Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

According to the dataz ya baadhi ya yaliyojiri ni kwamba:-

1. Wahusika wote wakuu wa EPA, toka wiki iliyopita wamekuwa wakiwatafuta wenyeviti wa mikoa wa UV-CCM, kwa kumtumia mwenyekiti mmoja kutakla kuwapa hela kwa ajili ya msimamo wa kumfukuza uanachama Nape, huko Dodoma.

2. Huyu mwenyekiti akapata tatizo kwamba wengi wao walikataa kwamba wako upande wa Nape, ndipo Tom Mwang'onda akatumwa kuwahi Dodoma in advance akiwa na hela nyingi sana kwa ajili ya hii shughuli ambapo dau lilikuwa kuanzia shillingi millioni moja mpaka mbili, kulingana na nafasi ya umuhimu wa mjumbe kwenye baraza la Uv-CCM.

3. Kikao kilipoanza, aliyekifungua ni Nchimbi, akatumia nusu saa kumtukana sana Nape, akafuatia Ngombale yeye akatukana wote kuanzia Nape mpaka wabunge wanao kikosoa chama, ndipo alipofuatia Makamba ambaye aliongea kwa karibu masaa mawili akiwatukana sana Nape na wabunge kina Mwakyembe, wakati wote huu Kawawa alikuwa amekaa kimyaa, ilipofika zamu yake, Kawawa alizungumzia vijana na kilimo na hasa kilimo cha matrekta, alipomaliza tu akaondoka na hakurudi tena, kwa sababu kilichotakiwa pale ni kuonekana tu kuwa angalau alikuwepo.

4. Baada ya Kawawa tu kuondoka, kukawa na kikao cha kamati ya utekelezaji ambapo Nape, aliitwa na kuulizwa maswali mengi sana kwamba kwa nini amesema uongo kuhusu jengo, akatakiwa aende kwenye public na kusema kuwa anaomba radhi kwa kusema uongo, kitu ambacho Nape alikataa kata kata kuwa hana mpango wa kubadili msimamo.

5. Ndipo usiku kukawa na kikao cha kupitisha majina, ambapo Nape alitoka nje hasa ilipoanza nafasi ya mwenyekiti, alipotoka tu Nchimbi akawaaambia wajumbe kua ana hoja nzito toka kwa kamati ya Utekelezaji, nayo ni kufukuzwa uanachama kwa Nape, wajumbe wwengi wakaja juu kuwa haiwezekani, kuona hivi Makamba akasimama na kuchukua fomu ya Nape huku akiionyesha kwa wajumbe, aliwaambia kuwa Nape ni mtoto wake na ndiye pekee anayemjua mle ndani kuliko wote,

- Na kwamba ameshaongea naye sana kuhusu hili tatizo, kwa hiyo wasijifanye wanajua sana, hiyo ya kufukuzwa kwake Nape yeye ameshaimepitisha tayari na hata huko mbele yeye ndiye atakayekwenda kutoa maelezo zaidi sio wao, wajumbe wakabaki na mshangao na Mkamba akiendelea kuwatisha kuwa hapa tatizo sio Nape tu ila wale wote wanaomuunga mkono nao wote lazima watajadiliwa kwa kina na kufukuzwa pia, hapo ndipo wajumbe wakapitisha hiyo hatua ya kumfukuza Nape, baada ya kikao kufungwa wajumbe wakiwa wanajitayarisha kuondoka ndipo mjumbe mmoja akasimama na kusema kwa sauti kubwa sana kuwa kwa nini Nape asianyang'anywe kadi pia?

- Mwenyekiti Nchimbi kwa tabasamu kubwa sana akasema kwa nguvu sana kuwa hiyo nayo imepitishwa.

