Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Kama CCM itapitisha huu uamuzi wa kijinga wa kumuadhibu 'whistle blower' Nape na hasa kwa kumkatalia kugombea uongozi ili angalau akashindiwe huko mbele ya safari, au mbaya zaidi kumfuta uanachama, hii itadhihirisha rasmi kuwa ndani ya UVCCM na CCM kwa ujumla Demokrasia imekufa na kilichobaki ni kwa kila kiongozi kuchukua chake mapema.

Ni vema wakabandika bango pale makao makuu ya UVCCM kuwa UVCCM sasa ni Chuo Kikuu cha Kufundisha Vichanga Jinsi ya Kujiunga na Mtandao wa Mafisadi.

UVCCM chini ya Kihiyo Nchimbi, Kamanda rushwa Yusufu Makamba, Director wa DSM car parking project Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mzee wa nyama changa Rashid Kawawa na Jemedari wao mkuu JK, ni Kitengo Maalum cha Kuwafunza Vichanga Uongozi Mbovu Unaoshurutisha Kila Mmoja Kushiriki Katika Ufisadi au la kufutwa Uanachama.

Wako wapi akina Warioba, Butiku, SAS, Mr. & Mrs. Malecelas n.k. katika kukemea huu uonevu wa wazi unaohatarisha Demokrasia kiduchu iliyopo?
 
Mwandishi mahiri Padri Karugendo alibashiri kuanguka kwa Nape Mnauye mwezi August 08. Alisema katika semina ya kutathini uchaguzi wa 2005 Karugendo alifichua ufisadi wa CCM yeye akiwa kama mmoja wa waagalizi wa uchaguzi huo. Nape alipinga na kumtukana Karugendo kwa kuichafua CCM. Wakati wa mapunziko Karugenmdo alimwita Nape na kuongea naye kwa kina bila mafanikio.Kwenye biblia inasimulia jinsi Saulo aliyekuwa muovu aliokoka akiwa njiani kwenda Damascus na kuwa Paulo ambaye alikuwa muhubiri mahili wa injili. Lakini Mt. Paulo aliteswa sana na mafarisayo. Tumfananishe Nape na Saulo amabaye alibadilika kuwa Paulo hivyo ategemee shuluba ndani ya CCM. Na ndivyo imekuwa! Je, Nape atarudi nyuma? Saulo hakurudi nyuma.


Duhh...wokovu wa Bwana umeingia JF.
 
Mzee Kawawa ana mwanae kwenye hicho kinyanganyiro cha Uenyekiti wa UVCCM...hivyo namuona Mzee Kingunge anampa Mzee mwenzie "Support" Makamba ni Katibu Mkuu hana jinsi iwapo Mwenyekiti wa UVCCM akishirikiana na Mzee Kawawa na Ngombale wametaka iwe hivyo.

Mtihani hapo ni wa JK, hawa wazee wamemuweka mtegoni.
 
Mkuu asante sana, siasa za bongo wazijua nimekuvulia kofia...endelea kutuhabarisha...maisha ya dogo Nape yako hatarini kila anayegombana na Nchimbi mauti humkumba....natamani kutuma rambi rambi kwa familia ya Nape

Dahhh machozi hapa yananitoka nakumbuka bifu la NCHIMBI na dada yangu AMINA CHIFUPA hivi hivi kiutani utani mtu akaondoka na hatunaye tena......jamani mshaulini kijana awe makini hawa watu wabaya wana mkono mrefu sana.
 
Nchimbi ana dhamira zake na kwa bahati mbaya sana anadhani amefanikiwa katika dhamira alizojiwekea, na hii yote ni kwa sababu yote anayoyaona yakitokea hayaangilii kwa umakini anaamini ana waungaji mkono wengi katika dhamira zake na kutoutambua ukweli huu inatokana na kuwaangalia watu waliomzunguka kwa macho ya kilevi. Anadhi waungaji mkono wake ni wengi.maskini hafahamu kuwa idadi aipatayo imezindishwa na macho yake ya kilevi kwa "pombe alizokunywa".

