Private Maritime Security Companies (Makampuni Binafsi ya ulinzi wa meli)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,957
12,550
Private Maritime Security Companies (PMSC) haya ni makampuni binafsi ya ulinzi ambayo hukodiwa na mashirika ya meli, ambapo huweka walinzi (Security guards) wenye mafunzo maalumu kwenye meli na husafiri na meli kwa ajili ya ulinzi wa sehemu hatarishi na kuzuia wazamiaji, maharamia.

Makampuni haya kazi yake kubwa ni kupambana sehemu zenye hatari kwa kutumia silaha au kutotumia silaha, kutoa taarifa zinazoashiria hatari na namna ya kukabiliana na hatari hizo, kushauri, kushauri kampuni kuhusu mambo ya usalama na tahadhari za kuchukuliwa.

Miaka ya 2000 kampuni hizi binafsi zilianza kuenea kwenye shipping line za meli za Container na magari ili kupunguza uvamizi maeneo hatari na meli zinapokuwa nje ya bandari baadhi ya nchi tofauti.

Mafanikio
Meli nyingi ambazo hutembea na walinzi wa makampuni binafsi zimekuwa na rekodi nzuri ya kutovamiwa na maharamia sehemu hatarishi,kuweza kutambua via shiria vya hatari na kuzuia hatari yoyote ambayo ingejitokeza.

Changamoto
Kampuni hizi huajiri walinzi wa 5 mpaka 10 kwenye meli moja, endapo itatokea shambulizi kubwa la uvamizi idadi ya askari inakuwa ni ndogo. Hivyo kampuni hizi imeonekana kuwa ni suluhisho la muda mfupi katika masuala ya ulinzi na kukabiliana na maharamia.

Pili kampuni nyingi za ulinzi zimesajiliwa na nchi ambazo zina usajili huru wa meli (Open Registry/ Flag of Convenience) ambapo baadhi ya mataifa hawakubaliani na hii sheria.Mataifa mengine huogopa endapo itakuwa ni sheria kutakuwa na kudukuliwa kwa taarifa za siri za kiusalama.

Liberia ni nchi iliyosajili meli nyingi, na ndio zinapita maeneo hatarishi Duniani na makampuni mengi ya ulinzi wa meli binafsi yamesajiliwa kwa bendera ya Liberia na visiwa vya Marshall.

Mwaka 2011 nchi ya Italy ilipitisha sheria nchini kwao kila kampuni ya meli iliyosajiliwa pale inapofanya kazi kimataifa lazima iwe inatembea Walinzi binafsi melini, baada ya miaka kadhaa mbele haikuwa na nguvu tena.

Utaratibu endapo Meli yenye walinzi binafsi imefika bandarini nchi yoyote.

Meli yenye walinzi binafsi endapo ikafika bandari husika basi wakala wa meli(Ship agent) anatakiwa atoe taarifa kwa bandari na kuna utaratibu kulingana na nchi husika watakuja wanajeshi watakabidhiwa silaha zote na kwenda kuzitunza kwenye ghala la silaha. Na siku meli inapoondoka silaha zitakabidhiwa melini kama zilivyopokelewa.


Baadhi ya nchi zenye makampuni haya binafsi ya ulinzi ni Liberia,Mauritius na South Africa, makampuni haya hutumia vijana waliopita jeshini au wastaafu kisha huwapa mafunzo ya awali ya meli(Basic Safety Courses/Mandatory Courses), kisha hupewa mafunzo ya masuala ya usalama na njia za kutambua hatari, mafunzo ya silaha na namna ya kukabiliana na maharamia.

Watu wanaweza wakauliza swali
Kwanini meli hazipiti Pale walipo Houthi, makampuni binafsi ya ulinzi si kila meli inaingia mkataba nao. Hata baadhi waliongia mkataba na hayo hawawezi kupita kupambana na Houthi sababu ni meli moja huwa na walinzi wachache wastani ya walinzi 5.

Hapo Chini ni list ya kampuni binafsi za ulinzi melini (Private Marine Company Security) Ambrey ni kampuni maarufu sana kwenye hizi shughuli na ndio kampuni iliyobeba watu wa mataifa mbalimbali.


1.ALFA Marine Protection Ltd British Virgin Islands UAE

2.Al Safina Marine Management LLC

3.Ambrey Limited United Kingdom
4.Black Pearl Maritime Security Management Limited United Kingdom

5.Britannia Maritime Security Ltd United Kingdom

6.Diaplous Maritime Services Ltd Cyprus

7.ESS & SA Maritime B.V. The Netherlands

8.Hua Xin Zhong An (Beijing) Security Service Co. Ltd
China

9.Marine One Private Limited Sri Lanka

10.PVI Risk Management Pte. Ltd. Singapore

11.Sea Guardian S.G. Limited Greece
12.Seagull Maritime Ltd Malta United Kingdom


images (3).jpeg
images (2).jpeg
images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom