Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Jamani naanza kupata uoga.wasije wakamtoa roho huyo kaka jamani.maana nawaogopa hawa watu wanaojifanya wao ndio wenye nchi.

Mtu Kwao,

Hat mie nimesema wafanye yote but Roho ya huyo kijana wasiiguse.....lakini muda wa mabadiliko ni sasa.Kama mwanamapinduzi hali ni lazima ukumbane nayo,but keep on daring and dare forever.The wind of change is blowing from South to North,East to west.Keep on daring buddy!
 
Mkuu,

Wafanye yote lakini wasiiguse roho ya huyo kijana......Eti,CCM wamuenzi tena baba yake?


Mkuu,utashangaa na hata wakifanya hivyo hata mie nitashtuka sana.Ni lugha ya kigeni kabisa
Hilo ndilo linaniogopesha mkuu mana huyu jamaa watu anaokwaruzana nao wanakufa.sijui ni woga au nini, mimi sijui
 
Jamani naomba kuuliza KUGOMBEA UENYEKIYI UV-CCM UNATAKIWA KUWA NA UMRI GANI?
2. HUYU NCHIMBI ANAMIAKA MINGAP NOW?

3. Kwanini Makamba, Kingunge,Mzee Kawawa na Nchimbi wamekuwa na kiburi namna hii hii jeuri wanaipata wapi lazima kuna chimbuko lake.
Na kwanini wanaendelea Kumwenzi Lowasa huyu Lowasa ana nini cha ajabu kinachomfanya awe na kiburi kiasi hiki. Au ni hizo pesa za EPA ,RICHIMOND ndizo zina mtia kiburi?
Kwanini hadi sasa JK anaendelea kuwabembeleza hawa Mafisadi? NADHANI SASA NI WAKATI MUAFAKA JK AKAACHA SHERIA IFANYE KAZI YAKE BILA KUANGALIA HUYU NI MKWA AMA MDOGO.
5. NAPE kuwa makini wasije kukufanyia kitu mbaya kama IPI MALECELA,KOLIMBA N.K.

Wasiwasi wangu tu Halmashauri ya CC itakayo kaa leo isije ikafuata mkumbo wa huyu FISADI NCHIMBI, yaelekea 75% ya CCM inakumbaia mafisadi sasa hiyo iliobaki 25% ina kazi ya ziada ya kusafisha Chama kuanzia chuni hadi juu asivyo patachimbika kama sio kukalika ktk uchaguzi mkuu 2010.- Nimtazamo wangu tu
 
Sasa ianbidi kijana Nape asimame kama mitume walivyosimama ,wasiwaogope akina Farao.Bahari ya shamu ni pana lakini ukitanguliwa na nguzo ya moto utapita tu
 
Muda simrefu ccm watatwangwana makonde ndani ya vikao vyao kama wenzetu wa kenya na uingereza kama sijakosea ktk vikao vyao
 
Muda simrefu ccm watatwangwana makonde ndani ya vikao vyao kama wenzetu wa kenya na uingereza kama sijakosea ktk vikao vyao

Kenya na Asia wanatwangana mangumi lakini sio UK. Wenzetu UK pamoja na kulimana sana vijembe lakini hata siku moja hawawezi kutwangana ngumi bungeni.

Kupigana ngumi ni matokeo ya hoja za manguvu. Dawa ni kusikiliza hoja za wengine hata kama hukubaliani nazo na pia kutenda haki kwa watu wote.
 
Mkisikia kulikologa ndo hili uongozi wa MAKAMBA,NCHIMBI na BABU KINGU ni wa kukalili.....wamechemka sana eti wao wasiulizwe na vijana kwa vile ni wazee.....duh hii kali JK kama unajua hawa watu ndio wanao kuvulugia mipango yako na kukuzunguka.
Hapo sasa Nape ndo mnampa umaarufu wa hali ya juu sasa atauzika jimbo lolote akitaka kugombea ubunge huyu kijana.
 
Labda,kwa hao wazee niwaulize swali linalohusina na wanachoita heshima.Je,baba akimbaka bintiye,bado ataendelea kutegemea heshima kutoka kwa huyo binti? Ni kwa nini ategemee respect kutoka kwa huyo binti? kwa kigezo kipi? Urefu wa umbo na mvi pamoja na kuwa na miaka mingi tu? HAPANA HILO halitoshi kuwa tu kigezo cha kutaka heshima wewe kama mkubwa,kuna la ziada!
 