Sasa hivi ni Naibu waziri wa ulinzi anaongea maneno ambayo hajui athari zake kwa nafasi na dhamana aliyonayo, anakwenda mbali zaidi na kudiriki kutukana watu wanaoweza kutambua na kulalamikia dhurma katika jamii kuwa ni wendawazimu.

Anaongea kama mtawala mkuu katika nchi itayoendeshwa na utawala wa Ki-dictator.

Nchimbi napenda kutumia fursa hii kukukumbusha kuwa ni afadhali kama ungepewa wizara ya mambo ya ndani ya nchi...ungeweza kuwatumia Polisi utakavyo na wao wangekulinda kwa sababu Polisi ni jeshi la serikali na wapo kwa ajili ya viongozi wa serikali na masuala ya raia kwao ni secondary issue, lakini huko ulipo ni jeshi la wananchi na wapo kwa ajili ya wananchi na si watu wenye ndoto za aina yako hapo ndiyo mwisho wako unajiandika...jaribu kuangali mfumo na utendaji wa taasisi hiyo unayoiongoza utajua nina maanisha nini.

Aliyekuweka hapo ni kwasababu hakupendi usijidanganye na kufikiri kuwa wewe ni the most favored desciple"Peter/Petro", ninafahamu kuwa mwisho wetu sote ni mmoja lakini wako hautakuwa na kificho wala utata na kwa wengi itakuwa ni uhuru kamili, hakuna mtu anaetaka kuandika historia kupitia wewe lah..! isipokuwa historia imeamua kujidhihirisha na yenyewe ndiyo itachagua wa kuiweka...mikono yako imejaa hatia, na kwa jinsi ulivyolewa na kupofuka hutapata nafasi ya kutubu dhambi zako, wachache wakuzungukao, ni walewale wamtumikiao kafiri wapate chao.

Haiwezekani mtu ukosoe chama kwa maslahi ya chama uitwe mwendawazimu, hayao ni matusi ya dhahiri, inaonekana hata elimu uliyoipata(INGAWA NA WASIWASI NA VYETI VYAKO )ilikuharibu akili badala ya kukujenga, ndiyo tunao wasomi wa aina yako wengi tu...hata wewe ni shahidi.

Kwa hiyo kwa kufuata kanuni mpo tayari kumuweka bata na mbuzi watuongoze kuliko watu wenye sifa na mawazo ya kimapinduzi sivyo? Ninyi si ni Chama Cha MAPINDUZI..? Vp muogope mawazo ya kimapinduzi na kuchagua kuishi katika kivuli cha HOFU na UFISADI,

Haya na tuendelee kusubiri na muda si mwingi maoni haya yangu yatakapotafutwa na kusomwa tena na tena na kuchukuliwa na kuhusishwa na tukio kwa namna moja au nyingine
 

A what cost?

At a minimum cost compared to the burden we use to bear kila siku ambayo CCM na club ya mafisadi wanapokua madarakani.

Maanke gharama tunazobeba za kujilea sisi na wadogo zetu pale mama zetu wanapofariki kwa kukosa madawa hospitalini ni kubwa zaidi,

Gharama tunazobeba katika kutafuta elimu hasa elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo yenye ubaguzi mithili ya makaburu ni kubwa sana,

Gharama tunazobeba kutokana na tulizobebeshwa na IPTL,RICHMOND,DEEP GREEN,NET GROUP,EPA nk ni kubwa sana.


Nachelea kusema ni bora tujiaandae kukabilana na gharama zitokanazo na anguko la Zimwi CCM,and finally najua kila kitu kitanyooka kwani pia Mungu yupo upande wa watanzania wabebao gharama hizo.Mungu Ibariki Tanzania,Nchi ya Ahadi.Inawezekana
 
... hivi ni kweli amavuliwa uanachama au atachukuliwa hatua zingine tu za kinidhamu kwa ajili kutoa siri za chama kwenye vikao ambavyo sio rasmi.

Kama ni kweli basi wamemuonea kijana wa watu. Kwa nini wasimuenzi hata baba yake

Vipi UVCCM wakikuonyesha Katiba yao inayosema kwamba kiumbe chochote kitakacholalamika nje ya kikao kinaweza kikatimuliwa? Bado utasema wamemuonea? Utasema wampeteshe ili wamuenzi baba yake?

