Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

2025 Nitampigia kura January Makamba na Mashariki tufaidike.
 
Salaam Wakuu.
Takribani ni Mwaka mmoja toka Serikali ya Awamu ya 5 ishike hatamu naona Trip za Wakubwa zaidi kwanzia PM zaidi ya 90% ni Kusini, yaani Lindi na Mtwara, mathalani PM baada ya Kutoka tu Arusha Juma lililopita kapitiliza Mtwara na leo hii Ruangwa ambako ndiyo jimbo lake, ni zaidi ya mara 3 anashinda huko wakati kuna Mikoa hajakanyaga Kusikiliza Kero za Wananchi wao wenyewe maana ndiyo inatia Uzito. Ikumbukwe ni Waziri Mkuu na si Mbunge wa kawaida.

Naye Mkulu toka State House ndiyo Kabisaaa, ameenda Chato naye si Chini ya Mara 3 na leo yupo huko kwa kisingizio eti kaenda Msibani.Mbona Bukoba walikufa Watanzania na wengi zaidi na jirani na Chato ila hajawahi Kanyaga?

Kama wewe si wa Kusini ama Kanda ya Ziwa hususani Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita nje na Dar es Salaam utasubiri saana.Kumbuka Ukweli hisia huja zaidi baada ya Kujionea.

Aliyoyakataza Muasisi wa Taifa hili la Tanznaia Hayati; Mwl. JK Nyerere yaani, Ukabila, Ukanda na Udini yanarejea kwa Kasi ya Ajabu saana, kwa Pamoja wapenda Tanzania tuyapinge kwa nguvu zetu zote.
Mbona Arusha amekuja huku...?! Shinyanga na Simiyu ameenda lini...?!
 
Mbona Arusha amekuja huku...?! Shinyanga na Simiyu ameenda lini...?!
Nakwambia frequently yupo kanda ya Kusini kuliko yoyote. Na kuna Mikoa kibao hajakanyaga na hali kusini kaenda mara nne. Huona kuna Bias fulani hivi.
 
Mnafurahisha kweli.Mbona kwetu Mara kanda ya ziwa hajafika? ama ni kanda ya ziwa kaskazini? ha ha ha ha
Watanzania fanyeni kazi acheni majungu.
Hawa watu wa ajabu sana... Magufuli alikuja Arusha, Majaliwa kaja Arusha...

Mtu anakwambia eti ameenda na Simiyu sijui wamefika lini...?!
 
Mpakani mwa wasukuma huko singida emu fuatilia uone kama hautokuta wasukuma wengi singida. Pia kanda ya ziwa nako anaenda kwa wasukuma tu mkoa wa Mara hajakanyaga. Na kwa upande wa mwanza kwa ndugu zangu wakerewe hakuna kwenda...over
Na Arusha pia kuna wasukuma wengi ama...?!
 
Bora hata wamepeleka bodaboda 200 Arusha maaana zingepelekwa shinyanga ingekuwa tabu hum
Ambulance tu zenyewe imekuwa ni Shida, halafu pia hata zile ambulance zingeenda tuseme hata Arusha, wengine wangetukanwa...

Ingekuwa kama ile Boda Boda Arusha waliochagua ukawa wakati Mwanza waliochagua ccm wamachinga wanafukuzwa mjini...

Wangesema ccm wamezileta huku ili kwamba wawadanganye wananchi waachane na upinzani...
 
Nakwambia frequently yupo kanda ya Kusini kuliko yoyote. Na kuna Mikoa kibao hajakanyaga na hali kusini kaenda mara nne. Huona kuna Bias fulani hivi.
Umesema Magufuli kakanyaga Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita haswa haswa...

Ndio maana nakuuliza Simiyu alienda lini...?! Au Shinyanga ameenda lini...?!

Mbona huongelei Waziri Mkuu amekaa Arusha zaidi ya week...

Au una lengo la kuwaaminisha watu kitu fulani...
 
kweli ni picha mbaya kwa watu wa mikoa mingine, sijui watu wa bukoba wanajiskiaje km anaishia chato na bukoba hafiki wakati ni kama 200s km tu
 
Taja mkoa ambao waziri mkuu hajafika kwa mwaka 2016
 
Back
Top Bottom