Torra Siabba
Senior Member
- Jul 24, 2016
- 105
- 102
Wakati serikali mkoani Mwanza ikiwa imetenga maeneo maalumu kwaajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga kufanya biashara zao, wafanya biashara hao wameanza kurudi kufanya biashara kandokando ya barabara jambo ambalo lilipigwa marufuku na Serikali.
Jana nilifanya ziara maalumu jijini Mwanza ambapo nilizunguka mitaa ya Nyerere Road, Rumumba, Pamba road, Rufiji, Dampo na kukuta machinga kibao wakiwa wamepanga biashara zao kandokando ya barabara jambo ambalo limekuwa likikatazwa na serikali bila ya mafanikio kwakua Machinga wamekuwa hawataki kwenda kwenye maeneo maalumu yaliyopangwa kwaajili yao.
Baadae nilipata nafasi ya kwenda kwenye soko la Mchafu kuoga lililipo Igogo, Nyamagana jijini Mwanza na kukuta idadi ndogo ya wafanya biashara pamoja na lile la Kiloleni.
Mkoa wa Mwanza umekuwa miongoni mwa mikoa korofi kwa machinga kutokuwa wasikivu licha ya serikali kuwapangia maeneo ya kufanya biashara zao lakini wao kuamua kufanya biashara barabarani.
Pia Soma Machinga wachachamaa Mwanza hali ni tete wanarusha mawe kwenye maduka