Sijakuambia Actor sio muhimu bali msingi wa movie ni story/writer na director!!
Ukishakuwa na stori iliyoenda shule na director mzuri; unaweza kwenda pale Kariakoo na kufanya casting randomly na kupata crew mzima hamna hata mmoja aliyewahi kuwa mbele ya kamera hata kwa dakika moja!! Lakini pamoja na yote hayo, bado inaweza kutoka bonge la movie kwa sababu kuna director mzuri na story mzuri!!!
Huwezi kutafuta story/mwandishi na director randomly!!
Huyo Muigizaji atakayeshindwa ku-perform to expectation, hiyo under performance itatokana na mapungufu ya director kwa sababu director yupo pale, pamoja na mambo mengine, pia kuhakikisha maandishi (script) yanakuwa transformed into motion picture physically and emotionally and make it like real!
Kama maandishi yanasema Actor anatakiwa kukimbia kwa namna ya kuikimbia hatari basi Director anatakiwa kuhakikisha Actor anakimbia huku, physically and emotionally akionesha kwamba ni kweli anaikimbia hatari!! Hii ni kwa sababu, kwa mfano, anayeikimbia hatari na anayekimbia kwa mazoezi; hawa wanakuwa tofauti, physically and emotionally! Kwahiyo, nafasi ya muigizaji ni kuonesha hizo physical and emotional characteristics ili iwe kama kweli na pale penye mapungufu; director ndie anatakiwa kunyoosha hayo mapungufu na ndio maana, kwa wenzeetu waliokuwa serious, unaweza kukuta scene ya dakika moja inakuwa shot kwa masaa kadhaa
REMEMBER: Kabla acting crew haijaingia location lazima wafanye rehearsals mbele ya director wakianzia na table read...!!! Sasa kama Acting Crew imefanya rehearsals round kadhaa na bado Actor anashindwa ku-deliver; hilo sio kosa la actor tena bali director. Isitoshe, ni huyo huyo director ndie ame-approve hiyo shot yenye under performance...