Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sasa kama anataka kutisha mtu kachagua the wrong target. Kuna siku Slaa aliambiwa unavunja sheria kuongelea skandali za madini Bungeni akamwambia Marmo, si mnikamate!

Halafu Polisi na DPP wao walipokuwa wanatafuta mafaili kwenye komputer za gazeti la Kubenea Slaa akawambia "ninayo mimi...nilishawaambia mimi ninayo"! Mzee keshachoka na uhuni wa CCM, kesha jidatia mtu yule haogopi mtu. Kikwete amtishe Slaa?

mkuu,

Wanamapinduzi wenye misimamo kama hiyo ndiyo wanaoweza kufanya kitu mkuu.Unajua JK bado anafikiri kila mtu siku hizi anaogopa kukamatwa na polisi.
 
Sasa kama anataka kutisha mtu kachagua the wrong target. Kuna siku Slaa aliambiwa unavunja sheria kuongelea skandali za madini Bungeni akamwambia Marmo, si mnikamate!

Halafu Polisi na DPP wao walipokuwa wanatafuta mafaili kwenye komputer za gazeti la Kubenea Slaa akawambia "ninayo mimi...nilishawaambia mimi ninayo"! Mzee keshachoka na uhuni wa CCM, kesha jidatia mtu yule haogopi mtu. Kikwete amtishe Slaa?

We Pimbi Mzushi hebu tupe updates za "investigation" yako kuhusu dokta Masau na potential lawsuit......
 
Hata Mrema naye alibatizwa hilo jina la Mwendawazimu, au?

sadakta, haya huyu naye aliwaita waislam waliovunja mabucha ya Nguruwe back in 90's kuwa ni wendawazimu

2790.png
 
Nape ajibu mapigo

Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kufukuzwa kwenye Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Baraza Kuu la umoja huo, Nape Nnauye ameibuka leo asubuhi na kuwataka wanaomuunga mkono wasikate tamaa kwa sababu mapambano bado yanaendelea.

"Najua kuna wanachama wengi wananiunga mkono. Nawahimiza wasikate tamaa kwa sababu haki itajulikana vikao vya juu vya chama vitakapokaa na kubaini ukweli wa jambo hili. Bado tunaendelea," amesema Nnauye alipozungumza na mwandishi wa habari hizi leo asubuhi.

Amesema kwamba anajua wapo wanachama na wasiokuwa wanachama wa CCM wanaomuunga mkono na kuwataka wasikatishwe tamaa na yaliyotokea Dodoma jana mjini Dodoma.

Kuhusu kauli ya Baraza Kuu la UVCCM kwamba alisema uongo kuhusu mradi wa jengo la UVCCM, amesema asingeweza kulizungumzia hilo kwa sasa kwa sababu linashughulikiwa na Kamati Kuu ya CCM lakini akasema anatarajia kwamba haki pia itatendeka.

"Sitaki kulizungumzia zaidi suala hilo kwa sasa lakini ninaamini penye haki, dhuluma hujitenga na wananchi watakuwa mashahidi," amesema.

Amemlaumu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akisema kwamba akiwa Kamisaa Mkuu wa uchaguzi wa UVCCM maamuzi yake yameegemea upande mmoja.

Baraza Kuu la UVCCM jana lilimvua uanachama Nape katika kinachodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya chama pamoja na kumwengua rasmi katika kinyang'anyiro cha kuwania uenyekiti wa umoja huo katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Nape amekuwa gumzo kubwa katika uchaguzi huo kutokana na kulipua alichokiita bomu la ufisadi kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM jijini Dar es Salaam.

Kijana huyo amekuwa akiwataka mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu, Kaimu Katibu Mkuu, Francis Isaac na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Edward Lowassa wawajibishwe kwa kupitisha mradi ambao anadai hauna maslahi kwa umoja huo.

Alitoa hoja hiyo muda mfupi baada ya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa UVCCM, nafasi ambayo ni nyeti kwa vile inampa mhusika kushiriki kwenye vikao vya juu vinavyotoa maamuzi mazito kwenye chama tawala.

Mwanasiasa huyo chipukizi amekuwa akinukuliwa mara kwa mara akidai kwamba mkataba huo ulipitishwa kinyemela hata kabla haujafikishwa kwenye vikao vya juu vya CCM.

