Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

Sasa ni Kanda ya Ziwa na Kusini Basi

Salaam Wakuu.
Takribani ni Mwaka mmoja toka Serikali ya Awamu ya 5 ishike hatamu naona Trip za Wakubwa zaidi kwanzia PM zaidi ya 90% ni Kusini, yaani Lindi na Mtwara, mathalani PM baada ya Kutoka tu Arusha Juma lililopita kapitiliza Mtwara na leo hii Ruangwa ambako ndiyo jimbo lake, ni zaidi ya mara 3 anashinda huko wakati kuna Mikoa hajakanyaga Kusikiliza Kero za Wananchi wao wenyewe maana ndiyo inatia Uzito. Ikumbukwe ni Waziri Mkuu na si Mbunge wa kawaida.

Naye Mkulu toka State House ndiyo Kabisaaa, ameenda Chato naye si Chini ya Mara 3 na leo yupo huko kwa kisingizio eti kaenda Msibani.Mbona Bukoba walikufa Watanzania na wengi zaidi na jirani na Chato ila hajawahi Kanyaga?

Kama wewe si wa Kusini ama Kanda ya Ziwa hususani Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita nje na Dar es Salaam utasubiri saana.Kumbuka Ukweli hisia huja zaidi baada ya Kujionea.

Aliyoyakataza Muasisi wa Taifa hili la Tanznaia Hayati; Mwl. JK Nyerere yaani, Ukabila, Ukanda na Udini yanarejea kwa Kasi ya Ajabu saana, kwa Pamoja wapenda Tanzania tuyapinge kwa nguvu zetu zote.

Bukoba siyo kanda ya ziwa siyo?
 
SINGIDA NI NJIA TU wanapita. Siku wakija na bajeti ya maendeleo pamoja n Development plan ya mkoa ndio nitawaunga mkono.
Mkoa wangu singid Sifa yake pekee ni kutoa kura za kutosha kwa ccm bila hio ccm kufanya jitihada za kuuendleza. Naamini siku wakichoka na huku kwetu ndio kifo kamili cha ccm kitatimia.
Wabunge wenyewe w Mkoa huu wanakuja kupatia ubunge tu huku , wao ni Dar na Arusha.
 
Back
Top Bottom