Wilaya ya Geita pekee ina upungufu wa zaidi ya Walimu elfu 6 wa shule za msingi

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,315
10,017
Ndugu zangu habari.

Naleta kwenu mada hii kufuatia takwimu mbalimbali zinazoonyesha kumekuwa na ongezeko kubwa Sana la watu Kanda ya ziwa hususani Mikoa ya Tabora, Mwanza, Geita, Shinyanga na Simiyu.

Kutokana na ongezeko hili kubwa imekuwa ni changamoto Kwa serikali kupeleka huduma za kutosha maeneo haya.

Mathalani mahitaji ya taasisi za elim kanda ya ziwa ni makubwa kwan hata uwepo wa shule moja moja ya sekondari katika Kata haikidhi.

Kwa takwimu za karibuni inaonyesha Halmashaur ya Wilaya ha Geita pekee ina upungufu wa zaidi ya walimu elfu 6 wa shule za msingi.

Ni dhahiri kwamba ongezeko kubwa la watu Kanda ya ziwa haliendani na uwezo qa serikali kihuduma za jamii.

Je ni nini serikali ifanye kudhibit ongezeko hili?
 
Serikali ingeachana na mabadiliko ya mitaala kwanza hadi ikamilishe mapungufu makubwa ya waalimu,ili iweze kubaini mapungufu ya kimtaala.

Mtaala uliopo sasa haujatekelezwa kikamilifu kutokana na upungufu mkubwa wa waalimu,unawezaje kujua mapungufu yake?

Mtaala mpya una uhakika gani utatekelezeka wakati tatizo la upungufu ungalipo!
 
Mleta uzi fafanua zaidi

Ni wilaya ipi?, Geita mjini au Geita vijijini?

Au ni mkoa wa Geita wote kwa ujumla?
 
Ndugu zangu habari.

Naleta kwenu mada hii kufuatia takwimu mbalimbali zinazoonyesha kumekuwa na ongezeko kubwa Sana la watu Kanda
Mama Samia atarekebisha na walimu zaidi wataajiriwa na shule kujengwa kabla ya 2025... Tumpe nafasi. By the way Kanda ya ziwa tuongeze matumizi ya uzazi wa mpango. Ongezeko la watu kanda hiyo haliendani na raslimali zilizopo.

Pia tuombe serikali ya mama iongeze mafunzo kwa wakulima na wafugaji ili waongeze tija kwenye uzalishaji kwa eneo dogo wanalolima/fuga ili kupunguza uharibifu wa mazingira
 
Ndugu zangu habari.

Naleta kwenu mada hii kufuatia takwimu mbalimbali zinazoonyesha kumekuwa na ongezeko kubwa Sana la watu Kanda ya ziwa hususani Mikoa ya Tabora, Mwanza, Geita, Shinyanga na Simiyu.

Ni dhahiri kwamba ongezeko kubwa la watu Kanda ya ziwa haliendani na uwezo qa serikali kihuduma za jamii.

Je ni nini serikali ifanye kudhibit ongezeko hili?
Tatizo walimu wengi wapo mijini shule zenye uhaba wa walimu ninza vijijini zaidi ila katikati ya mikoa,wilaya na majiji walimu ni wengi hadi wamezidi
 
Mleta uzi fafanua zaidi

Ni wilaya ipi?, Geita mjini au Geita vijijini?

Au ni mkoa wa Geita wote kwa ujumla?
Hakuna Wilaya ya Geita mjin au Geita vijijin, hizo ni halmashaur za wilaya ya Geita
 
Hakuna ongezeko la watu kanda ya ziwa. Bado Kuna mapori makubwa Geita ambayo ni dalili ya uchache wa watu.

Upungufu wa walimu ni administrative issue na haiwezi kuwa indicator ya ongezeko la watu.
Mapori sio dalili ya uchache wa watu.
 
Uko sahihi, lakini mahitaji ya walimu elfu sita kwa Halmashauri ya Wilaya nahisi Kuna exeggration somewhere.
Nyakati hizi ni rahisi sana kupata ukweli(uhalisi). Idadi ya walimu kila wilaya nchini ipo (Chama cha walimu). Hii idadi yaweza kulinganishwa na idadi ya shule, watu, eneo n. k.
 
90% ya shule za Geita Dc zinawanafunz Zaid ya 1000 na nying NI 2000+
Mkuu kuna tofauti kati ya Geita District Council na Geita Town Council. Sijui unamaanisha ipi yenye wanafunzi kwa idadi unayosema? Na vyovyote vile council yoyoykati ya hizo bado walimu elfu sita ni wengi sana. Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa mfano, HALINA idadi ya hao walimu. Sembuse Geita?
 
Ili upate ukweli ingia www.necta.go.tz Kisha ufungue matokeo ya darasa la nne 2022 Kwa shule utakayoona wewe iwe sample. St Joseph, wema, na bupanga ni private uziondoe.

Kisha uje hapa jukwaani.
 
Back
Top Bottom