Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Hapakui ..

Mm Nina viwanja vingi Sana njia ya kibaha Ila sijafikiria kununua sijui kisemvule wala chanika.

Ila haraka haraka sehemu ya kununua kiwanja ni GOBA,MBEZI,KIGAMBONI
Nitakuja ndugu yangu unigawie na mie hata kwa bei nafuu nipate hata pakuweka vyumba viwili, najua hata mashamba utakuwa nayo huko.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Tangu ameingia Magufuli na Sasa mama Samia,ikulu kumekuwa kwa kikuda Sana.

Imagine wameziba hadi kuta za fences ili mradi tu wapita njia wasione wale tausi mle ndani. Kule chini baharini ndiyo balaa,ukienda hata kwa kupotea njia utarukishwa kichura hadi makende yalalamike kwenye suruali kmmk.
Yule jamaa alikuwa mwoga sana

Lengo lake alitaka akae milele hivyo akaona akiacha pawe wazi watamtoa na ndo maana alikimbilia Dodoma kujificha, akaona haaptoshi akaenda kwao
 
Za jioni

Miaka 20 Dar sijawahi kufika maonesho ya Sabasaba.

Wapi haujawahi kufika au unapasikia kukaa kote Dar?

Mbopo napasikia.

Kina sehemu inaitwa king'ong'o kwa kweli hapa hapana sijawahi kufika.

Kijichi.

Kivule.
Lupaso...Kwa Mkapa
 
Dar kubwa sana, sidhani kama kuna mtu ashawahi kufika kila kitongoji...
Nilikuwa mzurulaji sana na hadi naondoka Dar miaka ya tisini baada ya kuishi hapo takribani miaka kumi nikiwa nina gari yangu binafsi bado sikuimaliza yote wakati huo. Leo hii Dar imepanuka sana siaminia kama kuna mtu anaweza kuja hapa na kutamka kuwa anaijua Dar yote hata angekuwa mzurulani kunizidi enzi zangu.
 
Sijafika maramba mawili, kifuru, chamazi, kivule, chanika, goba kulangwa, kidzudi
 
Back
Top Bottom