Ni sawa nasubiri kunyooshwa na huyo Mungu mwenyewe muweza wa yote, mie ni binadamu sijakamilika huwa nakosea hata ikiwa nje ya LGBT ni mkosefu pia, na kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.
Sijakataa kuambiwa ukweli pale napokosea wala sidhani km naogopwa ndani ya hii forum, maan hata mie mwenyewe hakna ninaye muogopa.
Nafuata misingi na taratibu zote za hii forum, na sijawahi kukiuka, km ningekua navuka mipaka basi mamlaka husika inge deal na mie ipasavyo, kulingana na kosa lenyewe.
Na kuhusu hili la picha za jana hujui chanzo ni kipi, labda ungeuliza vizuri ueleweshwe, mie n mstaarabu san najua mipaka ya mawasiliano, kuna muda personal attacks zinakuja kwangu na matusi, kejeli na maneno yasiyofaa, huwa najibu kwa hekima tyuuh japo ninayemjibu lazima akwazike.
Kuhusu malezi na misingi ya dini, ni sawa nilikua napoteza muda, sidhani kwa hilo km kwako ni tatizo. Hakuna mwanadamu yeyote aliyekuwa mkamilifu, na hakuna jipya chini ya jua. Pia vitu na viumbe wote wema na wabaya wote ni wa Mungu, maana viliumbwa na yeye.
Hivyo niseme kila mtu ana uhuru wa kuishi vile anavotaka, pasipo kukiuka kanuni, taratibu na sheria za nchi zilizowekwa.