Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

This thing is incredible, maneno ya hii kitu inakuwa very interesting nimebahatika kuongea na wanaohusika, sana na this whole thing:-

1.According to deal ni kwamba Rais alipomteua Pinda kuwa PM kabla ya kuvunja baraza la mawaziri, kulikuwa na kikao cha CCM na joint UV-CCM, ambacho kilikuwa na lengo la kutoa azimio la kumpongeza Rais kwa chaguo lake, la Waziri Mkuu mpya.

2. Nchimbi akagoma akisema kuwa Uv-CCM au yeye under any capacity, hawezi kuwa involved na huo ujinga kwa sababu yeye hamtambui Pinda, kwa hiyo he is out na hilo azimio. Ujumbe ukafikishwa kwa rais kama ulivyo, na according to more dataz ni kwamba kwa makusudi mazima wale wote aliowapandihsa chati Nchimbi, kupitia UV-CCM, kina David, Masha, na Kamalla wakapewa uwaziri kamili.

3. Nchimbi akatanagaza rasmi ndani ya vikao vya CCM kuwa yeye sasa ni mfuasi wa Lowassa, kwa 100% na kwamba no matter what Pinda is no body to him, na kwamba majuzi Nchimbi alipoamua kumtumia muandishi wake kuandika uongo kuhusu habari za jengo na Nape huko CC, ni muungwana mwenyewe aliyempigia simu mwenyekiti wa IPP, akitaka kujua huku akifoka kuwa hiyo habari nani aliyeipeleka huko Nipashe, mwandishi alipobanwa ndio akatema sumu yote na kumtaja Nchimbi. Ni baada ya mkwara mzito sana aliopewa mwenyekiti wa IPP, ndio maana Nipashe wakaomba msahama na hata kumtaja waziri anyewapa habari za ndani za CC.

4. Ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewaagiza UV-CCM kukutana jana, kuamua kuhusu majina na sio anything else, sasa according to the dataz ni kwamba Nchimbi na Makamba wanasubiriwa sana na CC, kwa sababu Kingunge haingii tena CC, nimedokezewa na wajumbe kama wanne wa CC kuwa huko kutawaka moto siku ya tarehe 9, maana no way hii kitu ya Nchimbi inaweza kupita huko kwa sababu wanajua kuwa ikifika NEC itakuwa aibu kubwa sana kwa CC wanaweza kuzomewa kama Butiama na muafaka, the dataz ni kwamba Nape ameambiwa atulie na kusuubiri tarehe 9.

My Take:

Kwa kweli sasa hili taifa tumefika mbali sana, yaani the lowest mark kwa any president aliyewahi kuliongoza taifa hili, I mean Nchimbi anwezaje kuwa na utovu wa adabu kiasi hiki na bado akapewa uwaziri mdogo wa Ulinzi kama adhabu? Haya ni mambo ya aibu sana sio tu kwa mwenyekiti wa CCM na viongozi wote wa CCM, bali ni kwa wananchi wote wa taifa hili. I want kuamini kuwa CC itasimama kidete na kumfundisha adabu Nchimbi, otherwise tutakuwa tumekubali kuwa under mafisadi, tunaisubiri kwa hamu tarehe 9, kusikia maamuzi ya mwisho.

Ahsante Wakuu na Tunaendelea Kufuatilia Kwa Makini na Ukaribu Sana hizi Stunning Events. Kesho Tutakuwa Na Zaidi Ya Yalioyjiri na Pia Tutazungumza na Nape Mwenyewe.
 
Gustanza,
Mwalimu alikuwa akitumia nguvu ya hoja na si ubabe ubabe unaoendelea hivi sasa ndani ya CCM. Go on!
 
Really? Are you kidding me? Yaani hata Mwalimu mwenyewe asingeweza ku-veto maamuzi ya akina Lowassa, Makamba, Kingunge na Nchimbi? Are you serious!?!

[1]:Marshall, sasa naona unazeeka vibaya! Kumbuka G-55? Ni nani kama sio Mwalimu aliyekuwa mstaari wa mbele kumpiga Malecela?

[2]: Kumbuka uchaguzi wa kupendekeza mgombe wa CCM 1995? Bila Mwalimu, nani angemstopisha Lowassa?

[3]: Je, umesahau jinsi Mwalimu alivyomshutumu Prez. Mwinyi pale kilimanjaro Hotel kwa ujingaujinga wake?

[4]: The same Mwalimu ambaye aliyewahi kutamka kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Kawawa kwamba: "Kawawa alikuwa kibaka huyu...!"

[5]: I mean, I can go on and on and on...

Please, give me a break [here]!

1. Kwanza naomba kuliweka one thing wazi, mimi sio mzee kama wewe mkuu kwa hiyo la kuzeeeka vibaya ni lako maana si unajua kuwa umekaribia ku-retire na kuwa Senior Citizen, mkuu nina miaka 30 na zaidi kabla ya ku-retire kwa hiyo la kuzeeka vibaya ni lako na ni out of the ishu!

2. You can go on and on, lakini huwezi kukwepa the real deal ya Mwalimu ya kushindwa mara mbili kumuweka Salim kuwa Rais kwa kugomewa na wajumbe tena wa Zanzibar tu, tena mara mbili kuanzai 1985, na 1995. Mwalimu alikuwa a true politician aliyejua how to pick up a political fight hakuwa mbabe mbabe tu wa ujinga ujinga, alikuwa mbabe wa hoja!

Next time fikiri kabla ya kuandika mkuu huwa hatukurupuki hata siku moja!
 
Gustanza,
Mwalimu alikuwa akitumia nguvu ya hoja na si ubabe ubabe unaoendelea hivi sasa ndani ya CCM. Go on!

Naelewa mkuu Jasusi. Nachokataa hapa ni hili la Field Marshall kuwa ni Mkapa peke yake ambaye angeweza ku-veto hayo maamuzi , kwamba, hata Mwalimu Mwenyewe asingweza. Which is so untrue!
[1]: Kumbuka G-55? Ni nani kama sio Mwalimu aliyekuwa mstaari wa mbele kuwapiga akina Malecela, Kassaka na Mateo Qares?

[2]: Kumbuka uchaguzi wa kupendekeza mgombe wa CCM 1995? Bila Mwalimu, nani angemstopisha Lowassa?

[3]: Je, umesahau jinsi Mwalimu alivyomshutumu Prez. Mwinyi pale kilimanjaro Hotel kwa ujingaujinga wake?

[4]: The same Mwalimu ambaye aliyewahi kutamka kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Kawawa kwamba: "Kawawa alikuwa kibaka huyu...!"

[5]: I mean, I can go on and on and on...!
 
Nape kafanya kosa moja kubwa kimkakati, ambalo nadhani ndilo liliyomcost nafasi zake kwenye Chama chake. Alianza vibaya sana kwa kujaribu kumnyang'anya fisadi upanga huku akimwabia waziwazi kuwa ukiniachia upanga huu nitautumia kukukata shingo, wakati fisadi huyo bado kashika mpini wa ule upanga. Angetumia akili kidogo tu kwa kuanza na SWAT analysis nzuri kulingana na hali ya hewa kwenye chama chake, halafu akabiliane na threats dhidi yake kwa busara sana. Kifupi, angejifunza kwa marehemu Mwanawasa.

Sasa huko CCM yeye ni "Persona non grata." Jambo zuri kwake ni kuwa kafukuzwa katika mazingira yaliyong'arisha jina lake zaidi ya na huenda akajipatia wafuasi wengi zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma. Ana options mbili

(A) Aachane na siasa za CCM atafute chama cha upinzani chenye sera zinazokaribiana na imani yake, halagu aendeleze mapambano. Inawezekana njia hii ikamtisha kidogo, ila ukweli ni kuwa kama ana data nzuri za ndani ya CCM halafu akipata chama kizuri cha upinzani akaamua kuwasha moto mkali sana, CCM watamfuata tena, hasa ukizingatia background yake.

