Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,876
- 2,888
Baada ya mvutano wa muda mrefu na kituo cha TV cha EATV baada ya mkataba wao kwisha na "Ze Comedy" wakasaini mkataba na TBC1 kisha wakapata pingamizi kuhusu matumizi ya jina "Ze Comedy" ndani ya Runinga ya TBC1 toka kwa msajili wa nembo za biashara kwamba hata majina kama "Masanja Mkandamizaji, Joti, Mpoki, nk." Kwamba yasitumike katika kituo cha TBC1, sasa nao Ze Comedy wameamua kwenda mahakamani kupinga amri ya EATV kuhusu matumizi ya jina Ze Comedy na majina yao. Pia watadai fidia ya milioni 200 kwa kufanyiwa mizengwe hiyo.
Mimi nawaunga mkono hawa jamaa maana tanguzamani nilikuwa nafahamu kuna Joti na Mpoki. Achilia mbali jina Ze Cmedy na Masanja na wengine. Hii ina maanisha kuwa hawa EATV watataka hata sura zao zisionekane katika TBC1 kitu ambacho hakiwezekani.
Tuchangie