Kwa nini unacheka?
Nimekumbuka mbali sana,
Nikiwa naelekea Istanbul nipo na jamaa angu(comrade), tunakatiza Atlantic Ocean, baada kama ya lisaa nilianza kuhisi hali si nzuri, pilot akatangaza hali si shwari kwani kuna mechanical issue na hawajui haswa tatizo linasababishwa na nini, jamaa akasema hawajui kinachoendelea zaidi ya kufanya water landing.
Ndege nzima ukimya ulitawala kulikuwa kuna watu wamelala ilikuwa usiku, naona flight attendants wanapita huku wanaenda kule sasa ndio walikuwa wanawachanganya abiria mimi nikiwemo kwani captain alikuwa hajatoa taarifa zaidi, yule mshikaji wangu alikuwa anatukana hovyo, anarudi huku kuangalia dirishani sijui alitaka apitie pale
halafu anatukana mwenyewe " fuk,shit, fuuuuuk, nope it's ok, fuk, fffffuk" asee we acha tu, mimi hapo moyo unapiga si kawaida, ku survive water landing ni bahati sana , we acha tu, sikia kwa mwingine tu, unaweza kujisaidia
Thats why nimewaza hiko kisa baada ya kuona hio ndege ndio tulikuwa tumepanda A340,
ni kama umenirudisha nyuma sana.
Thanks.