Nape pia amekuwa akiweka alama ya kuuliza kwenye uhai wa mradi huo hasa katika kipengele kimojawapo ambacho kinasema kwamba mwekezaji ataendeleza mradi huo milele, huku Jumuiya hiyo ikipata asilimia 25 na mwekezaji akipata asilimia 75.

Tusubili news kamili kesho au jioni hii hii
 
Hivi huyu Nape anataka kuongoza umoja wa Vijana lakini mbona bado anatumia tactics za 1947?

Hivi hana BLOG huyu? hapo ndipo ninapowapendea CHADEMA maana karibuni wote ambao wako active kwenye net wana BLOGS regardless hata kama wao wanaonekana wendawazimu lakini at least they are in the game

no wonder huyu NAPE katimuiliwa
 
Haya mambo tuna kila sababu ya kuangalia kwa kina kuwa ni kwanini yanatokea sasa ,
\kwani ukiangalia kwa kina utaanza kujiuliza kuwa wale wana NEC ambao walitaka mafisadi wa EPA wachukuiw hatua hawatakuwa na mjadala kikao cha keshokutwa huko Dododma maana sasa issue itakuwa NNAPE.

Wenzangu na miye wa Zanzibar na hoja yao kuwa ni nchi ama laa na mjadala ambao huenda ungeweza hata kubadilisha historia ya taifa hili sionio kama utakuwepo tena kwani issue sasa ni Nnape.

Wale waliohoji kuhusu Richmond ,mjadala huo hautakuwepo tena kwani umezimwa kisayansi na kwa kutumia mbinu za kikomunist kwelikweli.

Kwani sioni kama ni kweli kuwa hawa wazee akiwemo kawawa eti wanaweza wakawa wamefanya walichofanya bila kufanya political calculations za kutoshga na haswa kuhusiana na madhara ambayo wanaweza kuyapata baada ya uamuzi huo.

Nnape , anapaswa kuamua moja na kama kweli alikuwa ni mtu anayepingana na ufisadi hana budi sasa kufanya maamuzi mazito ,na hilo litampa kinga ya kuendelea kuishi kwani akiwa humohumo kikitokea chochote atakuwa amemalizika kwa stsil ile ile.\
\
Najaribu kuijitahidi kuangalia haya mambo kwa upana wake na haswa hao waliojihusisha kumngoa ,naona baraka za Mwenyekiti wa Chama taifa yaani Kikwete mwenyewe, ama pia wanaweza kuja kesho na kusema kuwa CC imeamua kumrejesha kwani vijana waliamua kwa jaziba ila kutokana na ukweli kuwa vijana hawamtakio basi hawezi kuwa kiongozi wao na hivyo asiwe mgombea.
 
Mheshimiwa,

Niliipitia ile iliyowekwa hapa na Mwanakijiji, nikaona inafanana fanana na kile alichosema Rais. Manake kuna maneno mule ya mtaani taani Rais aliyatumia naona yamo humo pia, kwa hiyo inawezekana ni ile yenyewe ambayo haijahaririwa.

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=17595

Aliposema akitaka anaweza kumwambia IGP akukamate imo pia. Nadhani hii ndio yenyewe, au ?
Kuhani,
Ni kweli unachosema. Iliyowekwa kwenye JF na audio mbalimbali zilizorekodiwa live siku ya tarehe 21 zipo. Lakini official version ya Ikulu nani kaiona hadi leo?

Hata version ya Hansard ambayo kwa kawaida inatoka immediately, hata leo haipo. Ni vema kujiuliza hii maana yake nini? Alichokisema kimeenda kuhaririwa in line na alichokisema off record? Imeenda kuandikwa upya na kimsingi alikuja na version gani na ipo wapi na kama ali devert ni kwanini Rais alidevert kwenye version iliyokuwa imeandaliwa, ukiacha michapo ya hapa na pale ambaye watoa hotuba wengi hufanya hivyo! Tuko hali ngumu kama nchi!
 
