Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

C6D457AD-76CE-40B9-A9E9-E4AAE6E5B677.jpeg
46A958D8-1A3E-4B48-A4F9-7AD39B7AA4AB.jpeg
66DE4D76-850E-4C79-B81D-6A80B2E7E49B.jpeg
E639D583-9941-4A51-8084-67E3B595E8AF.jpeg
 

Ila Morogoro kubwa jamani daah

Yeah Mungu akijalia na yeye mwenyewe akiwiwa basi tutafahamiana! Haya mambo ya kusambaziana picha ndiyo yanatuponza wengine mi nimejipostia zangu status mtu anaiba anasambaza mwisho wa siku mi ndiyo naonekana mbaya sema nashukuru Mungu alinielewa tukayamaliza!
Haki Morogoro ni kubwa kuliko Tanzania.jamani nilikaa kwenye gari kutoka dar to moro Town..moro Town mpka ifakara,ifakara tu mlimba.mlimba tu ndani ndani huko..jamani jamani waaaahiii uvumilivu ukanishinda ikabidi nimuulize jirani yangu “samahani dada eti tunaenda mbinguni”kha!!
Morogoro ndani ndani huko kama barabara ni mbovu aise ni bora kusubiri jua liwake barabara ichangamke kwanza maana...

Sasa ngoja nikuchekeshe😁😁😁 siku hiyo akati narudi mvua ilikuwa inanyesha niko kwenye boda natoka kijijini huko kwenda mlimba stand nikastuka boda anapunguza mwendo nikamuuliza Chief Vipi mbona umepunguza mwendo?akasema dada kuna mteremko na utelezi mkali hatua chache ..hapo mvua imekata kama dk 10 kumbuka😁😁😁hata kabla sijamaliza kutafakari itakuwaje...nikajikuta niko chini na udongo ulivyo wa mfinyanzi...loh hapo Naendelea kuserereka tu usisahau niko juu ya kilima...napiga jicho kushoto na kulia simuon boda wala boda yenyewe😆😆😆😆

Ikabidi sasa nitumie mbinu za kivita na za kimkakati kuzuia kuserereka,kibegi kipo juu juu kama antena 😁😁😁(jamani...)
Nikanasa,😜😜😜niko katikati ya giza totoro kumi na moja kasoro hiyo katikati ya mlima ikabidi nimuombe boda nae atumie mbinu za kivita ili asiendelee kuserereka akaniacha mwenyewe kilimani 😂😂😂 wooooiii namkuta chini kule amekula tope matata sana hakuna wa kumpa mwenzie lawama.ilibidi kubadilisha nguo nilipofika stand😄😄😄na huo ndo ulikuwa utalii wangu wa ndani..khooooo

Tuondelee kuomba uzima na afya tutakuja kuonana nao tu.🧚‍♀️🧚‍♀️

Huwa sifurahishwi na watu kugombana gombana aise..kama mmeelewana ni vyema kabisa binafsi ninalifurahia hilo..ona jinsi ilivyovyema na kupendeza...ndugu wakae pamoja kwa umoja.🤛🤛🤛
 
Back
Top Bottom