Mkisikia kulikologa ndo hili uongozi wa MAKAMBA,NCHIMBI na BABU KINGU ni wa kukalili.....wamechemka sana eti wao wasiulizwe na vijana kwa vile ni wazee.....duh hii kali JK kama unajua hawa watu ndio wanao kuvulugia mipango yako na kukuzunguka.
Hapo sasa Nape ndo mnampa umaarufu wa hali ya juu sasa atauzika jimbo lolote akitaka kugombea ubunge huyu kijana.

Mkuu wangu,

Heshima mbele.Hawa ni wendewazimu kwani wanatumia misuli ya mikono na midomo kuliko kushirikisha hata mishipa ya kupeleka damu ubongoni.

Kweli mkulima kala Mbegu,ategemea kutuua njaa!
 
--------------------------------------------------------------------------------

Taarifa ya Habari TBC, Nape anakaririwa akisema hakusudii kukata rufaa kwa sasa kwa kuwa Baraza Kuu si Kikao cha mwisho katika CCM ingawa amevuliwa uanachama UVCCM na kupendekezwa kuwa avuliwe nafasi zote za uongozi katika CCM. Amesema anaamini kuwa ametumia haki yake ya kidemokrasia kuelezea hisia zake ya mambo yaliyotokea UVCCM

Maoni yangu:
Inaonekana kuna vuguvugu la chinichini katka CCM na vikao vinavyofuata tutasikia tutasikia maamuzi na mapendekezo ya Baraza Kuu UVCCM yakatupiliwa mbali na kuwaaibisha vibaya Wajumbe wa Baraza Kuu. Hii itapelekea vita vya chini kwa chini kuongezeka ndani ya CCM.
__________________
 
TBC wanamhoji mojakwa moja live sasa hivi
 
Anasema msimamo wake juu ya ujenzi wa Jengo la UVCCM liko palepale.
 
This thing is incredible, maneno ya hii kitu inakuwa very interesting nimebahatika kuongea na wanaohusika, sana na this whole thing:-

1.According to deal ni kwamba Rais alipomteua Pinda kuwa PM kabla ya kuvunja baraza la mawaziri, kulikuwa na kikao cha CCM na joint UV-CCM, ambacho kilikuwa na lengo la kutoa azimio la kumpongeza Rais kwa chaguo lake, la Waziri Mkuu mpya.

2. Nchimbi akagoma akisema kuwa Uv-CCM au yeye under any capacity, hawezi kuwa involved na huo ujinga kwa sababu yeye hamtambui Pinda, kwa hiyo he is out na hilo azimio. Ujumbe ukafikishwa kwa rais kama ulivyo, na according to more dataz ni kwamba kwa makusudi mazima wale wote aliowapandihsa chati Nchimbi, kupitia UV-CCM, kina David, Masha, na Kamalla wakapewa uwaziri kamili.

3. Nchimbi akatanagaza rasmi ndani ya vikao vya CCM kuwa yeye sasa ni mfuasi wa Lowassa, kwa 100% na kwamba no matter what Pinda is no body to him, na kwamba majuzi Nchimbi alipoamua kumtumia muandishi wake kuandika uongo kuhusu habari za jengo na Nape huko CC, ni muungwana mwenyewe aliyempigia simu mwenyekiti wa IPP, akitaka kujua huku akifoka kuwa hiyo habari nani aliyeipeleka huko Nipashe, mwandishi alipobanwa ndio akatema sumu yote na kumtaja Nchimbi. Ni baada ya mkwara mzito sana aliopewa mwenyekiti wa IPP, ndio maana Nipashe wakaomba msahama na hata kumtaja waziri anyewapa habari za ndani za CC.

4. Ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewaagiza UV-CCM kukutana jana, kuamua kuhusu majina na sio anything else, sasa according to the dataz ni kwamba Nchimbi na Makamba wanasubiriwa sana na CC, kwa sababu Kingunge haingii tena CC, nimedokezewa na wajumbe kama wanne wa CC kuwa huko kutawaka moto siku ya tarehe 9, maana no way hii kitu ya Nchimbi inaweza kupita huko kwa sababu wanajua kuwa ikifika NEC itakuwa aibu kubwa sana kwa CC wanaweza kuzomewa kama Butiama na muafaka, the dataz ni kwamba Nape ameambiwa atulie na kusuubiri tarehe 9.