Tuseme Chama kibovu sio Nape kaonewa.

Ndio maana Nchimbi ataendelea kuoneka electioneering genius!
 
Nchimbi ana dhamira zake na kwa bahati mbaya sana anadhani amefanikiwa katika dhamira alizojiwekea, na hii yote ni kwa sababu yote anayoyaona yakitokea hayaangilii kwa umakini anaamini ana waungaji mkono wengi katika dhamira zake na kutoutambua ukweli huu inatokana na kuwaangalia watu waliomzunguka kwa macho ya kilevi. Anadhi waungaji mkono wake ni wengi.maskini hafahamu kuwa idadi aipatayo imezindishwa na macho yake ya kilevi kwa "pombe alizokunywa".

Sasa hivi ni Naibu waziri wa ulinzi anaongea maneno ambayo hajui athari zake kwa nafasi na dhamana aliyonayo, anakwenda mbali zaidi na kudiriki kutukana watu wanaoweza kutambua na kulalamikia dhurma katika jamii kuwa ni wendawazimu.

Anaongea kama mtawala mkuu katika nchi itayoendeshwa na utawala wa Ki-dictator.

Nchimbi napenda kutumia fursa hii kukukumbusha kuwa ni afadhali kama ungepewa wizara ya mambo ya ndani ya nchi...ungeweza kuwatumia Polisi utakavyo na wao wangekulinda kwa sababu Polisi ni jeshi la serikali na wapo kwa ajili ya viongozi wa serikali na masuala ya raia kwao ni secondary issue, lakini huko ulipo ni jeshi la wananchi na wapo kwa ajili ya wananchi na si watu wenye ndoto za aina yako hapo ndiyo mwisho wako unajiandika...jaribu kuangali mfumo na utendaji wa taasisi hiyo unayoiongoza utajua nina maanisha nini.

Aliyekuweka hapo ni kwasababu hakupendi usijidanganye na kufikiri kuwa wewe ni the most favored desciple"Peter/Petro", ninafahamu kuwa mwisho wetu sote ni mmoja lakini wako hautakuwa na kificho wala utata na kwa wengi itakuwa ni uhuru kamili, hakuna mtu anaetaka kuandika historia kupitia wewe lah..! isipokuwa historia imeamua kujidhihirisha na yenyewe ndiyo itachagua wa kuiweka...mikono yako imejaa hatia, na kwa jinsi ulivyolewa na kupofuka hutapata nafasi ya kutubu dhambi zako, wachache wakuzungukao, ni walewale wamtumikiao kafiri wapate chao.

Haiwezekani mtu ukosoe chama kwa maslahi ya chama uitwe mwendawazimu, hayao ni matusi ya dhahiri, inaonekana hata elimu uliyoipata(INGAWA NA WASIWASI NA VYETI VYAKO )ilikuharibu akili badala ya kukujenga, ndiyo tunao wasomi wa aina yako wengi tu...hata wewe ni shahidi.

Kwa hiyo kwa kufuata kanuni mpo tayari kumuweka bata na mbuzi watuongoze kuliko watu wenye sifa na mawazo ya kimapinduzi sivyo? Ninyi si ni Chama Cha MAPINDUZI..? Vp muogope mawazo ya kimapinduzi na kuchagua kuishi katika kivuli cha HOFU na UFISADI,

Haya na tuendelee kusubiri na muda si mwingi maoni haya yangu yatakapotafutwa na kusomwa tena na tena na kuchukuliwa na kuhusishwa na tukio kwa namna moja au nyingine
Mkuu,walinena,Tukanena na bado tutanena lakini unabii unakaribia.Kwa hali inayoendelea,ipo siku mioyo ya Watanzania iliyojaa visasi na uchungu wataamua kuonyesha kwa vitendo.

Hakuna damu imwagikayo ambayo haijahesabiwa kwani hata nywele za kichani ambazo hazi-sense nazo zimehesabiwa.

