Heaven Sent
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 32,717
- 98,375
Kwa kweli tunaangamizwa kwa kukosa maarifa. Kuokoka au kuabudu kanisa fulani sio immune ya kutokutenda dhambi; ni vile tayari nafsi yako tayari umeshaitengeneza inakuwa "conscience" kuomba rehema na toba pale unapotenda dhambi. Ndiyo maana sio tu waumini; hata Watumishi wengi wa Mungu wanatenda dhambi; hadi mimi najiona malaika kwa muda. " for all have sinned and fall short of the glory of God". Fact kwamba umeokoka, haimaamishi kwamba ndiyo umeshafika mbinguni sasa; wapo wengi walioacha wokovu njiani.
Fact kwamba mtu hajaokoka leo, haimaanishi kwamba hawezi akaokoka kesho. Tena kuna watu wanaweza wakaokoka nyuma yako, na wakasimama na Mungu imara kuliko hata wewe. "Anayesamehewa sana, hupenda sana". So kuna watu ambao leo unaweza ukawaona ni watenda dhambi wakubwa; lakini siku wakitubu na kusamehewa; humpenda Mungu sana na kumshika sana.
Ukimuona mtu hayupo kwenye njia salama; unamuonya na kumuelekeza kwa hekima. Sio unafika kwa mtu afu unaanza kumwambia "huko unaposali umepotea ndugu yangu, hakuna Mungu". Au ndiyo wale wanakutenga kabisa kwa sababu huamini pamoja nao. Humsaidii mtu unayemuona anapotea kwa kumtenga Wakati mwingine matendo yako mema, yanaweza yakawavuta watu wakaja kwa Mungu wako. Tusipende kujiona watakatifu sana, ilhali kila mmoja wetu anajua matendo yake anayoyafanya huko sirini. "Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke". (1 Korintho 10:12)
Na hii ni kwetu generally; tuna katabia ka kuona wale wanaofanya dhambi tofauti na za kwetu ndiyo watenda dhambi sana kutuzidi. Yaani unajiona wewe ni bora kwa sababu unasengenya na mwenzako ni mzinzi; but mwisho wa siku ninyi wote wawili mnastahili mauti kama mshahara wa dhambi zenu. So kila mmoja ajichunguze, apigane vita yake taratibu. Dhambi za mtu mwingine hazikufanyi wewe kuwa mtakatifu.
"Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu". (Mathayo 21:31)

Kwa wale wanaojilewa wako vizuri wengi wao.
Ila wake wanao jihesabia bora kuliko wengine wote ambao hawako kwenye makanisa yao hai ndio mtihani.
Kwa mfano mtu anasalia Siloam anamuona yoyote asiye kua Siloam ni mwenye kupotea, kadhalika na wanajiita walokole huwaona wote wasio fungamana nao wamepotea.
Hapo ndio kwenye shida na walokole na wenye kujiita wameokoka.