Nadhani unaumizwa na ukosefu wa ujuzi wa sheria za Kimataifa na pia kung'ang'ania kuitetea Israeli, nashuku, kwa sababu za kidini.
Ingekuwa vizuri- na hili hufanywa na watu wote wenye akili- kufanya utafiti kabla ya kuandika!
Mkuu Sijali , angalia post yako no.132.
Kwani ni vita tena aisee duuuh!!??
Pole aise, sasa kama wahitaji kujua kuwa watunga sheria ndiyo wavunja sheria kama wewe unavyojinadi kuwa hakuna wahamiaji haramu, hebu nenda nchi yoyote hapa hapa Afrika mashariki yetu [tuseme wewe ni Mtz nenda katika nchi wananchama hao watano] bila vibali uone utakuwa nani baada ya kukamatwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari.
Pili, usikalili kuwa dunia ilikuwa na msingi huo wa kuhama hama kila siku, nyakati zinabadilika na sheria zinatungwa mpya kulingana na mahitaji ya watu '' any society is dynamic and not static, Always we are in motion.
Hapo elewa kuwa UNHCR hawana uwezo wa kuilazimisha nchi kupokea au kuwatunza wahamiaji wawe halali, haramu au wakimbizi kwa nguvu pasipo makubaliano.
mf. Tz yenyewe ilishawahi kushirikiana na UNHCR kuwaondoa wahamiaji hao hapo Tz, ni hivi karibuni pale Nkurunzinza alipongangania kuwa rais wa Burundi kwa awamu ya mara ya tatu maana serikali ya Tz ilisema warudi kwao wakanze taratibu upya. Sasa wawe jina lolote utakalo waita halali au haramu ila bado kuna uhuru wa nchi na sheria ni lazima zifuatwe
Hao wahamiaji Tz iliowaondoa ni wa Burundi, wao walipitia Rwanda kabla ya kuja Tz kwa sheria ya UNHCR/UN mhamiaji [ambaye hapa ni mkimbizi] haruhusiwi kupitia nchi nyingine na kuhifadhiwa katika nchi ya nyingine. mf. wewe uko nchi 'A', unapitia nchi 'B' ili ukapate hifadhi nchi 'C' , hicho hakiruhusiwe. yaani Burundi hadi Rwanda kisha uje Tz kwa hifadhi hiyo huwa haipo na hakuna, sasa kama UNHCR wenyewe wanatambua hilo na ujue wanawaita kuwa hao ni wakimbizi/wahamiaji haramu UNHCR wenyewe kwa sheria yao na ya nchi zinawaona kuwa ni haramu.
Haa haaa ,, nicheke kidogo,,, Hamia basi bara la Ulaya au Amerika ya Obama ukutane na Trump siku akiwa Rais wa USA utajielewa utakuwa wapi baada ya kudakwa..
Tatu, mimi nimesoma na kuelewa vizuri mada za uhamiaji [shuleni, tafiti na washa mbalimbali nimeshiriki], sheria za ushirikiano wa kikanda [ yaani regional integration] kwa hiyo usifikili kuwa naandika na kuongea kutoka katika anga, au hadithi za abunuwasi hapana fikilia mara mbili angalia mantiki nilizokuandikia.
Pia, ukisema Israeli na dini sina hata chembe moja ya uandishi iliyoonesha kuwa nawatetea Israel kwa walichofanya na siyo sabbau ya dini; ila tambua kuwa wao wana haki kama nchi huru yeyote ile duniani [ nchi ya Israeli] ya kusema kuwa hawataki wahamiaji wawe halali au haramu, kwa mfano wahamiaji kwa nini wasiende Syria, Iran, Sudan, Palestina, Iraki au hata hapa Tz, kwa nini walazimishe kwenda wasipotakiwa, kwa nini wang'ang'anie Isaeli?
Mfano, Uingereza walikataa kuzungumzia wahamiaji haramu mimi nawaita hivyo kuwa ni haramu kwa sababu hawana hati za kisheria kuwa huko wanakohitaji na kulazimisha kuishi.