(b) Atuulie tu na kuwa mpole ndani ya CCM asipige kelele zozote, huenda akahurumiwa na wazee wa CCM hasa baada ya kumfudishwa na wazee:

Wakizungumza katika mkutano wa Baraza hilo lililofanyika mjini Dodoma jana, wazee hao Katibu wa CCM, Yusufu Makamba, Kaimu Kamanda wa Vijana, Kingunge Ngombale Mwiru na Mshauri wa Vijana Mzee Rashid Kawawa waliwaonya wagombea wote na wapambe wao kuacha kukikosoa chama hicho badala yake wawe wapole

Wazee hawa nao naona kama busara na akizli zimewapungua kwa kiasi kikubwa sana. Miaka ya themanini wakati mzee huyu Kawawa akiwa Katibu mkuu ndiye aliyekuwa anahubiri mshikamano na kukosoana. Nakumbuka katika mojawapo ya hotuba zake alisema wazi kuwa tujenge utamaduni wa kukosoa makosa badala ya kunungunika na vile vile tukubali kukosolewa huku tukiendeleza mshikamano. Kwa mantiki hiyo mimi sioni kosa la Nape,

Sijui kama baba yake angekuwa hai kuona haya anayotendewa mwanawe nadhani angepasuka kwa hasira. Alikuwa mhamsishaji sana na alizowea kusema kuwa ni afadhali ageuke ng'ombe kusudi wanamapinduzi wapate maziwa kuliko kufanya makosa yanayodidimiza mapinduzi. Katika kuhamsisha watu alikuwa anatumia kinanda kukamilisha hoja zake.
 
1. Kwanza naomba kuliweka one thing wazi, mimi sio mzee kama wewe mkuu kwa hiyo la kuzeeeka vibaya ni lako maana si unajua kuwa umekaribia ku-retire na kuwa Senior Citizen, mkuu nina miaka 30 na zaidi kabla ya ku-retire kwa hiyo la kuzeeka vibaya ni lako na ni out of the ishu!

C,mon Marshall! Umekaa kiwanja miaka yote hiyo unashindwa kuelewa kuwa "kuzeeka vibaya" is just a saying, some sort of euphemism? I'm shocked that you took it literally mkuu! I know una personal vendatta na Mwalimu, but take it easy.

2. You can go on and on, lakini huwezi kukwepa the real deal ya Mwalimu ya kushindwa mara mbili kumuweka Salim kuwa Rais kwa kugomewa na wajumbe tena wa Zanzibar tu, tena mara mbili kuanzai 1985, na 1995. Mwalimu alikuwa a true politician aliyejua how to pick up a political fight hakuwa mbabe mbabe tu wa ujinga ujinga, alikuwa mabeb wa hoja!

This is just another example of your "intellectual dishonesty" Marshall. Again, I know that una personal vendatta na Mwalimu, but take it easy. Sio lazima umu-diminish Mwalimu kiasi hicho in order to prove your point.

Next time fikiri kabla ya kuandika mkuu huwa hatukurupuki hata siku moja!

I think wewe ndo unapaswa kufikiria kabla ya kuandika. Wewe ndo umekurupuka hapa.
 
This thing is incredible, maneno ya hii kitu inakuwa very interesting nimebahatika kuongea na wanaohusika, sana na this whole thing:-

1.According to deal ni kwamba Rais alipomteua Pinda kuwa PM kabla ya kuvunja baraza la mawaziri, kulikuwa na kikao cha CCM na joint UV-CCM, ambacho kilikuwa na lengo la kutoa azimio la kumpongeza Rais kwa chaguo lake, la Waziri Mkuu mpya.

2. Nchimbi akagoma akisema kuwa Uv-CCM au yeye under any capacity, hawezi kuwa involved na huo ujinga kwa sababu yeye hamtambui Pinda, kwa hiyo he is out na hilo azimio. Ujumbe ukafikishwa kwa rais kama ulivyo, na according to more dataz ni kwamba kwa makusudi mazima wale wote aliowapandihsa chati Nchimbi, kupitia UV-CCM, kina David, Masha, na Kamalla wakapewa uwaziri kamili.

3. Nchimbi akatanagaza rasmi ndani ya vikao vya CCM kuwa yeye sasa ni mfuasi wa Lowassa, kwa 100% na kwamba no matter what Pinda is no body to him, na kwamba majuzi Nchimbi alipoamua kumtumia muandishi wake kuandika uongo kuhusu habari za jengo na Nape huko CC, ni muungwana mwenyewe aliyempigia simu mwenyekiti wa IPP, akitaka kujua huku akifoka kuwa hiyo habari nani aliyeipeleka huko Nipashe, mwandishi alipobanwa ndio akatema sumu yote na kumtaja Nchimbi.

4. Ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewaagiza UV-CCM kukutana jana, kuamua kuhusu majina na sio anything else, sasa according to the dataz ni kwamba Nchimbi na Makamba wanasubiriwa sana na CC, kwa sababu Kingunge haingii tena CC, nimedokezewa na wajumbe kama wanne wa CC kuwa huko kutawaka moto siku ya tarehe 9, maana no way hii kitu ya Nchimbi inaweza kupita huko kwa sababu wanajua kuwa ikifika NEC itakuwa aibu kubwa sana kwa CC wanaweza kuzomewa kama Butiama na muafaka, the dataz ni kwamba Nape ameambiwa atulie na kusuubiri tarehe 9.

My Take:

Kwa kweli sasa hili taifa tumefika mbali sana, yaani the lowest mark kwa any president aliyewahi kuliongoza taifa hili, I mean Nchimbi anwezaje kuwa na utovu wa adabu kiasi hiki na bado akapewa uwaziri mdogo wa Ulinzi kama adhabu? Haya ni mambo ya aibu sana sio tu kwa mwenyekiti wa CCM na viongozi wote wa CCM, bali ni kwa wananchi wote wa taifa hili. I want kuamini kuwa CC itasimama kidete na kumfundisha adabu Nchimbi, otherwise tutakuwa tumekubali kuwa under mafisadi, tunaisubiri kwa hamu tarehe 9, kusikia maamuzi ya mwisho.

Ahsante Wakuu na Tunaendelea Kufuatilia Kwa Makini na Ukaribu Sana hizi Stunning Events. Kesho Tutakuwa Na Zaidi Ya Yalioyjiri na Pia Tutazungumza na Nape Mwenyewe.

CCM kwa theatrics hawawezekaniki.
 
Nape kafanya kosa moja kubwa kimkakati, ambalo nadhani ndilo liliyomcost nafasi zake kwenye Chama chake. Alianza vibaya sana kwa kujaribu kumnyang'anya fisadi upanga huku akimwabia waziwazi kuwa ukiniachia upanga huu nitautumia kukukata shingo, wakati fisadi huyo bado kashika mpini wa ule upanga.

Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele sana, Nape had no other choice bali kufanya alivyofanya kwa sababu no way Nchimbi angeweza kumpa nafasi ya uongozi at anytime as long as ana nafasi ya uongozi ndani ya Uv-CCM,

This was the only way ya hata jina lake kuguswa na kuzungumziwa, otherwise lingeishia kutupwa kapuni kimya kimya, hapa kinachoendela ni vita kubwa ndani ya CCM kati ya makundi mawili, ambayo vilifikia kilele siku ile Lowassa alipojiuzulu u-Waziri Mkuu pale bungeni,

Unayoyasema ni kweli tupu, lakini sio kwenye siasa za Nchimbi na UV-CCM, na mafisadi, ukweli ni kwamba hii ndio njia pekee Nape aliyokuwa nayo ili angalau ku-raise his profile, ama sivyo angekwua nje ya ulingo siku nyingi sana, please mpe kijana heshima yake kwa sababu ametumia njia smart sana ya kumfikisha Nchimbi ukutani maana never katika historia ya Nchimbi amewahi kukimbizwa mchaka mchaka namna hii kwa sababu hii ngoma bado inaendelea na hasa kwenye jengo kutakuwa na kivumbi kikubwa sana huko CC.

Huwezi ku-deal na wahuni bila kushuka kwenye level yao ya uhuni.
 
Naelewa mkuu Jasusi. Nachokataa hapa ni hili la Field Marshall kuwa ni Mkapa peke yake ambaye angeweza ku-veto hayo maamuzi , kwamba, hata Mwalimu Mwenyewe asingweza. Which is so untrue!

Mwalimu alikuwa akipinga au kupigia debe jambo alikuwa anajenga hoja nzito zilizokuwa na mantiki sana kiasi kuwa watu wote across the spectrum wanamwelewa na kukubaliana naye. Ni kweli wakati mwingine hoja za Mwalimu zilikuwa na dosari, kwa mfano madai ya kuwa Mkapa ni clean, lakini kushindana naye kwa hoja ilikuwa ni kitendo kilichokuwa kinahitaji nishati kubwa sana kiasi kuwa hakuna hata mmoja aliyekuwa na ubavu wa kupingana naye.

