mzunguko ni mkubwa🤣🤣🤣ila kwa kua unatoa haijalishi ubatoa card au cashi basi fresh we ni wa maana saaana
hayo mengine achana nayo🤣
Joannah anatoa bhana
Kutoa halijawahi kuwa tatizo. Mimi Msukuma kwetu tunatoa si kwa mke tu, mpaka kwa watu tusiowajua wenye uhitaji, ni utamaduni wa ukarimu tu.
Na hata hapa JF hapa hapa kuna watu sijawahi hata kukutana nao, na nimewasaidia mitaji ya biashara "ndogondogo" kwa kujua matatizo yao na mipango yao tu. Kusaidiana kibinadamu tu.
Mimi naishi Marekani na sina mpango wa kuja Tanzania hivi karibuni, wao wanaishi Tanzania hawana hata ndoto za kufika Marekani, najua hatutaonana, lakini nimesaidia kiroho safi tu. Kama mtu anavyotoa sadaka kanisani au msikitini, wengine hatuendi kanisani wala msikitini ila tunasaidiana na watu tu moja kwa moja.
Kwa hiyo kutoa has never been a problem. Wala sina nia ya kukataa kutoa.
Kutoa ni suala la ubinadamu tu wala hata halihitaji kuwa katika muktadha wa mapenzi.
Kwangu tatizo si kutoa, kutoa kuna mpaka bajeti yake maalum.
Tatizo unamtolea nani? Unamtolea mtu golikipa mwenye mentality ya kuhudumiwa kila siku kwa sababu yeye mwanamke tu au mtu aliye productive?
Ikiwa unamtolea mtu golikipa, kwenye muktadha wa mahusiano kama mke au mwenza, anayetaka kutunzwa tu, hajui hata pesa inatengenezwa vipi, maana yake ukifa leo hata kuiendeleza pesa hawezi. Anategemea fadhila za wanaume. Huu sio mwanzo wa umalaya huu sasa?
Huyo ni mtu masikini wa mawazo, tegemezi, kilema wa kujitakia.
Anataka kuhudumiwa tu.
Huyo ni mtu mzigo kwa jamii. Yani hiyo mindset yake tu tayari ni turn off kubwa sana kwa mtu anayeielewa dunia ya leo.
Wanaume wanaojitambua wameshagundua hii trick ya kuwajaza upepo kwa kuwaita providers bila ya wanawake kuwa na mchango katika maisha, kwa makusudi, ni exploitation na actually inaondoa productivity na dignity ya mwanamke.
Wameikataa.
Hatutaki wanawake mizigo wasio na mchango.
Tunataka mwanamke ambaye hata tukifa leo tunajua ataendeleza biashara za familia.
Si mwanamke masikini mpaka wa mawazo.