Tena fungua akili yako uone vyema na kwa upana na marefu, Kwa mfano, ni mara ngapi waethiopia hapa kwetu Tz wamekamatwa na kuwekwa ndani ili warudishwe kwao, jela/rumande ni kwa sababu ndiyo mahala salama kwa muda huo kabla ya kurudishwa kwao walikotoka hakuna jingine zaidi ya hapo.
Na kama unasema hivyo unamaanisha kuwa hujui usemacho, rudia hata Historia ya Afrika uone ni jinsi gani jamii zilikuwa zinapigana ili kulinda mipaka yao isiingiliwe na watu wa jamii zingine, hapo walichokipinga ni wahamiaji wa jamii moja kuja katika jmaii/himaya nyingine kwa njia haramu, ila ziko jamii zingine zilizokubaliana katika mambo ya mipaka na kuvunja mipaka na kuondoa mipaka ya watu kutembeleana ila ni kwa makubaliano rasmi siyo kuamka tu kama nyumbu na kuanzisha safari ya ugenini tena kusikojulukana.
Kwa hiyo usikalili kalili tu na kujibu bila kuchunguza mada vizuri.
Mfano, watu wengi wako Isreali wanasoma, wanafanya biashara, wanafanya kazi ila kwa vibali maalum na siyo vinginevyo kama hao waliopitia katika jangwa pasipo hata barabara ama kituo cha uhamiaji wataka wafanyweje?.
Pia, wewe wataka kutuaminisha katika uhuru wa watu kutembea popote bila mipaka, hicho hakipo tena umoja wa ulaya [EU] wenyewe ilikuwa ni shughuli ngumu sana kukubali wahamiaji au wakimbizi kwa kulinda mipaka na nchi zao na hao hao ndiyo waanzilishi wa haki na sheria za wahamiaji. Angalia, hawakupigwa na polisi kule nchi za ulaya? Baadaye ndiyo wakarudi kuwapokea tena waliwachangua wa kuwapokea mf. ujerumani haikuwachangua kama njugu?
Tena hawajapokelewa wote, ni kwa kuchambuliwa kwa vigezo wameviita migrants with merits mf. Ujerumani ilichukua wanaoweza kufanya kazi yaani wataalamu pekee/educated, kwa nini vigezo viliwekwa ? Jibu hawatakiwi kule maana siyo kwao.
Tena unaandika kitoto sana , unasema kuwa dunia ni ya wote [weka hapo sauti ya kitoto ujisikilize], kuhusu dini.
Mungu mwenyewe katika hiyo dini/imani anasema Musa akawagawia watu wake [watu wa Mungu] ardhi kwa makabila na mipaka inatajwa katika huo ugawaji wa ardhi sasa wewe hiyo dini ipi unayosema inasema dunia ni ya wote?
Tena kama ni ya wote bona Mungu anasema mataifa yote yatakusanyika mbona anaweka wazi kuwa pana mataifa na kabali, na lugha alivipataje vigezo hivyo kama vya mataifa, lugha kama hakuna mipaka na mataifa?
Swali la mwisho je, wewe unaweza kukataa kwenu na kutaka kuishi kwa jirani yenu? Naamini jibu ni hapana kama utajibu ndiyo basi una matatizo sana.
Kama jibu ni hapana' basi ni sawa na hao wahamiaji kwenda nchi za watu kung'ang'ania kuishi huko tena bila kufuata utaratibu na sheria za nchi husika.
Tena, tafuta madesa/notes usome upya tena kwa umakini wa hali ya juu kuhusu wahamiaji, wahamiaji haramu, wakimbizi, na watafuta hifadhi kwa mfano watafuta hifadhi za kisiasa, kuna wahamiaji wa kutafuta kazi, elimu wote wana makundi ila wanapata hizo hadhi/makundi kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi husika na siyo vinginevyo unavyoaminisha watu.
Hapo, ndiyo urudi tujadili au kama huwezi nipe email yako nikutumie maana naona mengi bado hujui ila unajitutumua au nawe ni mhamiaji haramu hapo ulipo sasa waogopa kukamatwa.
Ok,turudi kwa Waarabu wanaonyanyasa waafrika kule kwao na wao unawatetea!!???
Asante.