Matusi hayo si kwa Nape pekee,yameelekezwa hata kwa wanapinduzi wote wanaosimamia mageuzi.Ni matusi mazito kwa wapambe wa demokrasia ndani ya Taifa hili.Ipo siku Nchimbi atawajibu watanzania kwa kuwaomba msamaha.Najua hatasubiria hata tume kama ile Ya Mandela kule South Africa ya maridhiano.Kiburi cha leo,kina kikomo Kesho
 
Katika hali ya mazoea ya michakato ya CCM, mara nyingi wale ambao huonekana mwiba huishia kwenye vifo vya utata, mfano katika michakato iliyopita ya UVCCM Taifa kuna wapiganaji ambao vifo vyao vilitokea kiutata, mfano:Marehemu ,IPIANA MALECELA,AMINA CHIFUPA, na aliyekoswakoswa JENNY MIANJI, kwa mazoea hayo watu wengi hasa ndani ya chama cha CCM Na UVCCM,walihofia mpiganaji mwenzao Bwana NAPE MNAUYE, angekuwa kwenye mtililiko huohuo ,
NA MARA NYINGI VIFO HIVYO MH.NCHIMBI ALIKUWA AKIHUSISHWA ZAIDI.
PIA Kutokana na kauli yake kama ilivyonukuliwa hapo chini aliyoitoa kwenye Baraza kuu la UVCCM taifa kuwa .

“Hatuwezi kuwa na taasisi kubwa kama hii halafu tukakosa WENDAWAZIMU hilo haliwezekani na ninasema leo hadharani kuwa WENDAWAZIMU wote ni lazima tutawashughurikia na ili iwe ni fundisho kwa wengine hilo linawezekana na liko ndani ya uwezo wetu”

kauli hii ni ya kudhalilisha na inaonyesha kabla ya maamuzi kulikuwa na jazba ambayo ukiangalia itamrudia mh.Nchimbi na kuleta mgawanyiko, kwa tafsiri ya MWENDAWAZIMU MH. NCHIMBI AOMBE RADHI KWA WAPIGA KURA waliomchagua NAPE, PIA NAPE AWE MAKINI KWANI KUNAWEZA KUKAWA NA MIPANGO MIKUBWA ZAIDI YA KUMMALIZA NA HATA KUTOA UHAI WAKE...POLE SHUJAA NAPE ,POLE WAPIGANAJI WAKE ...!!!!!
 
CCM sio wote mafisadi bali wameelemewa na mafisadi.

Kila wakati mimi nasema kwamba kama wapinzani wakichukua ikulu basi yale matunda yaliyooza kwenye CCM yote yataondolewa ili yasiambukize wenzao
Na hapo ndio CCM itabakia na watu wazuri.

Mpaka sasa sina msimamo wowote wa chama lakini bila CCM kuondolewa hatutafika popote.

SISI WATAALAMU WA MAMBO TUNASEMA CCM NI KAMA VILE MBWA KICHAA ALIYEMNG'ATA MBWA ASIYE NA KICHAA NAYE AKAPATA KICHAA, SASA DAWA SIYO KUWATIBU, ILA DAWA NI KUWATWANGA RISASI WOTE.demett
 
Nao hawakusita kuchukua maamuzi magumu na mazito

Inaonekana Nape alikua anatoboa siri za chama-teh teh teh.

yawezekana nape alikua anawafitinisha viongozi wa chama teh teh teh.

Ama naye CHIMBI alisimama ktk kikao na kunena.
Hayuko tayari kumwachia uenyikiti NAPE ama yeye avuliwe uanachama ama yeye Nchimbi abwage manyanga teh teh teh teh.
kazi kweli kweli

What is individual/personal interests in national interests. Nafikiri sasa ni wakati wa wananchi kuitaka nchi yetu kwani imetekwa na mafisadi kikatiba kabisa hadi wahisani kugoma kutoa fedha ni dalili taifa la Tanzania halionekani katika ramani ya nchi adilifu kisiasa na kiuchumi.

Hima hima wananchi tuseme yatosha!
 
Nape alikuwa sahihi ila timing ilikuwa mbaya. Angengoja wampitishe kwanza!
Tatizo la viongozi wetu bongo kukosa washauri wa kisiasa.

