Selfika na JF: Snap it. Show it

uwe kama moja tena jameni πŸ™†β€β™‚οΈ πŸ™†β€β™‚οΈ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
ila hiyo ni kwa sababu unajilinganisha na wengine...jilinganisha na wewe mwenyewe ndio itapendeza zaidi mfano kwenye hilo la kupunguza mwili
 
Ila Kuna kauli sijaipenda
Hiyo ya tecno Aiseee...Mara picha zinatoka vibaya...Sasa si Ni zao na wameridhika nazo ndio maana wakapost.

Kutumia iPhone kusimfanye mtu amdharau mtumiaji wa Samsung infinix au tecno...Ni priority tu jamani...hatuwezi kulingana.

Pia uzuri wa mtu upo machoni pa mtu... mambo ya kuanza kuponda wadada wa watu bila sababu za msingi sio uungwana.
Kama girlfriend wako Ni malaika kwako isiwe sababu ya wewe kuwakandamiza wasichana wengine na kuona hawafai...kuna wanaume wanaowaona wanafaa.
Na nyie wadada muache kuponda girlfriends za watu jamani lol

Mmezidi na nyie....jifunze kupunguza maneno mdomoni.
Ulimi huponza kichwa.

Pia mtu kukaa muda wote humu sio Kama Yuko useless au Hana kazi.
Kazi Ni kazi,haijalishi kubwa au ndogo zote Ni kazi.
Acheni kuona watu hopeless kisa wanashinda humu...kila mtu na priority zake...wengine jf Ni kama rafiki kwao.
It's a matter of choice &priority.
Kuna watu wapo humu nawajua Wana kazi na hela zao za maana...lakini hata siku moja hutawakuta wakikashfu watu

Jifunzeni kuongea na watu vema.
Hii jf Ina Watu wengi,waaminifu ,wema,wazuri...
Kupitia hii unaweza tengeneza undugu ujamaa na urafiki.

Tudumishe upendo,tafuteni Sana kuwa na amani na watu wote.
Heshima Ni kitu Cha bure
Jifunzeni kuongea lugha nzuri.
Ukijibu vizuri ama kukaa kimya hutakatika mkono Wala kichwa.

Samahani kwa nitakaowakwaza.
Ni maoni yangu tu.
 
Volume ipo sawa kabisa. Wise words
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…