Sasa Mizengwe ni zaidi ya ze Comedy

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,544
Hawa Jamaa wanakuja vizuri na michezo yao inachekesha + mafunzo

Mfano mchezo Wao wa leo jumapili kwa mlioshuhudia Wale akina Masanja wamebaki umaarufu tu,so kama walivyokuaga Eatv na pia Wanakosa reality hasa kwenye suala la kuigiza sehemu ya jinsia -ke,Kwa Sie wengine joti keshatuchosha na Yale mawigi na matiti.

Hongereni Mizengwe mpo vizuri kazeni buti pia elekezeni wapi tuwaletee ushauri kuzidi kujiboresha.
 
Hawa wajamaa ni wakali kinyama na hawana muda wa kupoteza kujisifusifu ni commedian asilia hasa yule mzee kijana mwenye mvi na yule amabaye yupo siriaz
images
 
-Mchezo/igizo lao la leo limehusu mke kusaidia ndugu zake pesa za shughuli, harusi na matatizo ya kifamilia. Mke kila kitu anasema jukumu aachiwe yeye eg. Vinywaji atasimamia yeye, nguo za bwana harusi(mdogo wake) atasimamia yeye, vyakula atasimamia yeye na kila kitu gharama zote aachiwe yeye. Pia matatizo ya ndugu zake kuhusu pesa na matatizo ya shule nk.
-Mume wa mke alikuwa na msimamo tofauti kuhusu gharama na maisha yenyewe yalivyo magumu.

Hata igizo la wiki iliyopita lilikuwa zuri kwa kijana kuazima gari na kujifanya mfanyabiashara wa mali za kaka yake na mwisho wa siku baadae akaumbuka.

**pongezi za dhati kwa waigizaji wa commedy ya mizengwe**
 
Hawa Jamaa wanakuja vizuri na michezo yao inachekesha + mafunzo

Mfano mchezo Wao wa leo jumapili kwa mlioshuhudia Wale akina Masanja wamebaki umaarufu tu,so kama walivyokuaga Eatv na pia Wanakosa reality hasa kwenye suala la kuigiza sehemu ya jinsia -ke,Kwa Sie wengine joti keshatuchosha na Yale mawigi na matiti.

Hongereni Mizengwe mpo vizuri kazeni buti pia elekezeni wapi tuwaletee ushauri kuzidi kujiboresha.
Watanzania kwa sasa wanaanza kuelewa nani mkweli na yupi mjanja mjanja.. hawa jamaa ni wakali kitambo sema hawana promo.. nimejifunza mengi sana kutoka kwao..kuanzia elimu na burudani
 
Sijawahi kukosa kuwatizama hawa watu, nikiwakosa najiskia vibaya. Mara Kibao nakutana nao Coco beach wanauza DVD zao huwa nazinunua tu
Hii mizengwe ndo comedy nayoilewa, siyo hao wengine wanafikiri eti comedy ni kudhihaki watu, kuvaa kiajabuajabu na kuongea kijingajinga
 
Back
Top Bottom