Meli ya Mirembe Judith kupunguza msongamano wa makasha bandari ya Dar es Salaam

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
06 August 2023
UWEKEZAJI KATIKA MELI MIREMBE JUDITH KUCHOCHEA MATUMIZI YA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Meli yenye uwezo wa kubeba makasha 600 iliyobatizwa jina MIREMBE JUDITH inayomilikiwa na kampuni ya kitanzania itakuwa inafanya kazi ya transhipment baina ya bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar

Video courtesy of Global TV online

Ujio wa meli hii utachangia kuongezeka kwa ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam kwa kuondoa msongamano wa makasha yanayoshushwa na meli kubwa kwa makasha yaendayo Zanzibar.

Pia itaongeza idadi ya meli kubwa zenye makasha yaendayo Zanzibar ambayo yatashushwa bandarini Dar es Salaam. Mizigo mingine ya makasha ya Zanzibar yaliyobebwa ktk meli kubwa imekuwa ikishushwa bandari ya Lamu Kenya.

Ujio wa meli hii ya Mirembe Judith itafanya safari ya makasha kuwa fupi kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.

Mkurugenzi wa bandari ya Dar es Salaam Bw. Mrisho Mrisho akizungumzia ujio huo ameongeza kuwa huo uwekezaji huo wa mtanzania ktk meli unaendana na mkakati wa bandari kuongeza ufanisi na idadi ya meli kubwa za transhipment kutia nanga katika bandari hii ya Tanzania.
1691316375929.png

Photo: Mirembe Judith vessel courtesy of marinetraffic.com

Kwa muda wa miezi mitatu mjadala kuhusu jinsi ya bandari za Tanzania zinavyoweza kuongeza ufanisi, wingi wa mizigo, makasha, idadi ya meli umekuwa ukiendelea na uchambuzi wa aina gani ya uwekezaji mchanganyiko unaweza kuongeza kwa ujumla wake wateja kutumia bandari za Tanzania.

The vessel MIREMBE JUDITH (IMO: 9141900, MMSI 677026000) is a Container Ship built in 1996 (27 years old) and currently sailing under the flag of Tanzania.
MIREMBE JUDITH is a Container ship built in 1996 by HAKATA SHIPBUILDING - IMABARI, JAPAN. Formerly was sailing under the flag of Panama. Formerly also known as ACACIA LAN, ACACIA LAN, CONFIDENCE, TIGER SPRING, EAGLE CONFIDENCE. It's gross tonnage is 5658 tons.
 
Kama kuna uhitaji vipi Azam hakuliona ? Maana tunajua mwepesi sana kuchangamkia fursa
 
Habari za kiuchunguzi zinabainisha kampuni kubwa ya kitanzania PMM Estates (2001) LTD yenye makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania inayohusika na ugavi, usafirishaji, bandari kavu na majenzi ndiyo ina miliki meli hiyo ya Judith Mirembe .

Ni habari njema kuona kampuni ya kitanzania ya watanzania ikionesha njia katika kubaini na kushiriki fursa za transhipment ya mizigo hivyo kuchagia katika uchumi na maendeleo ya nchi kupitia sekta ya bandari za baharini na corridors za usafirishaji pia mizigo kuchukukiwa na kufikishwa mlango hadi mlango End to End Solutions .

PMM Estates (2001) LTD is an inland container depot company (ICD) located along Nyerere road near CFAO motors in Dar Esalaam. We have been in the buisness of storing containers since 2010 with an excellent track record of customer satisfaction.

  • The company has sound experiences on handling and storage of goods of any size and complexities.
  • The company possesses efficient transport services through owned trucks and hired ones.
    The business premise is strategically position in vicinity to major transport routes.
  • On time processing of customers’ needs. PMM ICD processes containers at the time customer wishes.
    The process is fast due to commitment and specialist expertise of staffs.
    PMM handles a variety of containers with respectively specific equipment
 
Hongera Dada,Judith mirembe,much big up!

MESSAGE FROM THE PRESIDENT.

I have great pleasure in extending greetings and thanks to all our customers. I take pride in the introduction of PMM ICD which is one of the leading inland container depot firms in Tanzania.

We have accumulated immense experience and know how in the inland depot industry and have put strong emphasis on container handling services. Our professionalism in this particular field is based on the mission to provide refined services to all our clients.

PMM ICD is responding to new trade trends by placing more emphasis on building its logistics capabilties through improvement of fleet and investment in new facilities and other modes of transport.

I hope that this website will give you a better understanding of the services we offer to you. Regards,

DR. JUDITH IRUNGU MHINA Founder And Managing Director
PMMICD
 
Kuna mambo magumu nyie. Vp nafasi ya hao milembe mbele ya DP word

Wazawa pia wanaweza kama wakiaminiwa, mfano TPA walichagiza PMMCID walete meli kazi iendelee ya kuifanya bandari yetu kimbilio la wateja Zanzibar, Tanga, Comoros, Durban n.k
 
Kuna mambo magumu nyie. Vp nafasi ya hao milembe mbele ya DP word
Hao wanafanya kazi katika mazingira tofauti ,hao Dp world ni operator katika magati (Berths) na hiyo meli inadili na transhipments .


Mfano mzigo unaoenda Zanzibar unaweza kushushwa Dar hapo then ukafanyiwa tranship kwa kupelekwa zanzibar kwa hiyo meli , kumbukq mzigo ukiwa ni transhipment ina maana hapo Dar sio destination ila utapakiwa na kubadilishwa kweny meli nyingine ili ufike destination huko zenji basi hapo watakaofanyw huo mchezo ni wakina Milembe na meli yao.

Ila kumbuka transhipments zina umuhimu wake kwa vile port charges itapatikana pia kuongeza routes za meli kwa kuja meli nyingi , mfano zile zinazoenda Zanzibar moja kwa moja zinaweza kupitia hapo Dar kwa wafanyabiashara wanajua hii maana ni maelezo marefu ila zaidi kupata meli nyingi za kuja Dar ili watu waagizie mizigo ambazo mwanzo zilikuwa moja kwa moja zinaenda zenji.
 
Back
Top Bottom