moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 156,152
- 770,267
Hadithi inasisimua sana.Haki Morogoro ni kubwa kuliko Tanzania.jamani nilikaa kwenye gari kutoka dar to moro Town..moro Town mpka ifakara,ifakara tu mlimba.mlimba tu ndani ndani huko..jamani jamani waaaahiii uvumilivu ukanishinda ikabidi nimuulize jirani yangu “samahani dada eti tunaenda mbinguni”kha!!
Morogoro ndani ndani huko kama barabara ni mbovu aise ni bora kusubiri jua liwake barabara ichangamke kwanza maana...
Sasa ngoja nikuchekeshesiku hiyo akati narudi mvua ilikuwa inanyesha niko kwenye boda natoka kijijini huko kwenda mlimba stand nikastuka boda anapunguza mwendo nikamuuliza Chief Vipi mbona umepunguza mwendo?akasema dada kuna mteremko na utelezi mkali hatua chache ..hapo mvua imekata kama dk 10 kumbuka
hata kabla sijamaliza kutafakari itakuwaje...nikajikuta niko chini na udongo ulivyo wa mfinyanzi...loh hapo Naendelea kuserereka tu usisahau niko juu ya kilima...napiga jicho kushoto na kulia simuon boda wala boda yenyewe
Ikabidi sasa nitumie mbinu za kivita na za kimkakati kuzuia kuserereka,kibegi kipo juu juu kama antena(jamani...)
Nikanasa,niko katikati ya giza totoro kumi na moja kasoro hiyo katikati ya mlima ikabidi nimuombe boda nae atumie mbinu za kivita ili asiendelee kuserereka akaniacha mwenyewe kilimani
wooooiii namkuta chini kule amekula tope matata sana hakuna wa kumpa mwenzie lawama.ilibidi kubadilisha nguo nilipofika stand
na huo ndo ulikuwa utalii wangu wa ndani..khooooo
Tuondelee kuomba uzima na afya tutakuja kuonana nao tu.
Huwa sifurahishwi na watu kugombana gombana aise..kama mmeelewana ni vyema kabisa binafsi ninalifurahia hilo..ona jinsi ilivyovyema na kupendeza...ndugu wakae pamoja kwa umoja.![]()
Ila daaa!! Mkoa wa Morogoro ni mkubwa sana.
Tumetoka Dar saa 12 asubuhi tukaingia Moro mjini saa 2:00. Ifakara saa 7:30, Mahenge saa 1 usiku, Mwaya saa 4, Iputi saa 5, Ilonga Selous Game Reserve saa 6:30 usiku.
Mkoa huo huo mmoja unatembea masaa kibao