6. Hiki kikao ukweli ni kwamba kimeruka kanuni nyingi sana za umoja huo na CCM kwa ujumla, kwa sababu according to wanaojua vizuri mambo ya CCM, ni kwamba CCM kama chama inatawaliwa na kanuni moja tu ya maadili na usalama wake, kanuni yake ya Ibara ya kati ya 87 na 89 ni kwamba,

-Kiongozi yoyote wa taifa kama Nape, akifanya makosa against CCM, anatakiwa apewe;-

1. Onyo. 2. Onyo kali. 3. Karipio. 4. Kufukuzwa.

Meaning kwamba kufukuzwa ni baada ya hatua zote tatu za mwanzo kushindwa, sasa Uv-CCM wanatakiwa kuwakilisha adhabu yao kwa CC, swali la kwanza litakuwa je ni vipi kanuni zilifuatwa?

Wakuu haya ni baadhi tu yaliyojiri na hii sagga na tutaendelea kuyamwaga zaidi, kama tunavyoyapata lakini support imekua kubwa sana kwa kijana Nape, hii habari imewashitua wakulu wengi sana na hasa uwt, kwa maoni yangu jina la Nape halitarudi kwenye wagombea kwa sababu ya umri, lakini hili la adhabu hapana hilo halitasimama, na kuna wananchi wengi wanachama wa CCM, wanaomtaka arudishe kadi ili wajiunge naye hiyo siku ya kurudisha.

Ahsante wakuu, na tutaendeela kuhabarishana yanayojiri.
 
Tunavyo jua CCM kwa unafiki unaweza ukasikia wanaandaa maandamano ya kuwapongeza akina Makamba,babu Kingu na Nchimbi kwa kazi nzuri.....si mnawajua hawa kwa kuandaa maandamano.....
 
...mnawapa sana attention hawa,hawana issue waacheni wamalizane wenyewe maana watakuwa wametupunguzia matatizo sana,target yangu sasa ni Mbunge wa jimbo langu,tumeanza kuunda timu ya wataalam wa siasa jimboni kwetu kuangalia namna ya kupata kijana wa kushika banner,strategy & financing,lazima tumng'oe huyu maana ni part ya matatizo ya nchi yetu (sound like a joke lakini to me this is more than serious na campaign ndio tumeanza)
 
Hata huyo unayemuita MWENYEKITI hana tena nguvu ndani ya Chama anachokiongoza.Upole,Uzembe na Uoga wake unamfanya pia nae anakuwa mtu wa kuburuzwa ndani ya Chama....Huyu Bwana mdogo wanamfukuza kabisa Chamani kwa sababu wanayoiita "Utovu wa Nidhamu"..Ama kweli Lowassa ana nguvu za ajabu....

Jamani Tanzania kuna serikali za CCM mbili; moja na yenye nguvu ni ile inayoongozwa na Lowassa, RA na mafisadi wenzao na nyingine ni ile inayoongozwa na JK ... JK yupo kama "sanamu" tu; hana "madaraka"!
 
Mnafanya makosa kumtenganisha JK na akina LOWASA.
 
Jamani Tanzania kuna serikali za CCM mbili; moja na yenye nguvu ni ile inayoongozwa na Lowassa, RA na mafisadi wenzao na nyingine ni ile inayoongozwa na JK ... JK yupo kama "sanamu" tu; hana "madaraka"!

Hahahaha nimecheka sana ....unameseji kali sana mzee... raisi wetu kazi kuuza meno na tabasamu...
 
One thing is surely true. CCM chama kubwa, yaani uchaguzi wa UVCCM kila mtu yupo alerted. Pilipili msio ila yawawashia nini? Si mna Chadema yenu leave them alone chama chao acheni wafanye watakavyo na nyie mna vyenu. Get life guys..

Wote wanaotumia hii mitandao walikuwa ccm,labda kwa mtu ambaye amezaliwa baada ya mfumo wa vyama vingi.inaele wewe umezaliwa baada ya vyama vingi kuanzishwa,hivyo sio kosa lako
 
According to the dataz ya baadhi ya yaliyojiri ni kwamba:-

1. Wahusika wote wakuu wa EPA, toka wiki iliyopita wamekuwa wakiwatafuta wenyeviti wa mikoa wa UV-CCM, kwa kumtumia mwenyekiti mmoja kutakla kuwapa hela kwa ajili ya msimamo wa kumfukuza uanachama Nape, huko Dodoma.

