Waziri Mchengerwa anawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2024/25

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,079
12,526

View: https://www.youtube.com/watch?v=ezJ5n2FzdlYZUNGU: MGAMBO WANAWANYANYASA MACHINGA NCHI NZIMA
Naibu Spika Mussa Azzan Zungu amesem Asilimia kubwa ya Mgambo wamekuwa wakinyanyasa Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) bila kujali wanafanya biashara katika mazingira halali, amesema hayo Bungeni, leo Aprili 16, 2024.

Awali, Mbunge Jesca Msambatavangu aliuliza lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais ya Mwaka 2022 kuwasaidia Machinga wa Iringa Mjini kiasi cha Tsh. Milioni 700 ili kuboresha mazingira yao? Ambapo Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis alisema ahadi hiyo itatekelezwa.

Awali Mdau wa JamiiForums.com alizungumzia kuhusu hii changamoto, soma zaidi hapa - 'Nyau' Kariakoo wanavyowaliza Wamachinga, nani yupo nyuma yao?

Snapinsta.app_436163345_18323781844193701_4468427882341459283_n_1080.jpg

Snapinsta.app_436252760_18323781799193701_1892828155344781428_n_1080.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa akiwasili Bungeni tayari kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.
Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ujenzi wa soko umefikia 93%
Shirika kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam limeendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko jipya la Kariakoo lenye ghorofa sita za juu na ghorofa mbili za chini na ukarabati wa jengo kuu la soko la Kariakoo.

Mradi ulianza kutekelezwa Januari, 2022 na Mkandarasi ESTIM Construction Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 28.03, mtaalamu mshauri ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Utekelezaji wa mradi umefikia Asilimia 93. Hadi Machi, 2024 mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 17.24. Aidha, maandalizi ya ufunguzi wa soko yanaendelea ili biashara zianze mwanzoni mwa mwaka 2024/25.

Serikali kutumia Tsh. Bilioni 190.57 kununua V8 mpya za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ujenzi wa Makazi na Utawala
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Mikoa ikiwemo majengo ya utawala, Ikulu ndogo, makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa katika Mikoa 26.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16,2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/202 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara”

“Shughuli nyingine ni ununuzi wa magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri.”Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Namba 02)
Katika Mwaka 2024/25, Tume ya Utumishi wa Walimu imepanga kutumia Tsh. Bilioni 20.74 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo katika maeneo yafuatayo: -

Kusimamia ajira, maadili na maendeleo ya walimu kwa kuhakikisha kwamba walimu wanasajiliwa, wanathibitishwa kazini na kwa wale wenye sifa wanapandishwa vyeo na kubadilishiwa kada kwa wakati;

Kusimamia maadili na nidhamu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika utumishi wa umma;

Kufanya utafiti na kutathmini hali ya walimu nchini na kubainisha aina na mahitaji ya walimu, idadi na ngazi ya walimu wanaohitajika;

Kukamilisha utengenezaji wa mfumo wa TSCMIS, usimikaji wa miundombinu ya mtandao wa intaneti katika ofisi 115 za wilaya; na

Kuendelea na ujenzi wa jengo la ofisi ya tume makao makuu
 
Huzuni sana bunge, hutu mbunge wa wapi sjui kamaliza kuongea hapa saa 12 na dakika 5 hivi, kachoma sana muda kumshukuru raisi na kuahidi mambo ya uchaguzi, anakuaja kuanza hoja dakika chache muda umeisha, hii Tz
 
Hawa watu ni wabad sana.
 
  • Thanks
Reactions: Lax

ZUNGU: MGAMBO WANAWANYANYASA MACHINGA NCHI NZIMA
Naibu Spika Mussa Azzan Zungu amesem Asilimia kubwa ya Mgambo wamekuwa wakinyanyasa Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) bila kujali wanafanya biashara katika mazingira halali, amesema hayo Bungeni, leo Aprili 16, 2024.

Awali, Mbunge Jesca Msambatavangu aliuliza lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais ya Mwaka 2022 kuwasaidia Machinga wa Iringa Mjini kiasi cha Tsh. Milioni 700 ili kuboresha mazingira yao? Ambapo Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis alisema ahadi hiyo itatekelezwa.

Awali Mdau wa JamiiForums.com alizungumzia kuhusu hii changamoto, soma zaidi hapa - 'Nyau' Kariakoo wanavyowaliza Wamachinga, nani yupo nyuma yao?

View attachment 2965081
View attachment 2965086
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa akiwasili Bungeni tayari kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.
Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ujenzi wa soko umefikia 93%
Shirika kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam limeendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko jipya la Kariakoo lenye ghorofa sita za juu na ghorofa mbili za chini na ukarabati wa jengo kuu la soko la Kariakoo.

Mradi ulianza kutekelezwa Januari, 2022 na Mkandarasi ESTIM Construction Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 28.03, mtaalamu mshauri ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Utekelezaji wa mradi umefikia Asilimia 93. Hadi Machi, 2024 mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 17.24. Aidha, maandalizi ya ufunguzi wa soko yanaendelea ili biashara zianze mwanzoni mwa mwaka 2024/25.

Serikali kutumia Tsh. Bilioni 190.57 kununua V8 mpya za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ujenzi wa Makazi na Utawala
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Mikoa ikiwemo majengo ya utawala, Ikulu ndogo, makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa katika Mikoa 26.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16,2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/202 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara”

“Shughuli nyingine ni ununuzi wa magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”

Hizi bajeti za Tanzania huwa naziona kama 'pwagu na pwaguzi' tu!!!!
 
Back
Top Bottom