira ya nchi kimataifa.


Kwanini meli zetu tu ndio zilikuwa target(Why always Tanzania Zanzibar Ship), Meli nyingi zilizo sajiliwa Zanzibar zilikuwa ni za wamiliki wa mashariki ya Mbali,Ugiriki, Iran na Korea. Iran na Korea ni mataifa ambayo yapo kwenye vikwazo na mataifa makubwa kutokana na ishu za Nuclear. Vikwazo vya kiuchumi,kidiplomasia ndio vilifanya meli hizo kila zinapoingia nchi Fulani yenye bandari(Port State) kufanya ukaguzi wa hizo meli na kuziweka target Kisha kushikiliwa.

Meli mbalimbali zinakutwa na makosa ya silaha,madawa na kusafirisha binadamu lakini sio sababu za nchi hizo kuacha kusajili meli. Panama na Liberia wanameli nyingi na kila mwaka zinatoka list ya targeted ship au meli ambazo hazitakiwi kuingia nchi Fulani, kukutwa na madawa.

Unaposajili meli lazima ufate Sheria za nchi husika na ukikutwa na kosa utaadhibiwa na Sheria husika. Suala la kubeba madawa si la nchi Bali ni makosa ya wafanyakazi au wamiliki wa meli kutokana na tamaa nchi ikianza kusajili lazima ikaze Sheria kwenye usafirishaji wa madawa,silaha haramu na binadamu.

Baadhi ya nchi zinazofanya Usajili wa Open Registry na Closed Registry kwa wakati mmoja

China wanafanya Usajili wa Closed Registry na kupitia visiwa vya Hong Kong ambavyo vipo kwenye himaya ya China, Uingereza kupitia Cayman Islands na Marekani kupitia Marshall Islands vilivyo kwenye Himaya yao.

Hapa chini ni Moja ya thesis ambayo mtanzania mwenzetu alifanya wakati akichukua Master's yake chuo Cha World Maritime University nchini Sweden.


Namna ambavyo Nchi zenye Open Registry kama Liberia na Marshalls Island zinavyofanya na kufanikiwa zaidi

Liberia wao wameingia ubia na Corporate Company iliyopo New York, Marekani. Hivyo Sheria hutumika za Liberia na za Marekani kutokana na hiyo kampuni kuwa ni ya nchi ya Marekani. Hivyo matajiri wakubwa na wamiliki huvutika na sera za sajili za Liberia.

Faida za nchi kufanya Usajili wa Meli
1. Kupata pesa za Usajili wa Meli

2. Kuvuna baadhi ya Kodi kutokana na Usajili

3.Kuongeza wigo wa ajira kwa vijana ambao watafanya kwenye kampuni za meli

4. Kuongeza idadi ya meli zinazokuja Bandari yetu

5.Nchi kushiriki upitishwaji wa Sheria na maazimio ya Sheria za usimamizi wa bahari kidunia (International Maritime Organization {IMO} Convection and regulations)

6. Kuitangaza nchi kimataifa. Meli zinazosajiliwa na nchi yetu zitapepea bendera yetu popote duniani na nyuma na ubavuni mwa meli itaandikwa jina la bandari ya nyumbani (Home Port-kama ni Dar es Salaam, Tanga, Mtwara).

Meli popote iendapo inafuatiliwa na wenye mzigo,maagent,bandari na wakodishaji. Pia wamiliki hutumia majina au hupendelea kutumia majina ya Asili ya nchi husika kwenye Usajili was jina, nasi tunaweza kupata nafasi kwa wamiliki kutumia majina ya watu mashuhuri,vivutio au mbuga zilizopo hapa na kuitangaza vyema nchi.

Nini kifanyike ili Usajili wa meli za kigeni uendelee

Kuna msemo unasema "If you can't fight them,join them". Kama tumeshindwa kupambana na mataifa makubwa kwenye biashara ya Usajili wa Meli. Basi itabidi tutafute kampuni za kimarekani au Uingereza Kisha ofisi ndogo za Usajili wa Meli ziwe huko na meli za open registry zifuate Sheria za Tanzania na miongozo ya kampuni(Corporate Company) za washirika wetu Kama Liberia walichofanya.


images (9).jpeg


images (7).jpeg
 
Hong Kong unaifananisha na Dar es salaam kwenye kusajili meli.
Sijafananisha mkuu, Hong Kong ni Flag state na Dar es Salaam ni mji na bandari.

Hong Kong kama nchi wao ni Open registry, jamii Moja na Liberia, Marshal Island, Cayman islands, Panama na Zanzibar.
 
Back
Top Bottom