My Take:

Kwa kweli sasa hili taifa tumefika mbali sana, yaani the lowest mark kwa any president aliyewahi kuliongoza taifa hili, I mean Nchimbi anwezaje kuwa na utovu wa adabu kiasi hiki na bado akapewa uwaziri mdogo wa Ulinzi kama adhabu? Haya ni mambo ya aibu sana sio tu kwa mwenyekiti wa CCM na viongozi wote wa CCM, bali ni kwa wananchi wote wa taifa hili. I want kuamini kuwa CC itasimama kidete na kumfundisha adabu Nchimbi, otherwise tutakuwa tumekubali kuwa under mafisadi, tunaisubiri kwa hamu tarehe 9, kusikia maamuzi ya mwisho.

Ahsante Wakuu na Tunaendelea Kufuatilia Kwa Makini na Ukaribu Sana hizi Stunning Events. Kesho Tutakuwa Na Zaidi Ya Yalioyjiri na Pia Tutazungumza na Nape Mwenyewe.

Mkuu asante sana, siasa za bongo wazijua nimekuvulia kofia...endelea kutuhabarisha...maisha ya dogo Nape yako hatarini kila anayegombana na Nchimbi mauti humkumba....natamani kutuma rambi rambi kwa familia ya Nape
 
Mkuu wangu,

Heshima mbele.Hawa ni wendewazimu kwani wanatumia misuli ya mikono na midomo kuliko kushirikisha hata mishipa ya kupeleka damu ubongoni.

Kweli mkulima kala Mbegu,ategemea kutuua njaa!


Unajua kumeguka kwa CCM ndo hapa sasa kumeanza watu sasa wanagundua kuwa kuna watu wanajiona wao kama wafalme hawatakiwi hata kuguswa sasa matabaka yamesha anza kuna tabaka la wenye nazo ndo hilo la JK humo ndani yake wamo wale wooote wachafu ambao tunawajua..........
 
I said about this siku nyingi sana,

Mie nimeamua kuwa mkimya tu na kuendelea na shughuli zangu..
 


Mkuu asante sana, siasa za bongo wazijua nimekuvulia kofia...endelea kutuhabarisha...maisha ya dogo Nape yako hatarini kila anayegombana na Nchimbi mauti humkumba....natamani kutuma rambi rambi kwa familia ya Nape



Mkuu,

Si angalao umalizie na neno Natania?

Kwanza hebu tema mate chini mkuu!
 
Mwandishi mahiri Padri Karugendo alibashiri kuanguka kwa Nape Mnauye mwezi August 08. Alisema katika semina ya kutathini uchaguzi wa 2005 Karugendo alifichua ufisadi wa CCM yeye akiwa kama mmoja wa waagalizi wa uchaguzi huo. Nape alipinga na kumtukana Karugendo kwa kuichafua CCM. Wakati wa mapunziko Karugenmdo alimwita Nape na kuongea naye kwa kina bila mafanikio.Kwenye biblia inasimulia jinsi Saulo aliyekuwa muovu aliokoka akiwa njiani kwenda Damascus na kuwa Paulo ambaye alikuwa muhubiri mahili wa injili. Lakini Mt. Paulo aliteswa sana na mafarisayo. Tumfananishe Nape na Saulo amabaye alibadilika kuwa Paulo hivyo ategemee shuluba ndani ya CCM. Na ndivyo imekuwa! Je, Nape atarudi nyuma? Saulo hakurudi nyuma.
 
Unajua kumeguka kwa CCM ndo hapa sasa kumeanza watu sasa wanagundua kuwa kuna watu wanajiona wao kama wafalme hawatakiwi hata kuguswa sasa matabaka yamesha anza kuna tabaka la wenye nazo ndo hilo la JK humo ndani yake wamo wale wooote wachafu ambao tunawajua..........

Mkuu,

hiyo ndiyo mojawapo ya sababu zilizoiangusha hata USSR. Wacha anguko litimie.
 
Back
Top Bottom