Serikali ina baadhi ya shule za msingi zinazotumia Kingereza kama lugha ya kufundishia?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,278
Ni kweli serikali inazo baadhi ya shule ambazo zinatumia lugha ya Kingereza kufundishia?

Nimewahi kuona mjadala ukisema Olympio primary school iliyoko Dar es Salaam na ambayo inatumia lugha ya Kingereza ni shule mojawapo inamilikiwa na serikali.

Kama ni kweli hizi shule zilianzishwa kwa malengo gani na zinaanzishwa kwa utaratibu upi?

Wanafunzi wanapataje fursa ya kujiunga na hizo shule za Kingereza za serikali?

Walimu wake nao ni watumishi wa serikali kama walimu wengine wote na maslahi yao yanafanana na shule za Kiswahili?

Pia serikali ina mpango wowote wa kuongeza shule za aina hii hasa tukizingatia umuhimu wa Kingereza katika duniani ya sasa na jinsi Watanzania wengi wanavyokosa umahari kutokana na kuchelewa kujifunza na kutumia lugha hii katika ufundishaji?
 
Zipo, ila ni elimu ada, usijedaiwa michango ukaenda kushtaki kwa Diwani kuwa mnachangishwa
 
Sijawahi kuwasikiliza, kikoje Kingereza chao?
Bora asome International school namaanisha international School kweli achana na hizo za serikali na hizi zingine za kilaghai zinazoitwa English medium.

St. Constantine ,ISM, IST, Braeburn hizi ndio shule sasa English inanyooka huko kwengine hakuna kitu
 
mbeya zipo nne

Mkapa Primary ipo Mwanjelwq
Magufuli Primary ipo Pambogo
Azimio Primary ipo mjini

Nyingine ipo uyole jina linitoka

Kuna plan ya kuongeza zingine za ziada
 
Ada na michango ni kiasi gani?
Mfano hizo za Iringa Ada yake ni laki nne na points haifiki laki tano michango ni mchango wa chakula , mlinzi na vitu vidogo vidogo

Walimu wake ndio ni watumishi wa umma kama walivyo walimu wengine tu wa shule za kiswahili medium
 
Back
Top Bottom