Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Vijana vyenyewe vijinga. Kwa nini vikubali vibabu, Mwiru, Kawawa, na Makamba, vije kuingilia uchaguzi wao?

Mkuu hawa vijana kwa sasa unawaonea bure...wakati wa kuwatosa hawa wazee ndio umefika sasa lakini timu bado haijajipanga vizuri. Inahitaji watu bold kama Nape wanaoweza kusimama na kukemea fisadi Lowassa hadharani. I mean ulitegemea fisadi Nchimbi ndio apendekeze wakina Kingunge, Kawawa wangolewe. Iwapo kingunge alishindwa kupata kura za kuingia NEC Taifa sioni kwa nini iwe vigumu vijana kumtosa iwapo watapata viongozi wenye kifua.
 
This thing is incredible, maneno ya hii kitu inakuwa very interesting nimebahatika kuongea na wanaohusika, sana na this whole thing:-

1.According to deal ni kwamba Rais alipomteua Pinda kuwa PM kabla ya kuvunja baraza la mawaziri, kulikuwa na kikao cha CCM na joint UV-CCM, ambacho kilikuwa na lengo la kutoa azimio la kumpongeza Rais kwa chaguo lake, la Waziri Mkuu mpya.

2. Nchimbi akagoma akisema kuwa Uv-CCM au yeye under any capacity, hawezi kuwa involved na huo ujinga kwa sababu yeye hamtambui Pinda, kwa hiyo he is out na hilo azimio. Ujumbe ukafikishwa kwa rais kama ulivyo, na according to more dataz ni kwamba kwa makusudi mazima wale wote aliowapandihsa chati Nchimbi, kupitia UV-CCM, kina David, Masha, na Kamalla wakapewa uwaziri kamili.

3. Nchimbi akatanagaza rasmi ndani ya vikao vya CCM kuwa yeye sasa ni mfuasi wa Lowassa, kwa 100% na kwamba no matter what Pinda is no body to him, na kwamba majuzi Nchimbi alipoamua kumtumia muandishi wake kuandika uongo kuhusu habari za jengo na Nape huko CC, ni muungwana mwenyewe aliyempigia simu mwenyekiti wa IPP, akitaka kujua huku akifoka kuwa hiyo habari nani aliyeipeleka huko Nipashe, mwandishi alipobanwa ndio akatema sumu yote na kumtaja Nchimbi. Ni baada ya mkwara mzito sana aliopewa mwenyekiti wa IPP, ndio maana Nipashe wakaomba msahama na hata kumtaja waziri anyewapa habari za ndani za CC.

4. Ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewaagiza UV-CCM kukutana jana, kuamua kuhusu majina na sio anything else, sasa according to the dataz ni kwamba Nchimbi na Makamba wanasubiriwa sana na CC, kwa sababu Kingunge haingii tena CC, nimedokezewa na wajumbe kama wanne wa CC kuwa huko kutawaka moto siku ya tarehe 9, maana no way hii kitu ya Nchimbi inaweza kupita huko kwa sababu wanajua kuwa ikifika NEC itakuwa aibu kubwa sana kwa CC wanaweza kuzomewa kama Butiama na muafaka, the dataz ni kwamba Nape ameambiwa atulie na kusuubiri tarehe 9.

My Take:

Kwa kweli sasa hili taifa tumefika mbali sana, yaani the lowest mark kwa any president aliyewahi kuliongoza taifa hili, I mean Nchimbi anwezaje kuwa na utovu wa adabu kiasi hiki na bado akapewa uwaziri mdogo wa Ulinzi kama adhabu? Haya ni mambo ya aibu sana sio tu kwa mwenyekiti wa CCM na viongozi wote wa CCM, bali ni kwa wananchi wote wa taifa hili. I want kuamini kuwa CC itasimama kidete na kumfundisha adabu Nchimbi, otherwise tutakuwa tumekubali kuwa under mafisadi, tunaisubiri kwa hamu tarehe 9, kusikia maamuzi ya mwisho.

Ahsante Wakuu na Tunaendelea Kufuatilia Kwa Makini na Ukaribu Sana hizi Stunning Events. Kesho Tutakuwa Na Zaidi Ya Yalioyjiri na Pia Tutazungumza na Nape Mwenyewe.
Leadership Vacuum ilianzia mbali.

