Sakata la Wamachinga na mgambo Mwanza lilishia wapi? Walipewa maeneo au walirudi barabarani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Mwezi wa 2 mwaka huu 2023, kulizuka taharuki maeneo ya Mtaa wa Makoroboi, jijini Mwanza, ambapo mgambo walikuwa na zoezi la kuwatoa wafanyabiashara hao kwenye eneo walilokuwa wanafanyia kazi. Nini kilifata, wamachinga walipewa maeneo au wamerudi kuendelea kufanya kazi bararani?

Wamachinga wamekuwa wakitumika kisiasa huku kauli zinazotolewa na viongozi kuwa geresha tu. Mbunge akifika anakwambia acha wamachinga wafanye kazi barabarani lakini akifika Mkuu wa Mkoa anatoa katazo la biashara hizo kuendelea, na hata ikitokea wanatenga maeneo, yanakuwa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na sio sehemu rafiki kwa biashara kiujumla. Mwisho wa siku inakuwa nguvu za soda tu, watu wanaendelea na biashara zao pembezoni mwa barabara kama kawaida.

Kwa upande wa Mwanza hali ikoje? Biashara hazifanyiki tena kando ya barabara? Au wanasubiri tena siku wazuke watoe matamko mengine?

Update: Machinga Mwanza warudi kwa kasi barabarani

Pia soma:
Machinga wachachamaa Mwanza hali ni tete wanarusha mawe kwenye maduka

Tusipopaza sauti, Viongozi wa Machinga Mwanza watadhuriwa mikononi mwa Polisi
 
Makoroboi hawajarudi tena ila wamejaza kando kando ya barabara za mijni kote nani aende Kiloleli au Nyamhongolo?
 
Back
Top Bottom