Ahsante,,,ya bamia unatumiaje?,nielekeze
Mahitaji
[emoji261]Bamia kumi (10)
[emoji261]Mafuta ya maji (African Black castor oil au coconut oil au olive oil)
[emoji261]Juice ya Tangawizi
[emoji261]Asali
Jinsi ya kuandaa
[emoji263]Osha bamia zako vizuri kuondoa uchafu wote
[emoji263]unaweza kukata kata kuwa vipande vidogo vidogo au ukamenya tu (kuexpose undani wake)
[emoji263]Weka kwenye sufuria yako safi
[emoji263]Ongeza maji kiasi (kikombe kimoja au viwili vinatosha) na ufunike
[emoji263]Chemsha kwa dakika 10 hadi 15 mpaka ile gelly au ute wa bamia uwe umetoka wa kutosha
[emoji263]Epua na uache ipoe kwa dakika kadhaa
[emoji263]Baada ya hapo chuja kuondoa vipeke na upate gelly tuu
Kama unatengeneza steaming
[emoji263]chukua ute ulioupata gawanya mara mbili
[emoji263]Nusu ya kwanza changanya na tangawizi na asali na mafuta yoyote ya kimiminika (hasa Castor oil)
[emoji263]Baada ya kuosha nywele kwa shampoo (hakikisha nywele zako ni safi) paka mchanganyiko kwenye nywele zote
[emoji263]Vaa shower cap au steamer na ukae kwa dakika 30+
[emoji263]Osha kwa maji mengi
[emoji263]Chukua ule mchanganyiko uliobaki changanya na mafuta kijiko kimoja hapa utakua umepata leave in conditioner
[emoji263]Nywele zako zikiwa mbichi na safi pakaa vizuri kuanzia kwenye ngozi hadi kwenye ncha.
[emoji263]Chambua vizuri nywele zako kidodgo kidogo kuhakikisha imeingia vizuri kwenywe nywele zote.
[emoji263]Unaweza kusuka mabutu (bantu knots) au twists za njia mbili au tatu au nywele za mistari kawaida nywele lazima ziwe na unyevu kabisa.
[emoji263]Ukiona zinakauka unanyunyiza maji tena.
[emoji263]Ukimaliza acha zikauke vizuri utaendelea kupaka mafuta yako kama kawaida ili kuzifanya zing’ae.
[emoji263]Ukifumua unapata mawimbi mazuri unaweza kubana utakavyo nywele zako.