Nape is doing just fine, ngoma iko kwao sasa wazee wa CCM, naona tunachanganya either kwa makusudi au kwa kutokuelewa kuwa ni kwamba :-

1. Nape, "amesimamishwa" uanachama wa Baraza la UV-CCM the only thing Nchimbi can do for now, lakini ya kufukuzwa au kuvuliwa unachama linafanywa na CC, kwa kushirikiana na NEC.

2. The timing was right, kwa sababu no matter what Nchimbi asingeweza kumpitisha Nape, hata angekua legally bubu, infact bila ya hii njia aliyotumia Nape, asingefika hapa alipo sasa, ambapo CC ndio watakaoamua fate yake, hivi wakuu ni kweli mmesiwakia majina ya wagombea wote huko UV-CCM?

3. Nchimbi yuko kwenye corner ambayo hajawahi kuwepo katika maisha yake ya siasa Nape alikuwa na choices mbili, either kuingia bubu akatwe jina, au kupiga kelele afikie hapo alipo sasa hivi kweli unahitaji kuwa professor ku-figure that out? Nape had to create a crisic ili ku-survive, hapa Nchimbi amekanyaga makaa ya moto yeye mwenyewe bila kujua, kwa sababu no body listens to Makamba ambye yeye mwenyewe anatakiwa kuwa nje na wajumbe wengi wa CC, na I bet oyu siku hiyo ya CC Makamba hataenda kukimbia aibu!

4. So far habari za magazeti yote ni compromise wa Nchimbi, ambaye he would do anything kutuhadaa wananchi, alichofanya so far ni kumsimamisha kwa muda, mpaka CC na NEC watakapotoa uamuzi, NChimbi hawezi kumfukuza Nape unachama wa UV-CCM, wala CCM yenyewe, ninarudia anachoweza ni kumsimamisha kwa muda mpaka uamuzi wa mwisho utolewe na CC, ambayo italisema hili tarehe 9,

Ni haki ya wananchi kuilaumu CCM kwa mambo mengi lakini kwa hili ukweli anyetakiwa kulaumiwa at this stage ni Nchimbi, Mkamba, na Kingunge ambao wote watatu ni compromise ya Lowassa na Mkapa,

I mean kupigana na mafisadi sio kazi rahisi wakuu, we have enough history in our hands toka majuzi Pakistan tumeona Mwanamama shujaa Bhutto, akiuliwa na na fisadi ambaye sasa ameachia ngazi mwenyewe na mume wa marehemu kushika ngazi, tumeona Ukraine jinsi fisadi alivyojaribu kutumia sumu kumuua shujaa wao rais wa sasa, tumeona Philipines jinsi fisadi alivyomuuua shujaa Arroyo akidhani ameshinda, kwanza ni kumpa heshima Nape kuwa mpaka leo hajafa wala kudhurika, anachokifanya Nape sasa hivi ni kitendo so bold kwamba sidhani kama kuna kiongozi yoyote ndani ya CCM amewahi kukifanya,

Na belive me kuwa sasa hii pekee ndiyo itakayo kuwa njia ya wanyonge kuingia ndani ya CCM, ni kutumia uhuni kama wao wenyewe mafisadi ili kula nao sahani moja, Nape angefanya makosa makubwa sana kama msimamo wake kuhusu ufisadi, usingetoka nje yaani wakuu wa CCM wangeweza kuizima ile hoja isitoke nje, lakini hoja imetoka na Rais wa jamhuri akaamuru uchunguzi ufanywe na matokeo yake wadhamini wa UV-CCM wote wamemkana Nchimbi na Lowassa, tena mbele ya CC ulitegema Nchimbi aende Dodoma kufanya nini kumpitisha Nape, baada ya yeye na Lowassa kuwekwa kiti moto ndani ya CC?

