Kikwete: Rais Samia ni kiongozi asiye na papara na ni mtulivu

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,949

---
Hivi Ndivyo Kikwete Anavyomfahamu Rais Samia, 'Anaongoza Nchi Vizuri, Ana UtulivuWakati wa kuahirisha kikao cha demokrasia kilichofanyika jijini Arusha, Rais Kikwete ameweza kukumbushia historia ya safari uongozi wa Rais Samia baada ya swali aliloulizwa na mwandishi wa habari wa The Chanzo, Khalifa Said.
Rais Kikwete anakiri kujivunia sana na safari ya uongozi wa Rais Samia, na kumpongeza kuwa anaongoza nchi vizuri. Baadhi ya sifa muhimu alizozitaja ni pamoja na kuwa ana utulivu na hana hasira. Kikwete pia amekumbushia misukosuko katika uongozi wake.
---

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anajivunia jinsi Rais Samia Suluhu anavyoongoza nchi kwa utulivu licha ya changamoto anazopitia.

Kikwete ameyasema hayo jioni ya leo julai 18, 2023 jijini Arusha, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Demokrasia Unaoangazia Masuala ya Uongozi barani Afrika, ulioandaliwa na taasisi za MS-TCDC (Tanzania), Center for Strategic Litigation (Tanzania), na Institute for Security Studies (Afrika Kusini).

Amesema kuwa Rais Samia alianza kumvutia kwenye usuluhushi wa mgogoro wa Zanzibar baada ya uchaguzi wa mwaka 2000, ambao alifanikiwa kuuona upeo wake mkubwa katika uongozi baada ya kuwa kwenye kamati moja ya uchaguzi na usuluhishi juu ya mgogoro huo.

Alisema kuwa changamoto mbali mbali anazopitia Rais Samia katika uongozi wake ikiwemo mambo yanayoibuka, angepaniki kidogo tu angevuruga watendaji wake na nchi nzima kwa ujumla lakini utulivu unamsaidia licha ya hasira alizonazo.

"Rais Samia kufanikiwa kufikia leo ni utulivu pekee unamsaidia, maana hakuna nafasi ngumu kama aliyonayo lakini kwa sababu ya utulivu wake ingawa ana hasira lakini mambo yanaenda, hiyo pekee inatosha mimi kujivunia yeye baada ya kumuibua huko Zanzibar na kumleta Muungano," amesema.
 
Kesha vunja mkataba?

Utulivu unaoshindwa kuelewa sheria za mkataba wa DP world unatusaidia nini sisi!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom