Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Kama vikao vinaendeshwa kwa ubabe namna hiyo, hapo ndio unaweza kusema kwamba utatumia vikao halali vya Chama ama Jumuiya kukosoa uongozi wa Chama ama Jumuiya?

Hivi mwanachama wa UVCCM anaweza kuvuliwa uanachama kwa pendekezo la mtu mmoja na Mwenyekiti akafanya maamuzi kwamba imepitishwa? Hiyo ni demokrasia?

Kama kanuni za UVCCM zina kigezo cha umri, kwanini mtu ahangaike kupoteza muda wa kumjadili mtu ambaye hana sifa inayotakiwa? Kwa mfano kama kigezo cha mtu kugombea urais ni miaka 40, halafu atokee mtu mwenye umri wa miaka 38 akagombea, kweli watu wanaweza kupoteza muda wao kukaa wanamjadili mtu ambaye hana sifa?

Kwanini Nape anawanyima usingizi wakati wanadai kwamba kigezo cha umri kinamtupa nje ya kinyang'anyiro? Kwanini waendelee kum-discuss mtu ambaye kanuni za Jumuiya yao zinamtupa nje?

Kama habari hiyo hapo juu ina ukweli kwa yale yaliyoandikwa, basi UVCCM na uongozi mzima una matatizo na hilo ni tatizo la ugonjwa unaoitwa ufisadi.

Kansa ya Ufisadi haitakuja kuondoka ndani ya CCM mpaka watokee wapiganaji wenye balls za kuwakemea wakubwa/viongozi kwa kuwaambia waache ufisadi na hilo ndiyo alilolifanya Nape na sasa naona vigogo wenye chama chao wameanza kumkoromea kwamba anawavua nguo. Sasa akaongelee kwenye kikao kipi wakati viongozi wa vikao vyote ni mafisadi.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini ni Lowassa (fisadi), Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CC ni Bwana Chenge nae pia ni fisadi. Kaimu Kamanda wa UVCCM ni Mzee Kingunge nae ni fisadi mzuri tu. Katibu Mkuu wa CCM ni mpambe wa mafisadi na mwana mtandao mzuri sana. Ukipanda juu kwa JK ndio huyo ambaye anawakwepa kuwashughulikia maswahiba zake. Hivi kweli hapo tutegemee mabadiliko kwenye uongozi wa Jumuiya za CCM? Maana akitokea mwanachama wa kuleta mabadiliko atafungiwa jiwe na kutupwa baharini ili azame na kuwaacha mafisadi wakitesa.
 
Mkuu FMES,

Nadhani Makamba ametoa kauli ambayo inaonyesha wazi kwamba CCM haiko tayari kukosolewa. Kwamba hata ukiona kiongozi anafanya ufisadi kaa kimya umtii kwa kuwa yeye ni kiongozi. Hivi kweli Makamba anaitakia mema CCM? Kauli kama hiyo inaweza kutolewa na kiongozi mkubwa wa chama kama Makamba? Watu wakae kimya huku ufisadi ukiendelea? Nani afichue huo ufisadi? Maana ufisadi wa serikalini ni kazi ya wapinzania kufichua. Lakini ufisadi wa ndani ya CCM ni jukumu la wana CCM wenyewe kufichua na siyo kukaa kimya eti kwa kuwa anayefanya ufisadi ni kiongozi.

Mbona Maregesi na yule katibu wa CCM wa Singida walioondolewa kwenye uongozi kwa tuhuma hizo hizo za ufisadi. Halima Mamuya nae aling'olewa UWT kwa sababu kama za mradi wa UVCCM. Leo kwa kuwa ufisadi umemgusa Lowassa ndio watu wakae kimya? Mbona hawakukaa kimya kwenye issue ya Mamuya? Lowassa ana nini ndani ya CCM?????
 
1.
Nadhani Makamba ametoa kauli ambayo inaonyesha wazi kwamba CCM haiko tayari kukosolewa. Kwamba hata ukiona kiongozi anafanya ufisadi kaa kimya umtii kwa kuwa yeye ni kiongozi. Hivi kweli Makamba anaitakia mema CCM? Kauli kama hiyo inaweza kutolewa na kiongozi mkubwa wa chama kama Makamba? Watu wakae kimya huku ufisadi ukiendelea? Nani afichue huo ufisadi? Maana ufisadi wa serikalini ni kazi ya wapinzania kufichua. Lakini ufisadi wa ndani ya CCM ni jukumu la wana CCM wenyewe kufichua na siyo kukaa kimya eti kwa kuwa anayefanya ufisadi ni kiongozi.

Unajua mkuu kinachoendelea ni vita vya ufisadi, sasa kuna makundi mawili ndani ya CCM, wanaounga mkono kundi la mfisadi la Lowassa na lile la wasiounga mkono,

Ni kweli kundi la wanaounga mkono lina wakubwa wengi sana kuanzia kina Msekwa, Kiungunge, Makamba, Chenge, Karamagi, Msabaha, na wabunge wengi sana,

Na kuna upande wa pili wa kina Mwakyembe, Sendeka, Kilango, Seleli na wengineo, sasa ninaamini unaweza kuelewa kinachoendelea huko UV-CCM ni cinema tu, lakini huu ndio ukweli kamili lakini it has nothing to do na chama cha CCM.


2.
Mbona Maregesi na yule katibu wa CCM wa Singida walioondolewa kwenye uongozi kwa tuhuma hizo hizo za ufisadi. Halima Mamuya nae aling'olewa UWT kwa sababu kama za mradi wa UVCCM. Leo kwa kuwa ufisadi umemgusa Lowassa ndio watu wakae kimya? Mbona hawakukaa kimya kwenye issue ya Mamuya? Lowassa ana nini ndani ya CCM?????

Ni kweli kabisa shutuma zao ni sawa kabisa na wote walitakiwa kufikishwa kwenye mikono ya sheria, lakini ndio hivyo tena bongo yetu mkuu, inakatisha tamaa lakini tutaendelea kujitahidi kuwapigia kengele tu, mpaka kieleeweke!
 
Mimi kinachonisikitisha ni kumshirikisha mzee wa watu Kawawa katika mambo kama haya.
I have a lot of respect for Rashid lakini hapa naona CCM wanamburuza katika mambo ambayo yanamshushia hadhi yake. Is he aware kuwa anatumiwa? Does he know that the CCM he is defending is not the CCM it was 20 years ago?
 
Kwa kweli imenisikitisha sana hili suala. mpaka natafakari uanachama wangu CCM. hii indumaza na kudhoofisha nguvu za kichama.

ILA YOTE YANAKUJA KWA KUWA MAKAMBA HANA SHULE NA MSEKWA KAPACHIKWA!!!!

Ingekuwa Malecela hali ingekuwa tofauti! yule bwana ni TREKTA kweli kweli!
 
With due respect, hivi NCHIBI UNA UMRI GANI UNAMPOMKATAA MWENZAKO?!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Just in Halmashauri Kuu ya UVCCM inayokutana Dodoma imemvua Uanachama wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Nape NNauye kwa sababu nyingine ikiwamo utovu wa nidhamu...wengine wenye habari zaidi watufahamishe zaidi.
 
Just in Halmashauri Kuu ya UVCCM inayokutana Dodoma imemvua Uanachama wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Nape NNauye kwa sababu nyingine ikiwamo utovu wa nidhamu...wengine wenye habari zaidi watufahamishe zaidi.

..eeh, habari ndiyo hiyo? duh!
 
Rais Kikwete asema siasa basi, sasa tuendeshe nchi kisayansi

Rais Jakaya Kikwete, ametoa tahadhari kuwa kuendesha mambo kisiasa hakuna tija ya kutosha isipokuwa kisayansi. RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba kama nchi ikiendelea kuzalisha wanasiasa kwa wingi itaishia kwenye malumbano na migogoro isiyo na tija, badala yake amewataka Watanzania kuijenga katika misingi ya sayansi na teknolojia.

Unapomvua uanachama wa UV-CCM, mjumbe wa NEC kama ni kweli then inakuwa ndio sayansi anayoisema mkulu hapa, only in Tanzania!

Kama ni kweli, sasa ni wakati wa Nape kujipanga upya na kutafuta nafasi zingine za uongozi ziko nyingi sana, sasa ni kazi ya CC ku-deal na uhuni wa jengo la vijana, Lowassa can do all lakini one thing ni kwamba hawezi kurudi tena kwenye power, ingawa sio siri kua atawasumbua sana wengine hasa huku kwenye nafasi za chini.
 
Duh! Hii CCM ndiyo mufilisi kabisa 🙁 Badala ya kumkumbatia Shujaa Nape wameamua kuwakumbatia mafisadi akina Lowassa na mafisadi wa kihindi. Mafisadi wote wa EPA, Richmond, Rada, Ndege ya Rais, Helicopters na magari ya jeshi bado wamekumbatiwa ndani ya chama hicho!! lakini mpambanaji wa mafisadi ndiyo wa kumfukuza!!!

Sasa tumepata uthibitisho rasmi kwamba kweli CCM ni Chama Cha Mafisadi na hawastahili kabisa kuwepo madarakani kwa kuwa matatizo yetu mengi Tanzania yanasababishwa na CCM.

CCM ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya Tanzania.
 
Nape! Mhanga wa utetezi wa ufisadi.

Basi aende upinzani na mambo yasonge mbele. Maana mapambano ni makali sana. Ataki, na abaki huko na ajiunge na mafisadi.

After all kwani mapambano lazima uwe katika chama cha mafisadi? au chama kingine chochote?

Wengine tunapambana bila vyama, na mapambano ni makali sana.
Nape karibu. Tupambane tukiwa nje ya vyama vyao. tuone mwisho ni upi yaani nani ataibuka mshindi.
 
.......wait a minute, hicho kikao cha kumvua wamefanya lini na saa ngapi?
 
Nao hawakusita kuchukua maamuzi magumu na mazito

Inaonekana Nape alikua anatoboa siri za chama-teh teh teh.

yawezekana nape alikua anawafitinisha viongozi wa chama teh teh teh.

Ama naye CHIMBI alisimama ktk kikao na kunena.
Hayuko tayari kumwachia uenyikiti NAPE ama yeye avuliwe uanachama ama yeye Nchimbi abwage manyanga teh teh teh teh.
kazi kweli kweli
 
sisemi mengi sasa na nyodo za kina uneducated makamba,phony & unqualified Nchimbi,200yrs old Kawawa,out of touch Lowassa na mafisadi wengine naona zimenipa steam ya kutosha to do something right...its hard to believe hiki ndio chama tawala na tunasubiri kitatuongoza vizuri kwa haki na kupata maendeleo hii karne ya 21,kuanzia leo nitafanya kila niwezalo kuing'oa CCM na nitaanzia jimboni kwangu kwenye nafasi ya ubunge...i'll use every weapon to my disposal kuanzia money,brain,influence,time etc,kukubali kutawaliwa na kushindwa kila chaguzi na CCM sasa ni kitu kisichokubalika na siamini kama hawa ni soooo smart kuendelea kutushinda...kila mtu afanye kitu sio kulalamika hapa tuu!
 
Kikao kilikuwa kinfanyika leo Dodoma, habari nilizopata sasa ni kwamba ukweli:-

1. Makamba na Nchimbi, with a back up ya Lowassa, na Kingunge walitoa mapendekezo ya kumvua uanachama wa UV-CCM, ili hatimaye asigombee uenyekiti wa UV-CCM.

2. According to habari nilizozipata sasa hivi kutoka kwenye kikao hicho ni kwamba wana uwezo wa kumvua uanachama wa UV-CCM temporarly, na baadaye the ishu itakwenda CC, kabla ya kikao kuisha tarehe 9.

3. Kwa sababu ya wakulu wengi kuhusika na hii idea, inakubalika na wengi ndani ya CCM kuwa itakuwa ni ngumu sana kwa Muungwana, ku-side na Nape huko CC, maana yeye kwenye hili ndiye muamuzi wa mwisho.

Anyways, tunaendelea kufuatilia kwa karibu na makini yaliyojiri since so far hayajapatikana yote kwa uwazi.
 
Back
Top Bottom