Haya mambo tuna kila sababu ya kuangalia kwa kina kuwa ni kwanini yanatokea sasa ,
\kwani ukiangalia kwa kina utaanza kujiuliza kuwa wale wana NEC ambao walitaka mafisadi wa EPA wachukuiw hatua hawatakuwa na mjadala kikao cha keshokutwa huko Dododma maana sasa issue itakuwa NNAPE.

Wenzangu na miye wa Zanzibar na hoja yao kuwa ni nchi ama laa na mjadala ambao huenda ungeweza hata kubadilisha historia ya taifa hili sionio kama utakuwepo tena kwani issue sasa ni Nnape.

Wale waliohoji kuhusu Richmond ,mjadala huo hautakuwepo tena kwani umezimwa kisayansi na kwa kutumia mbinu za kikomunist kwelikweli.

Kwani sioni kama ni kweli kuwa hawa wazee akiwemo kawawa eti wanaweza wakawa wamefanya walichofanya bila kufanya political calculations za kutoshga na haswa kuhusiana na madhara ambayo wanaweza kuyapata baada ya uamuzi huo.

Nnape , anapaswa kuamua moja na kama kweli alikuwa ni mtu anayepingana na ufisadi hana budi sasa kufanya maamuzi mazito ,na hilo litampa kinga ya kuendelea kuishi kwani akiwa humohumo kikitokea chochote atakuwa amemalizika kwa stsil ile ile.\
\
Najaribu kuijitahidi kuangalia haya mambo kwa upana wake na haswa hao waliojihusisha kumngoa ,naona baraka za Mwenyekiti wa Chama taifa yaani Kikwete mwenyewe, ama pia wanaweza kuja kesho na kusema kuwa CC imeamua kumrejesha kwani vijana waliamua kwa jaziba ila kutokana na ukweli kuwa vijana hawamtakio basi hawezi kuwa kiongozi wao na hivyo asiwe mgombea.

Hapa ilikuwa mh JK atumie busara zake kumaliza makundi yanayojijenga ndani ya chama chake, lakini mh raisi na mwenyekiti wa chama cha mafisadi ni mtu wa porojo bila nguvu ya utekelezaji, nillisha kata tamaa mapema sana. Pale alipokuja na orodha ya wala rushwa, madawa ya kulevya, majambazi eti anawapa muda waache...raisi huyo...inakuja EPA kamati juu ya Kamati...kama haitoshi anawaongezea muda wezi, kali zaidi Katibu Kiongozi naye anasema wahusika wana familia tuko makini.....Nape amejimaliza mwenyewe ...Mwenyekiti JK atamchinjia baharini hata damu yake isionekane.....
 
One thing is surely true. CCM chama kubwa, yaani uchaguzi wa UVCCM kila mtu yupo alerted. Pilipili msio ila yawawashia nini? Si mna Chadema yenu leave them alone chama chao acheni wafanye watakavyo na nyie mna vyenu. Get life guys..
 
BUSARA gani tena? kama alishindwa busara ya kawaida ya kuwatia ndani waliotutesa kwa kutuibia mabilioni ya fedha .

Akitumia busara kwa NAPE nitamshangaa sana.

Maana Nape ni mgogoro wao wenyewe hukohuko uvccm lakini gogoro la FEDHA ZETU linatugusa wote.

Hata NAPE wakimtosa huko ccm mimi hainiumi maana ana options nyingi LAKINI wakitutosa fedha zetu zimepotea hizo na zitatugharimu miaka mingi kuripa kodi.
Atumie BUSARA kwanza kwa MAJAMBAZI kuyapa mda wa kurudisha vitu walivyotujangili.
 
Kwenye hii dunia ya blogs na habari kuvuja, kufukuzana kwenye uongozi au uanachama
ni kitu ambacho viongozi inatakiwa mukiache.

Kama kina Nyerere walikuwa na uwezo wa kuwafukuza watu kirahisi, msifikiri mwaka 2008 bado mtaendelea kuwanyamazisha wenye mawazo tofauti na nyie kwa kuwafukuza uanachama au kazi.

Kwenye siasa hakuna adui kama ambavyo hakuna rafiki. Mtu anaweza kufukuzwa kama tu atakiuka maadili ya uongozi. Maadili hayo ni yale yanayoendana na sheria za nchi na wala sio hii ya sasa, ukikosana na Mwenyekiti tayari inakuwa balaa.

