Series (Special thread)

Series (Special thread)

Richard Alpert.. huyo jamaa si ndo yule ambae hazeeki?
Richard aliishi kitambo sana tangu miaka hiyo ya 1800s na hazeeki yupo vile vile. Kuna scene naikumbuka kipindi Benjamin Linus ndo anafika kisiwani yupo mdogo kabisa anakutana na Richard, jamaa yupo vile vile.
Linus anakua mpaka anafikia utu uzima jamaa yupo vile vile!

Jacob na Black Smoke si walizaliwa mapacha hawa?.. mama yao wakati anajifungua hakujua kama amebeba mapacha, akampa jina mtoto wa kwanza aitwe Jacob. Baadae wanaangalia vizuri kumbe ana mtoto mwengine, bi mkubwa akasema yeye ashatoa jina moja hatoi jengine!
Naona hata Ben asingemuua Jacob bado Richard angeweza kusurvive kwa muda mrefu zaiid pale kisiwan..
Nilifanikiwa kuimaliza lakin bado iliniacha na maswali meng sana.
 
Snowfall kali ilaa Changamoto matukio mengi hasa ya mauaji inakuwa kama Bongo movie yani Boom lishatokea huoni limetokeaje au imekuwaje...!! Nimemaliza season 1 ila kuendelea naona uvivu sana series za hivi hazinogi yani matukio ya kimafia ndo yananogesha series lakini yanaoneshwa eti tayari ishatokea.. Escobar ndo best series ya drug dealers aiseee
Snowfall mi niliishia season 1 tu tena kwa shida sana ..

Yaan haiamasishi kwenda season 2
 
Mzigo
20220317_110829.jpg
 
Nipo hapa nakodolea kitu murua taratibuuuu inaitwa AlRawabi School for Girls

kaseries flani ka kufurahisha kuburudisha yani una relax week end inaisha taratbuuuuu

Wazazi wenye watoto hii inawafaa sana kuna kitu kikubwa sana utajifunza ukiangalia hii series
 
Mhhhh! Yaishe mkuu maana ukiulizwa nini kimepooza hautaweza nijibu kwa facts bali utaishia kuongelea mtazamo wako na sio mtazamo wa wengine wengi tunaofatilia iyo series mpaka leo ipo season 5 na kama ingekuwa storyline imepooza it means wangeishia season ya 1 maana ile ni biashara lazima ilete faida na neno la mwisho hakuna series yoyote duniani iliyotoka ikapendwa na wote.
Baharia mweuc muache tu, ila snowfall imeingia kwenye top series ambazo nimetizama, huwa si mwepesi kukubali kitu ila dogo Franklin ile ni talent, namuona mbali sana huyu chalii
 
Kwenye series ya LOST kuna mambo ya ajabu sana ndani ya kile kisiwa nikikumbuka nabaki kushangaa tu:

1. Kwanza kisiwa hakipo kwenye ramani. Yani unajikuta tu umetokea.

2. Ukiingia hamna kutoka. Japo watu baadae waliweza kutoka baadae.

3. Hauwezi kuumwa ukiwa ndani ya kisiwa.

4. Wanawake wote wanaopata mimba ndani ya kisiwa wanakufa.

5. Sheria za physics hazifanyi kazi kabisa mule ndani.. kwa mfano unaweza ukarusha jiwe juu likachelewa au likawahi kufika.

6. Kuna jamaa kazaliwa miaka ya 1800 lakini hazeeki.

7. Kuna huyo mtu ambae haonekani.

8. Kama ulikuwa unaumwa ugonjwa wowote ukiingia ndani ya hicho kisiwa tayari ushapona!

Hatari sana.. ongezea jambo lililokustahajabisha kwenye hii series kama umewahi kuicheki.
Season 1 mpaka season 4 ya Lost, ni hatari sana.. dah umenikumbusha mbali sana, Kate na mzee Sawyer, good old days.. zilizoendelea niliishia njiani kwakweli, ile time travel ilinishinda
 
Season 1 mpaka season 4 ya Lost, ni hatari sana.. dah umenikumbusha mabli sana, Kate na mzee Sawyer, good old days.. zilizoendelea niliishia njiani kwakweli, ile time travel ilinishinda
Kuna twisting za kutosha mule kutoka kwa Desmond Hume.. ile nilimaliza mpaka Season ya 6 (final).

Series za zamani zamani story zake huwa ni kali sana.. ukianzia kwa 24, Prison Break, Breaking Bad, All Americans, n.k.

Na huyu mtunzi wa hii series ya Lost, Michael Giacchino ameandika movies na series nyengine ambazo ni kali. Kikawaida nikiiona mizigo yake lazima nipite nayo.
 
Kama kuna aliewahi kuiona Person of Interest au Alias aniambie ipi inanoga sana?
Nianze na ipi?
Na story zake kwa ufupi..
 
Kuna twisting za kutosha mule kutoka kwa Desmond Hume.. ile nilimaliza mpaka Season ya 6 (final).

Series za zamani zamani story zake huwa ni kali sana.. ukianzia kwa 24, Prison Break, Breaking Bad, All Americans, n.k.

Na huyu mtunzi wa hii series ya Lost, Michael Giacchino ameandika movies na series nyengine ambazo ni kali. Kikawaida nikiiona mizigo yake lazima nipite nayo.
Series zake nimeona Lost na Alias tu, movies ndio nyingi na yuko poa sana, mission impossible, Star wars, Jurasic park n.k

Zamani ilikuwa balaa mzigo wa greys anatomy mpaka leo ninao season 18 naenda nao tu.. series za siku hizi season 1 unaona kabisa mwisho unakuwaje au season 1 tu chalii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom