Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Ila Mwanaume kuweza kula hela ya Mchepuko itakuhitaji kutumia mbinu kubwa mno, ila wao Sasa wakihitaji utasema waliiweka
Teh kuna siku nilikuta mahali wanasema walimu wa kike wengi wanapigwa sana na wanaume. Wengi wanawarubuni wawachukulie mikopo afu wakishapewa mapene wanawakimbia. Kuna wanaume ni makauzu wewe
 
Mmmh bado una moyo mzuri aisee. Wenzako mwanamke ukiitwa tu ka dinner, wakati anakunywa soda, anasikia kidume anauliza "vyumba vipo muhudumu? (Natania mweeh)
Bora anipige mzinga nimfungulie Biashara ili kama ni Kodi alipe kupitia biashara niliyomfungulia lakini sio hii mara Kodi, mara Ada n.k inakera
 
Kwa kweli tunaangamizwa kwa kukosa maarifa. Kuokoka au kuabudu kanisa fulani sio immune ya kutokutenda dhambi; ni vile tayari nafsi yako tayari umeshaitengeneza inakuwa "conscience" kuomba rehema na toba pale unapotenda dhambi. Ndiyo maana sio tu waumini; hata Watumishi wengi wa Mungu wanatenda dhambi; hadi mimi najiona malaika kwa muda. " for all have sinned and fall short of the glory of God". Fact kwamba umeokoka, haimaamishi kwamba ndiyo umeshafika mbinguni sasa; wapo wengi walioacha wokovu njiani.

Fact kwamba mtu hajaokoka leo, haimaanishi kwamba hawezi akaokoka kesho. Tena kuna watu wanaweza wakaokoka nyuma yako, na wakasimama na Mungu imara kuliko hata wewe. "Anayesamehewa sana, hupenda sana". So kuna watu ambao leo unaweza ukawaona ni watenda dhambi wakubwa; lakini siku wakitubu na kusamehewa; humpenda Mungu sana na kumshika sana.

Ukimuona mtu hayupo kwenye njia salama; unamuonya na kumuelekeza kwa hekima. Sio unafika kwa mtu afu unaanza kumwambia "huko unaposali umepotea ndugu yangu, hakuna Mungu". Au ndiyo wale wanakutenga kabisa kwa sababu huamini pamoja nao. Humsaidii mtu unayemuona anapotea kwa kumtenga Wakati mwingine matendo yako mema, yanaweza yakawavuta watu wakaja kwa Mungu wako. Tusipende kujiona watakatifu sana, ilhali kila mmoja wetu anajua matendo yake anayoyafanya huko sirini. "Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke". (1 Korintho 10:12)

Na hii ni kwetu generally; tuna katabia ka kuona wale wanaofanya dhambi tofauti na za kwetu ndiyo watenda dhambi sana kutuzidi. Yaani unajiona wewe ni bora kwa sababu unasengenya na mwenzako ni mzinzi; but mwisho wa siku ninyi wote wawili mnastahili mauti kama mshahara wa dhambi zenu. So kila mmoja ajichunguze, apigane vita yake taratibu. Dhambi za mtu mwingine hazikufanyi wewe kuwa mtakatifu.

"Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu". (Mathayo 21:31)
Dada yangu nashukuru kwa maelezo mazuri sana, nakupongeza kwa kuishikilia imani sawasawa na nakutakia au nakuombea ikawe hivyo kwako kwa kila hali na kwa kila wakati.

Unaweza ukawa ni moja ya watu walio okoka wenye kujitambua na kujielewa, ila nakuomba ujue wengi sana wanaojiita wameokoka ndani yao wana mapungufu mengi mno kiasi cha kuwa ni heri wale wanao hesabika ni waovu wana matendo dhahiri mema mengi.

Yote ya yote ni kuendelea kuishikilia wokovu na kuihubiri injili kwa kila jukwaa tutakalo pata.
 
Teh kuna siku nilikuta mahali wanasema walimu wa kike wengi wanapigwa sana na wanaume. Wengi wanawarubuni wawachukulie mikopo afu wakishapewa mapene wanawakimbia. Kuna wanaume ni makauzu wewe
Niambie nitumie mbinu ipi kuweza kula hela yako Mama Mchungaji?

Fanya tuchange nikufungulie biashara ila nitakwenda China kukufungia mzigo wa Dukani 🙈🏃🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom