Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

Pm amezuru kwao mara 4 ndani ya mwaka 1.
> mara ya kwanzai....akatoa kauli ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa.
>mara ya pili ...akakagua shule ya sekondari iliyo ungua.
>mara ya 3 ...akafungua duka la msd
>mara ya 4 ndo sasa.

mbona mikoa mingine hajakanyaga hata mara 1?
Na Dodoma alienda kisiasa tu
 
Pm kila baada ya miezi 3 anatimba jimboni kwake
Ujui kuwa pia ni mbunge anatakiwa ajue kero za walio mchagua au wewe unadhani ukiwa waziri Mkuu majukumu ya kuwakilisha wananchi wake yanakoma toa hoja ya msingi hila hii big No.
 
SINGIDA NI NJIA TU wanapita. Siku wakija na bajeti ya maendeleo pamoja n Development plan ya mkoa ndio nitawaunga mkono.
Mkoa wangu singid Sifa yake pekee ni kutoa kura za kutosha kwa ccm bila hio ccm kufanya jitihada za kuuendleza. Naamini siku wakichoka na huku kwetu ndio kifo kamili cha ccm kitatimia.
Wabunge wenyewe w Mkoa huu wanakuja kupatia ubunge tu huku , wao ni Dar na Arusha.
Unaona wengine wanalalamika waziri mkuu kutembelea wapiga kura wake Mara kwa Mara wewe unalalamika kuwa wabunge Wa singida hawashindi majimboni sasa nani yuko sahihi
 
nakumbuka kijamaa kilisema kinazunguka nchi nzima kuwashukuru waliompigia kura,alianza kanda ya ziwa akahusisha na baadhi ya mikoa along mwanza dar road tu..zenji alienda kumwaga sumu za fitna..
sijui mbeya tulikomzomea 2015 atakuja lini kutushukuru wapiga kura ?
Umeshasema mmemzomea xaxa anaanzaje kuja tena kwan x hamkumpigia kura aje kufanya nn ?
 
Hivi Arusha ni Kanda ya ziwa ama kuna wasukuma? maana ameshafika mara mbili ama zaidi, Arusha.
Dah kanda ya ziwa kubwa kweli.

Hii ni kama aliponunua bombandier oohh ohh pangaboy wanunue boeing , wakasambaza na picha kwenye mtandao kwamba tulishamiliki ndege kubwa pembeni zikiwekwa bombandier. Sasa wamenunua boieng kelele kibao tena.

Arusha wakapewa pikipiki ooh oohh sababu ya UKAWA, kwingine kumepelekwa ambulance upendeleo.
DAR mkajengewa barabara ya mwenge kimya na ma fly over, CHATO tu ka uwanja kelele. Ha ha ha ha ha

Watanzania fanyeni kazi , acheni majungu.
Majungu hayatawatoa hapo na kuwapa mkate wa kila siku. Badala yake yanazifanya akili kuwa butu.
 
Ujui kuwa pia ni mbunge anatakiwa ajue kero za walio mchagua au wewe unadhani ukiwa waziri Mkuu majukumu ya kuwakilisha wananchi wake yanakoma toa hoja ya msingi hila hii big No.
Mbona akina Kigwangala, Mwigulu na wengineo wamekwenda karibia kila eneo, kwani wao ndiyo hawana majimbo?
 
chuga wasije watume tuu hela mambo yakuja kuulizana makaburi ya faru wakati tunashida ya pesa hatutaki
 
chuga wasije watume tuu hela mambo yakuja kuulizana makaburi ya faru wakati tunashida ya pesa hatutaki
Arusha waziri mkuu alitembelea Wilaya zote...

Magufuli alishakuja pia...

Nimemuuliza lini hao walienda Simiyu kama anavyodai, lakini naona kimya...
 
Arusha waziri mkuu alitembelea Wilaya zote...

Magufuli alishakuja pia...

Nimemuuliza lini hao walienda Simiyu kama anavyodai, lakini naona kimya...
Mbona mmeng'ang'ana na Arusha tu, kwani hii nchi ni Arusha pekee?
 
Mbona mmeng'ang'ana na Arusha tu, kwani hii nchi ni Arusha pekee?
We umetaja sehemu walizotembelea sana, ukataja Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga...

Na Waziri mkuu ukataja kusini sana...

Ndio maana nikakuuliza lini Magufuli kaenda Simiyu...?!

Ni lini Waziri mkuu na Magufuli wamekaa na kutembelea Mwanza kuliko Arusha...?!

Kwanza hata sasa hivi, Magufuli yupo kwao Chato kwa mapumziko ya sikukuu, na sio kwa kazi za serikali...

Sasa haujioni ya kwamba wewe ni muongo, na una lengo tofauti kabisa...

Mbona Magufuli alivyoenda kushiriki ibada Singida hujalalamika...?! Ameenda Singida mbona hujaiweka kwenye Orodha unadai anapenda sana kanda ya ziwa, halafu hiyo kanda ya Ziwa ukataja mikoa minne...

Sijui Kagera na Mara ipo mikoa ipi...?! Halafu hapo hapo unadanganya watu eti ameenda na Simiyu na Shinyanga...

Niliona umeulizwa na mtu Bukoba ipo wapi ,unadai kanda ya ziwa magharibi, jamaa akakuuliza tena kwahiyo Mara itakuwa kanda ya ziwa Kaskazini...?! Hukujibu...
 
Salaam Wakuu.
Takribani ni Mwaka mmoja toka Serikali ya Awamu ya 5 ishike hatamu naona Trip za Wakubwa zaidi kwanzia PM zaidi ya 90% ni Kusini, yaani Lindi na Mtwara, mathalani PM baada ya Kutoka tu Arusha Juma lililopita kapitiliza Mtwara na leo hii Ruangwa ambako ndiyo jimbo lake, ni zaidi ya mara 3 anashinda huko wakati kuna Mikoa hajakanyaga Kusikiliza Kero za Wananchi wao wenyewe maana ndiyo inatia Uzito. Ikumbukwe ni Waziri Mkuu na si Mbunge wa kawaida.

Naye Mkulu toka State House ndiyo Kabisaaa, ameenda Chato naye si Chini ya Mara 3 na leo yupo huko kwa kisingizio eti kaenda Msibani.Mbona Bukoba walikufa Watanzania na wengi zaidi na jirani na Chato ila hajawahi Kanyaga?

Kama wewe si wa Kusini ama Kanda ya Ziwa hususani Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita nje na Dar es Salaam utasubiri saana.Kumbuka Ukweli hisia huja zaidi baada ya Kujionea.

Aliyoyakataza Muasisi wa Taifa hili la Tanznaia Hayati; Mwl. JK Nyerere yaani, Ukabila, Ukanda na Udini yanarejea kwa Kasi ya Ajabu saana, kwa Pamoja wapenda Tanzania tuyapinge kwa nguvu zetu zote.

Nyerere alikataza kwa maneno, kivitendo kaskazini akina Msuya walikuwa wanaweka umeme mpaka kwenye mabanda ya ng'ombe wakati makao makuu ya mikoa kibao haina umeme. Tulia kama unanyolewa, alipokuja che Nkapa ikiwa kama kawa, shemejiiiiiii, sasa waacheni walioishi kama wako motoni nao waionje pepo, kusini wameteseka jamani mweeee! Kutesa kwa zamu eeeeee!
 
Salaam Wakuu.
Takribani ni Mwaka mmoja toka Serikali ya Awamu ya 5 ishike hatamu naona Trip za Wakubwa zaidi kwanzia PM zaidi ya 90% ni Kusini, yaani Lindi na Mtwara, mathalani PM baada ya Kutoka tu Arusha Juma lililopita kapitiliza Mtwara na leo hii Ruangwa ambako ndiyo jimbo lake, ni zaidi ya mara 3 anashinda huko wakati kuna Mikoa hajakanyaga Kusikiliza Kero za Wananchi wao wenyewe maana ndiyo inatia Uzito. Ikumbukwe ni Waziri Mkuu na si Mbunge wa kawaida.

Naye Mkulu toka State House ndiyo Kabisaaa, ameenda Chato naye si Chini ya Mara 3 na leo yupo huko kwa kisingizio eti kaenda Msibani.Mbona Bukoba walikufa Watanzania na wengi zaidi na jirani na Chato ila hajawahi Kanyaga?

Kama wewe si wa Kusini ama Kanda ya Ziwa hususani Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita nje na Dar es Salaam utasubiri saana.Kumbuka Ukweli hisia huja zaidi baada ya Kujionea.

Aliyoyakataza Muasisi wa Taifa hili la Tanznaia Hayati; Mwl. JK Nyerere yaani, Ukabila, Ukanda na Udini yanarejea kwa Kasi ya Ajabu saana, kwa Pamoja wapenda Tanzania tuyapinge kwa nguvu zetu zote.
Acha majungu bro.
 
Back
Top Bottom