Nashukuru inajitokeza wazi. Wenye kufanya uchambuzi wameanza kuiona mapema sana. Walioko Bungeni pia wanafahamu fika kutokana na vyanzo vya Bunge ambavyo katika hatua hii sitavi disclose. Lakini

i) Nchi ipo pabaya

ii) Hakuna maamuzi katika ngazi zote za juu

iii) Rasilimali za nchi ndiyo kwanza zinamalizika na waliopewa muda wanautumia vizuri muda huu kufanya 'haswa'. Wachache wanaochukuliwa hatua ni vijisamaki na ni kiinimacho tu.

iv) Swala la 2010 kwa wanaokuwa na uchungu wanajua ni mbali sana. Any single mistake katika mipango inairudisha nchi 10 years back. Hali hii isipokemewa sasa na Watanzania wote bila kujali itikadi by the time tunafika 2010 tutakuta nchi imeisha. Ndiyo maana katika nchi kunapoporomoka imani ya Wananchi kuna mechanism ya kisheria ya kuleta mabadiliko ya nchi bila vurugu, na kuvunja amani. Watanzania wanaendelea kuaminishwa kuwa amani ni mtaji muhimu sana, sawa lakini amani kwa nani? hata kwa anayelala na mlo mmoja kwa siku tena wa kubahatisha, wakati hao wanaotumia amani kama mtaji wanakula kwa vijiko vya dhahabu?

v) Watanzania maskini wasiojua chochote wameburuzwa nchi nzima kuandamana kuunga mkono hotuba ya Rais, ambayo hadi dakika hii, tarehe 8/9/2008 hakuna anayejua the exact text ipo wapi, wala siyo iliyotolewa na Rais siku alipoisoma, wala siyo text ya Hansard?

vi) Kufukuzwa kwa mpambanaji Nape, ambaye nina imani siyo mtu aliyekurupuka, wala kutoa matamshi bila ushahidi kwa sababu mengi yametoka magazetini, ni fundisho kubwa kwa wote wenye mapenzi na nchi hii na wapambanaji dhidi ya ufisadi. Na bado wako wengi watafuata.

Ninachochukia ni mtu anayetoa matamshi kwa umbeya, hawezi kuthibitisha lakini atashikia bango. Huu ni ubabaishaji, lakini siyo kwa mfano ambao Nape ameutoa ambapo mikataba husika imechapishwa hadi kwenye magazeti.
 
Mkuu Yebo yebo,

JK hana uwezo wowote hasa linapokuja suala la mchezo mchafu.Yeye ni muumini mtiifu wa hiyo ibada ya mchezo mchafu,Sasa kweli kwenye nomination ya 2005 yale waliyoshirikiana na Nchimbi pamoja na Mtandao against other candidates yalikua na tofauti na haya? Mimi nimepoteza matumaini na rais wangu.He's just a back bencher.He is there only for clapping.

Yani madaraka yake ya muhimu kwa taifa yamepungua,he is ceremonial president.But kwa yale yasiyo na tija yuko mbele,active foreign minister.Ohh! I'm sick.
 
Dr. Nchimbi tarehe ya kuzaliwa 24 Dec 1971. Kijeba na miaka 37, anafanya nini kwenye umoja wa vijana ambao muda wa mwisho ni miaka 35?
 
Mimi siungani na baadhi ya Wachangiaji wanaosema kuwa Nape ahame Chama,anatakiwa abaki kulekule ili awaonyeshe msimamo wake ulio wa dhati.Kitu kimoja ambacho siridhiki na wapinzani ni kuwa ktk baadhi ya mambo na wenyewe wameweka maslahi yao mbele kuliko umoja wao, hivyo kukosa vision.Kwa mfano mgawanyiko wanaouonyesha ktk Jimbo la Tarime ni wazi kuwa CCM watachukua jimbo badala ya kuunganisha nguvu na kuwa na mgombea mmoja.

Kubwa ktk sakata hili, nikuwa mzee Kawawa ambaye nina mheshimu ktk mambo mbalimbali ameuungana na wale waliokuwa wanampinga Nape.Lakini kwa watu wengi pengine wanaweza wakafikiri kuwa huyu mzee ana mwanawe Zainabu Kawawa na ni mgombea na uwepo wa Nape ungekuwa kikwazo ktk kufanikisha mwanawe sasa ndio maana naye kaunga mkono hili.Ikiwa yeye alikuwa anachukia sana ufisadi alitakiwa aangalie ktk njia mbili na sio kwa mkondo mmoja.

Mwisho ni kuwa Nape ni kama mpiga filimbi ktk rushwa, na uzoefu ni kuwa wapiga filimbi mwisho wao unakuwa sio mzuri,hivyo basi nilikuwa nategemea kuwa mwisho wake utakuwa mbaya kwani system haikutaka kuona inakosorewa.

Nawasilisha.
 
Huyu Nchimbi kachokoza nyuki asitoke nduki huyu Lowasa wake atamtosa tu nyie subili atakavyo anza kukaangwa.....................
 
Chama Kina Wenyewe...Chama Chama Kimetukomboa...Kawawa, Kingunge, Nchimbi, Makamba Oyee...Wasaliti ziii...Na Mafisadi? Hivi Chama kipi kimetukomboa na kimetukomboa kutoka kwenye nini na kutoka kwa nani?
 
Mhe,Dr.W.Slaa,

Maneno adimu sana mkuu,tukiangalia hali iliyopo sasa hivi Tanzania hata kuhamasisha wananchi kunahitaji nguvu kubwa na lazima tukubali kuitumia kutokana na mazingira yaliyowekwa,hata hivyo hali ya uamsho wa vuguvugu la mabadiliko inaendelea kuwa rahisi kwani baadhi ya wananchi sasa wanagutuka.

Tanzania huku tuendako ni dhahiri kutakua na mabadiliko makubwa ya upepo wa kisiasa,hata serikali nayotawala bila shaka inaona hilo lakini kama mabadiliko haya yatakuja katka mazingira yaliyopo,mazingira ambayo Chama Tawala kinaamini kwamba ndicho chenye hatimiliki ya nchi hii pamoja na watawala wachache tu,basi watazuia mabadiko hayo kutokea kwa njia ya amani lakini kwa vyoyvyote vile Mabadiliko ni lazima

Unajua wakati wa mabadiliko,amani huvurugika mara nyingi kutokana na nature ya mfumo utumiwao na chama tawala.Wao ndio wazuiao mabadiliko ya amani na kuwafanya wanamageuzi na wananchi wazalendo kufuata hiyo njia nyingine.Naaamini kabisa kama tulimtoa mkoloni mweupe kwa njia ya amani,nasi lazima tumtoe mkoloni mweusi kwa njia ya amani.Na hili ndilo litakalotuunganisha zaidi watu wenye itikadi tiofauti katika kusimami mabadiliko,na mageuzi makuu katika taifa hili.
 
Hiyo ndio ccm bwana! kama Nape ameanzisha mapambano ya kweli na sio longolongo za kutaka uenyaketi bado ana nafasi nzuri sana ya kuendeleza mapambano ya kweli. Ajivue na uanachama wa CCM pia. Anasubiri nini?
 
1.
Nashindwa kujua Nec-UVCCM kwa nini badala ya kujadili majina ya wagombea huko Dodoma kama agenda za kikao zilivyowataka wao wakaenda kubadili agenda na kuifanya iwe ya kumjadili Nape Nnauye kiundani hadi kumvua uanachama wa UVCCM. Wangekuwa na kheri naye wangetoa jina lake lisipekwe CC kugombea Uenyekiti UVCCM lakini wao wakaenda mbali sana na agenda za kikao.

1. Survival ya Nchimbi, siku zote imekuwa ni Kingunge wa kusini mwenzake, huu mchezo mchafu ndio aliomfanyia Gama kwenye ubunge, Gama alipolalamika tena with very valid arguments, ni Kingunge aliyezima kwa chini chini kule CC,

2. Kikao hiki cha Dodoma, kilikuwa ni shinikizo toka kwa Mwenyekiti wa CCM, baada ya Nchimbi kuwekwa kiti moto ndani ya CC, kwa hiyo kule UV-CCM Nchimbi alikwenda kuonyesha power yake huku akiwa amejeruhiwa na kukigeuza kikao kuwa Nape, kwa sababu hata CC it was the same Nape na makelele ya muungano, lakini on his part hapa Nchimbi amechemsha sana kwa sababu Makamba hawezi kusimama naye ndani ya CC na huu ujinga, ukweli ni kwamba this was a political desparation, halafu ni clear kuwa Nchimbi ana akili ndogo sana ya siasa angekuwa na kubwa sana angefikiri sana kwamba Nape anajiamini nini hasa? Mwenyekiti wa CCM hakutakiwa kujihusisha na deal ya jengo, kwa mujibu wa katiba ya CCM alitakiwa kusubiri maelezo toka kwa Makamba, kama agenda ya mkutano, lakini mpaka leo haieleweki Rais aliingiaje kwenye kujihusisha na kuifuatilia hii deal hapo peke yake palitakiwa kumfanya Nchimbi ashituke!

2.
Sina imani na Mwenyekiti JK kama ana-balls za kusimama imara ndani ya CC na kusema CCM ni muhimu iwe inakosolewa na hivyo kuveto uamuzi/ mapendekezo ya Nec-UVCCM. Huu moto wa mabadiliko unawaka unavyotakiwa ndani ya CCM; wakina Kingunge, Kawawa, Lowassa na Makamba wao bado wanajiona wako mbali ya miali mikali ya moto huu. Siku zao zinahesabika, naona itafika siku watakisusia Chama Chao.

Hapa yatakuwa ni yale yale ya Lowassa, atoke au asitoke uwaziri mkuu, ninaamini kuwa rais siku hiyo atawekwa pembeni na uamuzi utatolewa na wengine, kama siku Salmin alipokataliwa kugombea term ya tatu, rais aliwekwa pembeni.

Kingunge na Kawawa, wamevutwa na Nchimbi, akidhani kuwa that way anamtisha Rais aliyemuamuru kwenda Dodoma haraka kufanya kile kikao, na ambaye tayari ameshachukua sides kwenye ishu ya jengo, kama hoja ya Nchimbi na Makamba, against Nape inatakiwa kusimama, basi Mwakyembe, Sendeka, Seleli, Kimaro, Sitta, na Mama kilango nao pia wanatakiwa kufukuzwa uanachama wa CCM kwenye hicho kikao cha tarehe 9, kama hii ni kweli je kwa nini Rais aliwapiga marufuku Makamba na Pinda kuwatisha wabunge wanaouliza waswali against CCM?

Hapa mkuu ngoma ni nzito sana, tarehe 9 kutakuwa na moto mzito sana kwa sababu Rais ni lazima atawekwa kiti moto na wajumbe kwamba kama ishu ya jengo haikutakiwa kusemwa nje ila kwenye vikao ilikuwaje Rais akairukia na kuwaamuru mawakili kuichunguza na kusema wazi kama ina tatizo?

This is all good na mabadiliko ya taifa letu.
 
...hotuba ya Rais, ambayo hadi dakika hii, tarehe 8/9/2008 hakuna anayejua the exact text ipo wapi, wala siyo iliyotolewa na Rais siku alipoisoma, wala siyo text ya Hansard?

Mheshimiwa,

Niliipitia ile iliyowekwa hapa na Mwanakijiji, nikaona inafanana fanana na kile alichosema Rais. Manake kuna maneno mule ya mtaani taani Rais aliyatumia naona yamo humo pia, kwa hiyo inawezekana ni ile yenyewe ambayo haijahaririwa.

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=17595

Aliposema akitaka anaweza kumwambia IGP akukamate imo pia. Nadhani hii ndio yenyewe, au ?
 
Ila mimi nashindwa kuelewa mtu akiwa na uajsiri wa kumtukana mjumbe wa kamati ya juu ya chama kuwa 'mwendawazimu',sijui atashindwa vipi kumtukana mwananchi wa kawaida kule kijijini,inabidi ujiulize inawezekana hata wakati mwingine anakereka na watu flani lakini anatukana tu kimoyomoyo au?

Hizi dharau sijui zinaletwa na msukumo gani hasa
 
Mheshimiwa,

Aliposema akitaka anaweza kumwambia IGP akukamate na lenyewe limo. Nadhani hii ndio yenyewe, au ?

Na huo mfano wake nae sijui,lengo lake lilikua ni kutoa tu huo mfano na si kutisha?
Hakutaka atakumtolea mfano mtuhumiwa mmoja wa RICHMOND au EPA maanake hapo aliheshimu haki za raia au?
 
Just in Halmashauri Kuu ya UVCCM inayokutana Dodoma imemvua Uanachama wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Nape NNauye kwa sababu nyingine ikiwamo utovu wa nidhamu...wengine wenye habari zaidi watufahamishe zaidi.

wanaacha kuwavua uwanachama akina lowasa, karamage, mzee wa vijisenti, maana hao ni wezi, kijana wa watu kavuliwa uanachama kwa ajili ya kufichua maovu. hii ndo Tanzania
 
Leadership Vacuum ilianzia mbali.

Nashukuru inajitokeza wazi. Wenye kufanya uchambuzi wameanza kuiona mapema sana. Walioko Bungeni pia wanafahamu fika kutokana na vyanzo vya Bunge ambavyo katika hatua hii sitavi disclose. Lakini

i) Nchi ipo pabaya

ii) Hakuna maamuzi katika ngazi zote za juu

iii) Rasilimali za nchi ndiyo kwanza zinamalizika na waliopewa muda wanautumia vizuri muda huu kufanya 'haswa'. Wachache wanaochukuliwa hatua ni vijisamaki na ni kiinimacho tu.

iv) Swala la 2010 kwa wanaokuwa na uchungu wanajua ni mbali sana. Any single mistake katika mipango inairudisha nchi 10 years back. Hali hii isipokemewa sasa na Watanzania wote bila kujali itikadi by the time tunafika 2010 tutakuta nchi imeisha. Ndiyo maana katika nchi kunapoporomoka imani ya Wananchi kuna mechanism ya kisheria ya kuleta mabadiliko ya nchi bila vurugu, na kuvunja amani. Watanzania wanaendelea kuaminishwa kuwa amani ni mtaji muhimu sana, sawa lakini amani kwa nani? hata kwa anayelala na mlo mmoja kwa siku tena wa kubahatisha, wakati hao wanaotumia amani kama mtaji wanakula kwa vijiko vya dhahabu?

v) Watanzania maskini wasiojua chochote wameburuzwa nchi nzima kuandamana kuunga mkono hotuba ya Rais, ambayo hadi dakika hii, tarehe 8/9/2008 hakuna anayejua the exact text ipo wapi, wala siyo iliyotolewa na Rais siku alipoisoma, wala siyo text ya Hansard?

vi) Kufukuzwa kwa mpambanaji Nape, ambaye nina imani siyo mtu aliyekurupuka, wala kutoa matamshi bila ushahidi kwa sababu mengi yametoka magazetini, ni fundisho kubwa kwa wote wenye mapenzi na nchi hii na wapambanaji dhidi ya ufisadi. Na bado wako wengi watafuata.

Ninachochukia ni mtu anayetoa matamshi kwa umbeya, hawezi kuthibitisha lakini atashikia bango. Huu ni ubabaishaji, lakini siyo kwa mfano ambao Nape ameutoa ambapo mikataba husika imechapishwa hadi kwenye magazeti.

njia ya box 2010 haondoki mtu. Na dawa ya box haitafanya kazi ndani zaidi ya miaka 30 ijayo.

Mimi ninachofikiri saizi ni wafanyakazi ndio wataiokoa nchi hii ,WANASIASA hawatoweza kitu.

Kifupi WAFANYAKAZI wote kuanzia ngazi ya kitongoji hadi mwisho WASIOGOPE kufukuzwa kazi WAGOME tu waache kufanya kazi mda wote mpaka pale SERIKALI itakapojiuzulu Na nchi kukabidhiwa Ma engineer na madaktari miaka 5 ndio uchaguzi utakapofanyika.

vinginevyo ni kelele za chura tu.
 
Hapa yatakuwa ni yale yale ya Lowassa, atoke au asitoke uwaziri mkuu, ninaamini kuwa rais siku hiyo atawekwa pembeni na uamuzi utatolewa na wengine, kama siku Salmin alipokataliwa kugombea term ya tatu, rais aliwekwa pembeni.

Kingunge na Kawawa, wamevutwa na Nchimbi, akidhani kuwa that way anamtisha Rais aliyemuamuru kwenda Dodoma haraka kufanya kile kikao, na ambaye tayari ameshachukua sides kwenye ishu ya jengo, kama hoja ya Nchimbi na Makamba, against Nape inatakiwa kusimama, basi Mwakyembe, Sendeka, Seleli, Kimaro, Sitta, na Mama kilango nao pia wanatakiwa kufukuzwa uanachama wa CCM kwenye hicho kikao cha tarehe 9, kama hii ni kweli je kwa nini Rais aliwapiga marufuku Makamba na Pinda kuwatisha wabunge wanaouliza waswali against CCM?
Hapa mkuu ngoma ni nzito sana, tarehe 9 kutakuwa na moto mzito sana kwa sababu Rais ni lazima atawekwa kiti moto na wajumbe kwamba kama ishu ya jengo haikutakiwa kusemwa nje ila kwenye vikao ilikuwaje Rais akairukia na kuwaamuru mawakili kuichunguza na kusema wazi kama ina tatizo?

This is all good na mabadiliko ya taifa letu. [/SIZE]

2790.png

Hiyo ya Mama Anna Kilango dont bet on it kwani DEDDY yupo mle atamlinda MOMMY lakini kimya cha huyu mheshimiwa kwenye sakata hili tunatutia wasi wasi....maana naona anacheka tuu
 
Huyu Nchimbi kachokoza nyuki asitoke nduki huyu Lowasa wake atamtosa tu nyie subili atakavyo anza kukaangwa.....................

Nani atamkangaa kama alimpiga biti Rais wa nchi ktk uchaguzi wa Pinda.

Teh teh teh teh teh teh te nasikia pia ni mtaaluma wa kutundika makoti hewani teh teh teh huo ndio u DR wake kwi kwi kwi kwi kwi
 
Mkuu Tom,

....naona maneno yako yanatimia kuhusu Nape......however, kumbuka nilikuambia pia kuwa Nape hakukurupuka/sio mjinga.........subiri tuone mwisho wake...........just an update kwa tuliyoyazungumza huko nyuma....mkuu Tom.......vipi na wewe mandalizi ya kugombea ubunge mkuu.....nafikiri mpaka sasa hivi utakuwa umeshaona picha huwa inachezwa vipi i.e. Nape case is typical!!
 
Na huo mfano wake nae sijui,lengo lake lilikua ni kutoa tu huo mfano na si kutisha?
Hakutaka atakumtolea mfano mtuhumiwa mmoja wa RICHMOND au EPA...

Sasa kama anataka kutisha mtu kachagua the wrong target. Kuna siku Slaa aliambiwa unavunja sheria kuongelea skandali za madini Bungeni akamwambia Marmo, si mnikamate!

Halafu Polisi na DPP wao walipokuwa wanatafuta mafaili kwenye komputer za gazeti la Kubenea Slaa akawambia "ninayo mimi...nilishawaambia mimi ninayo"! Mzee keshachoka na uhuni wa CCM, kesha jidatia mtu yule haogopi mtu. Kikwete amtishe Slaa?
 
Mimi nimesema hii kauli ya WENDAWZIMU ni udhalilishaji,it's the time naop hao vijana wa CCM wasimame na kum-discipline mwenyekiti wao.Ni dharau ya hali ya juu.Tusipoheshimiana huko juu tutegemee kweli mtu wa chini kuheshimiwa na hasa Mtanzania wa kawaida? Nyerere alipoanza mapambano ya kulikomboa Taifa waingereza walimwita kijana mwendawazimu! Lilikua tusi kubwa,leo hii Nchimbi nae kalitumia.

Ni tusi dhini ya wanamapinduzi wote,lilaaniwe vikali
 
Back
Top Bottom