Kwani rais alipokuwa anamuamuru Nchimbi kwenda kukutana Dodoma haraka ili arudishe majibu CC kama mujibu wa katiba unavyotaka hivi ni kweli Rais alitegemea kuwa Nchimbi atampitisha Nape? Kwa wale tunataka mabadiliko katika mwenendo wa uongozi wa taifa letu, this is best thing to happen toka siku ile Lowassa, alipojiuzulu sasa ni wakati wa kusubiri na kuona je CC itakubaliana na Nchimbi na Makamba? Kingunge haingii CC Kawawa wanamburuza tu tena huyu ni Kingunge, je Kinana, Salmin Amour, Malecela, Sitta, Anna Makinda (ambaye anarudi haraka kwa ajili tu ya kuhudhuria tarehe 9), watakubali haya?

I mean binafsi ninampa hongera nzito sana kijana Nape, ni wa-Tanzania wangapi wanaweza kusimama kidete kama alivyofanya? Wangekuwepo tungefikaje hapa as a nation? Hapa ni pressure kwa kila mjumbe wa CC na NEC, je watamuunga mkono Nchimbi na Makamba?

Ahsante wakuu, na kwa kweli bado tunafutailia kwa karibu yaliyojiri, in some few tutakuwa na more details za kutoka ndani ya mkutano wa jana na kutoka kwa wakulu mbali mbali!
 
mkuu,walinena,tukanena na bado tutanena lakini unabii unakaribia.kwa hali inayoendelea,ipo siku mioyo ya watanzania iliyojaa visasi na uchungu wataamua kuonyesha kwa vitendo.hakuna damu imwagikayo ambayo haijahesabiwa kwani hata nywele za kichani ambazo hazi-sense nazo zimehesabiwa.

Matusi hayo si kwa nape pekee,yameelekezwa hata kwa wanapinduzi wote wanaosimamia mageuzi.ni matusi mazito kwa wapambe wa demokrasia ndani ya taifa hili.ipo siku nchimbi atawajibu watanzania kwa kuwaomba msamaha.najua hatasubiria hata tume kama ile ya mandela kule south africa ya maridhiano.kiburi cha leo,kina kikomo kesho

jamani someni historia ya china,inayomhusu waziri mkuu aliyepita kabla ya huyu aliyeko sasa.[wu jiabao]yeye alipopata madaraka tu aliwashikisha adabu mafisadi wa china,maana ktk historia inaonyesha aliwaua mafisadi wakuu 87 na ndipo nchi ikaweza kusonga mbele kwa kasi ya ajabu.na hii kauli ya mbwa kichaa kamng'ata mbwa aliitoa yeye.sasa sisi wa tz masikini wa mungu sijui nani atakayeweza kuyafanya haya maana baada ya kifo cha sokoine mawaziri wanaokuja wote wana tamaa na hivyo wanataka kufanya biashara.it will be hard
 
Mkisikia kulikologa ndo hili uongozi wa MAKAMBA,NCHIMBI na BABU KINGU ni wa kukalili.....wamechemka sana eti wao wasiulizwe na vijana kwa vile ni wazee.....duh hii kali JK kama unajua hawa watu ndio wanao kuvulugia mipango yako na kukuzunguka.
Hapo sasa Nape ndo mnampa umaarufu wa hali ya juu sasa atauzika jimbo lolote akitaka kugombea ubunge huyu kijana.


Mkuu Fidel,

Very strong analysis na ni very realistic of the situation.
 
Mzee Kawawa ana mwanae kwenye hicho kinyanganyiro cha Uenyekiti wa UVCCM...hivyo namuona Mzee Kingunge anampa Mzee mwenzie "Support" Makamba ni Katibu Mkuu hana jinsi iwapo Mwenyekiti wa UVCCM akishirikiana na Mzee Kawawa na Ngombale wametaka iwe hivyo.

Mtihani hapo ni wa JK, hawa wazee wamemuweka mtegoni.

Mkuu,

Hizi comflict of interest sijui dawa yake ni nini.kuna watu wameshajiamulia kwamba ni wao na wano na wajukuu zao tu wenye hati miliki ya mamlaka katika Taifa hili.

