Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Salamu za mwaka mpya 2023 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa watanzania wote.
Amemshukuru Mungu mtukufu, mkarimu na mwingi wa rehema kwa kuiona siku ya leo tunapoaga mwaka 2022 sasa tunaingia mwaka mpya 2023, amewatakia watanzania wote mwaka wenye furaha na neema. Anawaombea wale wenye changamoto watazame mwaka mpya kwa uthubutu wa kutokukata tamaa na kupambana. Kwa marehemu wote, Rais Samia amewaombea pumziko la amani.
Amewasifu watanzania kwa kuvuka mwaka wakiwa na mshikamano, kulinda amani na kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Amewakumbusha viongozi kuongoza kwa juhudi, uadilifu, misingi ya haki na sheria.
Ameomba tuendelee kushikamana, kutunza umoja wetu na amani ya nchi. Pia, tujitahidi kuepuka misiba isiyo ya lazima mwishoni mwa mwaka huu na tunapoanza mwaka mpya.