Selfika na JF: Snap it. Show it

Si haki sawa jamani au??

Lazima wife atoe go ahead na huo ndio uanaume.
Haha i thought kwenu you guys uanaume ni kufanya vile unataka, bila kujali wife atajisikiaje! Ndiyo maana nashangaa hayo ya kumuomba ruhusa wife yameanza lini maana mie siku zote najuaga wanaume wa kiafrika huwa mpo huru tu na hampangiwi lolote haijalishi mmeoa au hamjaoa, no?
 
Ohooo!! Nishaharibu! Kumbe nilikuiba kweli [emoji2305][emoji2305][emoji2305] Nishalizua kwa huyu mzee! Ngoja nikalale mapema! [emoji125][emoji125][emoji125][emoji377][emoji377][emoji377]
Siku zako zinahesabika. Unamchukua mjukuu wangu halafu unakuja kujitapa hapa? Real!? I am gonna knock you out [emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Wakuu.

Japo hatujuani lakini tunaishi kama ndugu. Na hakuna kitu cha thamani kama kuombewa na kutakiwa mema na mtu usiyemfahamu. Maombi ya aina hii huwa na nguvu sana kwa sababu huwa ni maombi ya kweli yasiyo na ajenda wala mawaa.

Napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wote mlioniombea na kunitakia mema; na uponaji wa haraka. Japo Covid hii (tena Delta mwenyewe) ilinijia kwa nguvu sana lakini kwa maombi yenu na upendo wa Mungu nimepona. Bado tu kakikohozi ka mbali lakini hata nikikimbia kifua hakiwaki moto kama hapo kabla...na viuchovu uchovu tu vya hapa na pale. Kwa jina la Yesu naamini kuwa nimeshapona [emoji1545]

Sikuweza kumjibu mmoja mmoja lakini kwa umoja wenu napenda sana kuwashukuru mno 9.8ms squared, Heaven Sent, mahondaw, Makiwendo, Saint Anne, T 1990 ELY, Tinsley, Gregory 2000, Karma, Kashaija72, Chakorii na mawardat.

Asanteni sana wapendwa na Mungu Awalinde na kuwabariki sana. Hapa nilipo ni kama naishi peke yangu lakini kupitia kwenu nilijiona kama nina jeshi kubwa la watu wanaoniombea na kunitakia mema.

Hebu Mungu Akatubariki sote na mwaka huu mpya ulioanza ukawe wa mibaraka tele; na kila mmoja wetu akaweze kutimiza ndoto zake na malengo aliyojiwekea.

Nawashukuru sana [emoji1545][emoji1545][emoji1545]


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…