2. Huyu mwenyekiti akapata tatizo kwamba wengi wao walikataa kwamba wako upande wa Nape, ndipo Tom Mwang'onda akatumwa kuwahi Dodoma in advance akiwa na hela nyingi sana kwa ajili ya hii shughuli ambapo dau lilikuwa kuanzia shillingi millioni moja mpaka mbili, kulingana na nafasi ya umuhimu wa mjumbe kwenye baraza la Uv-CCM.

3. Kikao kilipoanza, aliyekifungua ni Nchimbi, akatumia nusu saa kumtukana sana Nape, akafuatia Ngombale yeye akatukana wote kuanzia Nape mpaka wabunge wanao kikosoa chama, ndipo alipofuatia Makamba ambaye aliongea kwa karibu masaa mawili akiwatukana sana Nape na wabunge kina Mwakyembe, wakati wote huu Kawawa alikuwa amekaa kimyaa, ilipofika zamu yake, Kawawa alizungumzia vijana na kilimo na hasa kilimo cha matrekta, alipomaliza tu akaondoka na hakurudi tena, kwa sababu kilichotakiwa pale ni kuonekana tu kuwa angalau alikuwepo.

4. Baada ya Kawawa tu kuondoka, kukawa na kikao cha kamati ya utekelezaji ambapo Nape, aliitwa na kuulizwa maswali mengi sana kwamba kwa nini amesema uongo kuhusu jengo, akatakiwa aende kwenye public na kusema kuwa anaomba radhi kwa kusema uongo, kitu ambacho Nape alikataa kata kata kuwa hana mpango wa kubadili msimamo.

5. Ndipo usiku kukawa na kikao cha kupitisha majina, ambapo Nape alitoka nje hasa ilipoanza nafasi ya mwenyekiti, alipotoka tu Nchimbi akawaaambia wajumbe kua ana hoja nzito toka kwa kamati ya Utekelezaji, nayo ni kufukuzwa uanachama kwa Nape, wajumbe wwengi wakaja juu kuwa haiwezekani, kuona hivi Makamba akasimama na kuchukua fomu ya Nape huku akiionyesha kwa wajumbe, aliwaambia kuwa Nape ni mtoto wake na ndiye pekee anayemjua mle ndani kuliko wote,

- Na kwamba ameshaongea naye sana kuhusu hili tatizo, kwa hiyo wasijifanye wanajua sana, hiyo ya kufukuzwa kwake Nape yeye ameshaimepitisha tayari na hata huko mbele yeye ndiye atakayekwenda kutoa maelezo zaidi sio wao, wajumbe wakabaki na mshangao na Mkamba akiendelea kuwatisha kuwa hapa tatizo sio Nape tu ila wale wote wanaomuunga mkono nao wote lazima watajadiliwa kwa kina na kufukuzwa pia, hapo ndipo wajumbe wakapitisha hiyo hatua ya kumfukuza Nape, baada ya kikao kufungwa wajumbe wakiwa wanajitayarisha kuondoka ndipo mjumbe mmoja akasimama na kusema kwa sauti kubwa sana kuwa kwa nini Nape asianyang'anywe kadi pia?

- Mwenyekiti Nchimbi kwa tabasamu kubwa sana akasema kwa nguvu sana kuwa hiyo nayo imepitishwa.

6. Hiki kikao ukweli ni kwamba kimeruka kanuni nyingi sana za umoja huo na CCM kwa ujumla, kwa sababu according to wanaojua vizuri mambo ya CCM, ni kwamba CCM kama chama inatawaliwa na kanuni moja tu ya maadili na usalama wake, kanuni yake ya Ibara ya kati ya 87 na 89 ni kwamba,

-Kiongozi yoyote wa taifa kama Nape, akifanya makosa against CCM, anatakiwa apewe;-

1. Onyo. 2. Onyo kali. 3. Karipio. 4. Kufukuzwa.

Meaning kwamba kufukuzwa ni baada ya hatua zote tatu za mwanzo kushindwa, sasa Uv-CCM wanatakiwa kuwakilisha adhabu yao kwa CC, swali la kwanza litakuwa je ni vipi kanuni zilifuatwa?

