Mkuu mimi niliishia ile proad ananyongwa, nilihisi ndio mwisho kwani imeendelea?? Je ile iliyoishia jack proad ananyongwa ni season ya ngapi?
Mkuu yule siyo jack proad, yule anaitwa nicholas brody kwenye season ya tatu mkuu.
Na jamaa hakunyongwa waraabu waliwahadaa wamarekani tu, kwenye season ya 4 episode ya 7 Pakistan intelligence services (ISI) waliwakutanisha carrie na brody kwenye self house yaliokuwa makazi ya general wa jeshi la Pakistan.
Season ya 4 carrie anakuwa ni station chief kabul, Afghanistan, alipewa information ambazo hazikuwa sahihi na CIA station chief wa Pakistan Sandy Bachman, kuhusu uwepo wa gaidi aliyekuwa anawindwa na wamarekani kwa udi na uvumba Haissam Haqqani kwenye eneo ambalo halikuwa sahihi anaua innocent people waliokuwa kwenye harusi kwa drone. (Anafahamika kama drone queen)
Haissam Haqqani alikuwa ni mtu ambaye alitengenezwa Saul na Dar Adal kwa lengo la kumuyumbisha head wa CIA pale Langley,senator aliteuliwa na rais kuiongoza CIA. Hivyo Saul na Mwanae Dar Adal hawakuwa na kazi zaidi ya kupiga fitina.
ISI wanamtengeneza mme wa balozi wa USA pale Pakistan kuwa informer wa kuwapa taarifa nyeti juu ya mipango ya CIA pale Pakistan na alifanikiwa kuwaonyesha safe house za CIA.
Quin alipewa mission ya syria, carrie alifanikiwa kutega bomu la kumuua Hissam kwenye mlango wa gate lake, ile anataka kulipua general akamwambia usilipue angalia kwenye gari amekaa nani, kuangalia anamkuta Dar Adal amekaa siti ya nyuma wanapiga story. Carrie alibaki mdomo wazi.
Season ya 5 na ilikuwa ni Berlin, nimeshaielezea mkuu na 06 nayo nimeshaigusia.
Season ya 07 iliyoisha juzi. Warusi wamemfanya mbaya carrie kawa kichaaa. Lakini pia wamemchafua rais wa marekani ambavyo ameamua kuresign kwenye hiyo nafasi yake. Dar Adal bado yuko kwenye federal prison.
Homeland is my favorite show all the time.
Gideon Raff huyu mwiziraiel anajua kuandika story na kudirect.