Leo hii nashindwa kuelewa ni kwa nini tukubali kuwa watumwa wa hizi familia chache zinazotuamulia mambo yetu? Hta suala la kumchagua nani,wanataka wao tu waamue? Jamani hebu tuamke na tuanze kupambana nao.Unajua tulipokua tunamtoa mkoloni mweupe hatukumaanisha kwamba sasa tunakubali kuwa chini ya utawala dhalimu wa mtu mweusi.Sisi tulikataa unyanyasaji na ukandamizaji wa ain yoyote,unyonyaji tuliupinga,babu zetu wakauwawa na kufa vifo viabya na vya aibu.Nashangaa leo baada ya miaka 47 ya kuushinda ule uhasidi bado tulilea uhasidi mbaya kuliko ule na tena kwa kasi ya ajbu.Leo hii wewe ni mwanachama au mjumbe wa UVCCM unampa back up mwanamapinduzi mwenzako kwa sababu unatamani mabadiliko,Wewe na Na kiongozi wako mnatukanwa 'MWENDAWAZIMU'. Ni tusi kubwa kama lile mkoloni alilokua akimtukana Nyerere .Akiwaambia wazee wa Tanu msijishughulishe na huyo kijana 'mwendawazimu'.

Sasa Wanachama na wajumbe wa UVCCM watamchukulia hatua Nchimbi? Hajataja majina ya watu au mtu,lakini kusema kuna wendawazimu hapo ni suala lingine? Na vipi huu udikteta wa mtu kupayuka na yeye kupitisha jambo bila kulijadili ndiyo utaratibu huko UVCCM? Kweli CCM hakuna Demokrasia.Nchimbi alijuaje kama aliyeropoka ni mwendawazimu na yeye akalipitisha hilo wazo?
 
Hizi comflict of interest sijui dawa yake ni nini.kuna watu wameshajiamulia kwamba ni wao na wano na wajukuu zao tu wenye hati miliki ya mamlaka katika Taifa hili.

Vijana vyenyewe vijinga. Kwa nini vikubali vibabu, Mwiru, Kawawa, na Makamba, vije kuingilia uchaguzi wao?
 
Mkuu FMES

Hongera sana kwa kunyangamua hili gogoro ndani ya CCM kwa sasa...somo linaeleweka vizuri sana. Nape Nnauye alitumia mbinu ambayo hata yeye mwenyewe sithani kama alitegemea ingempa jukwaa la juu kiasi hiki. Kwa kiasi fulani naanza kuona pengine mpango wote wa kugombea Uenyekiti ulikuwa na lengo la kuchokonoa haya mambo, kwa sababu sijui/sioni Nape alikuwa anategemea nini kuhusu kigezo cha umri. Sasa inaonekana kana kwamba alitengeneza mtego wa kumshika Nchimbi pabaya.

Nashindwa kujua Nec-UVCCM kwa nini badala ya kujadili majina ya wagombea huko Dodoma kama agenda za kikao zilivyowataka wao wakaenda kubadili agenda na kuifanya iwe ya kumjadili Nape Nnauye kiundani hadi kumvua uanachama wa UVCCM. Wangekuwa na kheri naye wangetoa jina lake lisipekwe CC kugombea Uenyekiti UVCCM lakini wao wakaenda mbali sana na agenda za kikao.

Sina imani na Mwenyekiti JK kama ana-balls za kusimama imara ndani ya CC na kusema CCM ni muhimu iwe inakosolewa na hivyo kuveto uamuzi/ mapendekezo ya Nec-UVCCM.

Huu moto wa mabadiliko unawaka unavyotakiwa ndani ya CCM; wakina Kingunge, Kawawa, Lowassa na Makamba wao bado wanajiona wako mbali ya miali mikali ya moto huu. Siku zao zinahesabika, naona itafika siku watakisusia Chama Chao.
 
Vijana vyenyewe vijinga. Kwa nini vikubali vibabu, Mwiru, Kawawa, na Makamba, vije kuingilia uchaguzi wao?



Mkuu,hatan mimi hilo limenishangaza sana.Jina ni Vijana lakini utakuta vijana hao hao,wameruhusu kukaa katikati ya vijeba wanaowaburuza.VIjana wenzangu,amkeniii! ukombozi ndiyo sasa.Youth for Change!


People's power forever.
 
Back
Top Bottom