ISIS
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 96,072
- 858,587
Kama kuna mwarabu wa kweli anapitia uzi huu..., basi ataendelea kushangaa sana sisi waafrika tulivyo wajinga... Na labda ataona kwa kweli tunastahili kutendewa hovyo kama wanavyowatendea dada zetu wanaokwenda kufanya kazi huko...
Hivi inawezekanaje sisi kujadili uzi huu ambao uko very specific juu ya UKATILI WA WAARABU..., halafu badala ya kushauri, au kulaani wanayofanyiwa dada zetu, eti sisi tunaanza utetezi wa kijinga..., Oooh.., hata wazungu hawatupendi..., Oooh..., hata watanzania wakatili...
Hoja aliyoleta mwenzetu sasa itapoteza maana kabisa ..., kwa sababu ya ushabiki maandazi... Kwa nini tusitoe ushauri namna ya kupunguza madhila haya kwa watu wetu wote wanaokwenda kutafuta ajira huko ughaibuni..? Kwa nini tusifikirie sasa kutunga sheria ya kulinda UTU wa watanzania popote pale walipo duniani... Nafikiri haya ndiyo yangekuwa mambo ya sisi kujadili badala ya kutoana mapovu kulinda "mabwana" zetu..
kweli kabisa! na tukumbuke asiyependa kwao ni mtumwa....na asiyependa asili yake na watu wake ni mtumwa kweli kweli!