Wakuu naomba majina ya movies ama series zile zime base kwenye true story hasa zile za wanamichezo mbalimbali. Movies ama series za namna hiyo nimetokea kuzielewa sana.
Nimetizama movie ya RISE hii inahusu maisha ya mchezaji Giannis Antetokounmpo anaekipiga katika kilabu ya kikaku Milwaukee Bucks nchini Marekani katika ligi ya NBA. Hii imeelezea maisha yake yote aliyo pitia mpaka kufikia hatua ya kucheza katika ligi kubwa na maarufu duniani, ni movie nzuri sana.
Pia nimetizama movie ya BIG GEORGE FOREMAN, hii imezungumzia maisha ya mwanamasumbwi Big George, huyu mwamba alikuwa ni noma sana. Huyu jamaa ndio alifanya nikamkubali Mohammed Ali, awali sikuamni kama kuna mtu anaweza mpiga Big George kwenye ulingo mpaka pale Ali alipo nisahihisha makosa yangu. Big George alikuwa na ngumi nzito sana, kiukweli sijawahi kuona. Mohammed Ali alipo mpiga Big George kule Zaire moja kwa moja nili mkubali Ali. Mohammed Ali ndio chanzo cha kumdunda Big George mpaka kumtoa kwenye masumbwi na kuhamia kwenye uchungaji huko. Akaja kurudi baada ya miaka 10 kufuatia kushuka kiuchumi na kutwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya pili.
Movies za namna hii huwa zinanisisimua sana na ninazipenda kupita maelezo, naombeni nyingine tafadhali.