Wakuu haya ni baadhi tu yaliyojiri na hii sagga na tutaendelea kuyamwaga zaidi, kama tunavyoyapata lakini support imekua kubwa sana kwa kijana Nape, hii habari imewashitua wakulu wengi sana na hasa uwt, kwa maoni yangu jina la Nape halitarudi kwenye wagombea kwa sababu ya umri, lakini hili la adhabu hapana hilo halitasimama, na kuna wananchi wengi wanachama wa CCM, wanaomtaka arudishe kadi ili wajiunge naye hiyo siku ya kurudisha.

Ahsante wakuu, na tutaendeela kuhabarishana yanayojiri.

...aiseeh kwa style hii ya Hitler watatumaliza wakishika nchi,huyu Nchimbi ndio awe raisi si tumekwisha...hawa inabidi tupambane nao kabla hawajashika the ultimate power!
 
tena ndoto ya Mhe. Nchimbi ni kuwa Rais wa URT siku moja, na katika historia yake hajawahi kushindwa jambo alilodhamiria (najua wapo watakaonipinga).
 
Hivi ni kweli Nchimbi akisha amua hakuna wa kumpinga katika maamuzi yake??Naona hapa wengine wanadai eti Jk anamungwaya sana huyu Nchimbi.........ngoja tusubili maamuzi yake tuone.Huu ni mtihani mwingine katika chama cha Jk.
 
...i dont know much about nchimbi zaidi ya kumsikia huku JF na kashfa zake za hapa na pale kuanzia vyeti na umafia kwa wenzake ndani ya CCM,tunahitaji kumjua lakini seems journalist wetu hawafanyi kazi yao,tafadhari wanaomjua waweke kila kitu na wasiache chochote kibaya na kizuri,seems ana power sana ndani ya CCM na wote tunajua kwa hali ya hewa ya sasa mwenye nguvu CCM ndio huyo anaweza kuwa mkuu wa nchi...we need to know this guy!
 
Hivi ni kweli Nchimbi akisha amua hakuna wa kumpinga katika maamuzi yake??Naona hapa wengine wanadai eti Jk anamungwaya sana huyu Nchimbi.........ngoja tusubili maamuzi yake tuone.Huu ni mtihani mwingine katika chama cha Jk.

Labda anaogopa ndumba maana nasikia jamaa kwa kupulizia na kutundika makoti hewani ni balaaa....lakini mbona Muungwana JK hajampa u full minister ?
 
tena ndoto ya Mhe. Nchimbi ni kuwa Rais wa URT siku moja, na katika historia yake hajawahi kushindwa jambo alilodhamiria (najua wapo watakaonipinga).

Mkuu,

Huyo ni haki yake kuota,ili mradi asiote kazini.Tutakula nae sahani moja,anafikiri kutangulia ni kufika.Asubiri muda ufike ndio aone wanamapinduzi wanavyofanya kazi.Atapotea katika medani za siasa muda si murefu,ukiona kiburi chake kimefika huko basi ujue mwisho wake kisiasa umefika
 
Labda anaogopa ndumba maana nasikia jamaa kwa kupulizia na kutundika makoti hewani ni balaaa....lakini mbona Muungwana JK hajampa u full minister ?

Daa...!!!! ina maana hapa jamaa anajivuna kwa kuwa ana ndumba?
 
Just in Halmashauri Kuu ya UVCCM inayokutana Dodoma imemvua Uanachama wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Nape NNauye kwa sababu nyingine ikiwamo utovu wa nidhamu...wengine wenye habari zaidi watufahamishe zaidi.
...Wanafiki hao..wanataka watu waendelee kulala usingizi wa pono hata kama nyumba inaungua wasiseme??? Nape kawapa ukweli mafisadi wamemaindi wakaamua kumtosa...

These Makamba and Kingunge.....Mh!!!!
 
Back
Top Bottom