Imagine hapa JF tungelikuwa tunafukuzana kwasababu tu tumekosana na Invisible, Mwanakijiji au FMES. Naamini wengi tungelikuwa tumeshahama blogs.

Hivi Nchimbi kweli anafaa hata kuwa waziri? Kama kanamshinda kajumuia haka kadogo, kweli huyu mtu ana management skills za kumfanya hata awe waziri?
 
One thing is surely true. CCM chama kubwa, yaani uchaguzi wa UVCCM kila mtu yupo alerted. Pilipili msio ila yawawashia nini? Si mna Chadema yenu leave them alone chama chao acheni wafanye watakavyo na nyie mna vyenu. Get life guys..

Hapana tunaongelea demokrasia .

Hata marehemu chacha aliposimamishwa chadema tulisema ila walikuwepo watetezi leo hii wanaoishangaa hatua ya uvcmm wakati nao waliichukua hiyohiyo.

Sisi tunachopinga hapa ni mtindo wa kufukuzana baada ya viongozi wa juu wa vyama kutuhumiwa.

Na kwanini wanakimbilia kutimua watu badala ya kuijadili hoja ? huu ubabe ndio hatutaki kuuona nchini kwetu.
watu huru tutapinga kilakinachotupeleka kusiko

Tatizo liliopo saizi ni JK kua nae anahusika moja kwa moja na ufisadi na anajua fedha zilikokwenda na njisi walivyozitumia ,sio muoga kufanya maamuzi maana jamaa namfahamu ubabe aliokua anafanya bagamoyo ila amuonee nani kumfunga wakati yeye anajua fedha zilikoenda.

Lowasa ndio Engineer wakati NCHIMBI na Makamba ndio ma TECHNICIAN wakati JK ni mananging director.

Mbowe naye ni tatizo sihitaji kwenda mbali.

Hapa solution ni wafanyakazi wote nchi nzima wagome kufanya kazi ,watu wagome kununua kitu chochote washinikize serikali abwage manyanga.

Na serikali ishikiliwe na Ma engineers pamoja na madaktari miaka mitano ndipo uchaguzi wa kisiasa ufanyike.

Vinginevyo tutapiga kelele bila mafanikio.Ukombozi wetu sasa unategemea tu wafanyakazi.

Hapa ni wafanyakazi
 
Kuhani,
Ni kweli unachosema. Iliyowekwa kwenye JF na audio mbalimbali zilizorekodiwa live siku ya tarehe 21 zipo. Lakini official version ya Ikulu nani kaiona hadi leo? Hata version ya Hansard ambayo kwa kawaida inatoka immediately, hata leo haipo. Ni vema kujiuliza hii maana yake nini? Alichokisema kimeenda kuhaririwa in line na alichokisema off record? imeenda kuandikwa upya na kimsingi alikuja na version gani na ipo wapi na kama ali devert ni kwanini Rais alidevert kwenye version iliyokuwa imeandaliwa, ukiacha michapo ya hapa na pale ambaye watoa hotuba wengi hufanya hivyo! Tuko hali ngumu kama nchi!

Nakubalina nawe kabisa ndg. Slaa, kama taifa limeweza kuhutubiwa na rais, na spika wa Bunge anasema hotuba ya rais haiwezi kujadiliwa kwani ina maneno yake mwenyewe mengi na imekosa mtiririko, basi binafsi nadhani tuna hali ngumu kama taifa, kwani nashindwa kuelewa ni mahali gani tunaweza kumuamini rais wetu tena pale atakapolihutubia taifa au bunge.
 
Achaneni nao dawa yao inachemaka, mbona hawatoki online wakasema kama sisi tunavyosema kama si kweli ni mafisadi?
 
One thing is surely true. CCM chama kubwa, yaani uchaguzi wa UVCCM kila mtu yupo alerted. Pilipili msio ila yawawashia nini? Si mna Chadema yenu leave them alone chama chao acheni wafanye watakavyo na nyie mna vyenu. Get life guys..

oh well... "kila mtu" is such a blunt statement!
 
Back
Top Bottom