Series (Special thread)

Mkuu vince, kama unakumbuka jinsi nilivyokua nakuuliza season 2 inatoka lini?

Niseme tu mie season tu sikuipenda kabisa mpaka nikajiuliza walikaa mda mrefu wakiandaa season tu afu haikua nzuri kama season 1.

Labda huenda mie ndio nimeona ni mbaya sasa hapa najiuliza hii season 3 mbona mapema hivi? Ngoja nione episode atlest 3 ndio nitoe hukumu yangu.
 
Narudisha mrejesho.. kiukweli hii ngoma mwanzoni nilianza nayo kivivu sanaa. Ilinichukua almost 1 week mpaka kuamua kuichukulia serious maana nilishaweka hadi mpango wa kuifuta, cha kushangaza jana nimeimaliza na ni ya moto sanaaa πŸ”₯ unaangalia mpaka mapigo yanaenda mbio.

Leo asubuhi nimeamua kuirudia upya ili nielewe vizuri sasa!

Aisee, shukrani sana kwa alie recommend. Kiukweli sijapoteza kitu zaidi ya kuongeza.
Ila wangeweka muendelezo tuone namna Cooper anavyoenda kum rescue Brand kule aliko kwenye other galaxy.
 
Kuna theory moja ya watazamaji tu maana walioandaa movie hawajathibitisha, kuwa huenda dr cooper alishakufa na safari yake kwenda kwenye space ni safari ya baada ya kifo

1. Kuna msemo alitumia tars kumwambia dr cooper "see on the other side" kumaanisha otherside of life

2. My Ghost, murphy alisema huwa ana ghost pia tukajakuambiwa kuwa dr cooper ndio alikuwa ghost wake 3. Big sleep metaphor , crew ya endurance walikuwa wakitumia kauli ya big sleep wakimaanisha hibernation ila kwa maana nyingine kifo kinaweza kuwa maana ya big sleep

3. The last thing you see, dr mann alimwambia cooper kuwa kitu cha mwisho mtu kukiona kabla ya kufa ni watu awapendao, kwa cooper itakuwa ni watoto wake hasa murphy na tukio aliloliona kwenye tessaract alipoingia kwenye blackhole ni kumbu kumbu za mwanaye, ukienda google nenda kasachi interstellar death thoery utaona kisha anza kuunganisha na matukio

Zipo sababu nyingi hadi kuhusu another dimensio, ni theory nzuri ingawa haijathibitishwa na waandaji wa movie pia kitu kingine watu wanachoamini huenda theory ikawa ni kweli ni aina ya movie anazotengeneza Nolan, ukiangalia inception kuishia na ile totem kuzunguka bila kudondoka kuashiria huenda dicaprio alikuwa yupo kwenye ndoto na mkewe alikuwa sahihi na hajafa, au movie ya Memonto, Tenet zote zinaishia na sintifahamu, na huenda ikapatikana theory ukaona movie inahusu hivi sio vile.
 
Kama umeipenda hiyo.
Jaribu hii kama hujawahi kuona

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…