Sasa Serikali iamue lugha ya Kiingereza iwe ya kufundishia shule ya msingi kuliko kuruhusu mikoa na wilaya kujiamulia. Huu ni ubaguzi!

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
679
823
Hivi sasa kuna utaratibu usio rasmi kuwa kama shule ya msingi ya serikali inao uwezo wa kuendesha mafunzo ya elimu ya msingi kwa lugha ya kiingereza hupewa ruhusa ya kubadilisha na kuwa english medium.

Kwetu sisi wazazi tunaona kuwa ni jambo jema kabisa kwani tumekuwa tukilihitaji kwa muda mrefu maana tumeshuhudia namna watoto wetu wanavyo shindwa mitihanini ya kidato cha nne kutokana na kutoielewa lugha ya kiingereza, labda hii inaweza kuwafanya wanafunzi kuizoea lugha ya Kiingereza.

Hivi sasa mkoa wa Dar es salaam unabadili shule hizi kwa kasi na hapo awali miaka saba sasa tuliambiwa ni majaribio ambapo hadi sasa hatujaelezwa matokeo yake.

Sasa ni muda sahihi wa kutupa matokeo au serikali iamue shule zote zitumie kiingereza, kuendelea kuruhusu shule kadhaa za umma kutumia kiingereza na nyingi kuendelea kutumia kiswahili ni ubaguzi wa kielimu.
 
Back
Top Bottom