Mkapa hakuwa na capacity ya Nyerere ndiyo maana alishindwa kupitisha watu wake kwenye kinyang'anyiro cha uraisi pamoja na kwamba alikuwa ameapa kuwa asingeachia kiti hicho kwa Kikwete.
 
Mkapa hakuwa na capacity ya Nyerere ndiyo maana alishindwa kupitisha watu wake kwenye kinyang'anyiro cha uraisi pamoja na kwamba alikuwa ameapa kuwa asingeachia kiti hicho kwa Kikwete.

Thanks kichuguu kwa kunisaidia hapa...
 
Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele sana, Nape had no other choice bali kufanya alivyofanya kwa sababu no way Nchimbi angeweza kumpa nafasi ya uongozi at anytime as long as ana nafasi ya uongozi ndani ya Uv-CCM,

This was the only way ya hata jina lake kuguswa na kuzungumziwa, otherwise lingeishia kutupwa kapuni kimya kimya, hapa kinachoendela ni vita kubwa ndani ya CCM kati ya makundi mawili, ambayo vilifikia kilele siku ile Lowassa alipojiuzulu u-Waziri Mkuu pale bungeni,

Unayoyasema ni kweli tupu, lakini sio kwenye siasa za Nchimbi na UV-CCM, na mafisadi, ukweli ni kwamba hii ndio njia pekee Nape aliyokuwa nayo ili angalau ku-raise his profile, ama sivyo angekwua nje ya ulingo siku nyingi sana, please mpe kijana heshima yake kwa sababu ametumia njia smart sana ya kumfikisha Nchimbi ukutani maana never katika historia ya Nchimbi amewahi kukimbizwa mchaka mchaka namna hii kwa sababu hii ngoma bado inaendelea na hasa kwenye jengo kutakuwa na kivumbi kikubwa sana huko CC.

Huwezi ku-deal na wahuni bila kushuka kwenye level yao ya uhuni.

Asante sana kwa kunimasha kwa hilo. Nitaangalia kwa makini mbio hizi zitaishia wapi, kwani wahenga walisema kuvuja kwa pakacha la uongozi itakuwa ni nafuu kwetu wachukuzi.
 
Mkapa hakuwa na capacity ya Nyerere ndiyo maana alishindwa kupitisha watu wake kwenye kinyang'anyiro cha uraisi pamoja na kwamba alikuwa ameapa kuwa asingeachia kiti hicho kwa Kikwete.

Urais wa Mkapa siku zote ulitegemea wakuu wa dola, hasa wa uwt kwa sababu according to the dataz hata uamuziw a kuwapiga kule Pemba hakuwa yeye aliyeamua, yeye alifahamishwa later tu huku wakuu wa dola wakiwa wameshahamisha askari wengi sana kutoka Bara kwenda Visiwani, tena walipelekwa wakiwa na nguo za kiraia kama watalii tu,

Infact hata wakati wa uchaguzi wa visiwani, wananchi wengi walipelekwa kutoka bara bila yeye kufahamishwa in advance, mauaji ya mwembechai yote hakuwa na any idea mpaka baadaye alipofahamishwa,

Uamuzi wa muungwana kuwa rais uliamuliwa na mstaafu wa uwt, sio yeye Mkapa, kwa sababu wakati wote huo mstaafu alikuwa kundi moja na Lowassa na Rostam, lakini kwa siri sana mpaka siku moja, Mkulu kaisi alipom-confront mkapa Chamwino kuhusu tetesi za muungwana kuwa rais, huku akifoka kwa hasira sana akayasema yote wazi kuwa ni mstaafu wa uwt ndiye aliyeamua sio yeye!

Ingawa ni kweli kama unavyosema kua angependa kumpitisha Kigoda, lakini the deal ilikuwa in the play kwa siku nyingi sana, yeye mkapa aliambiwa wiki nne kabla ya kwenda Chamwino kwenye mchakato wa CCM, huku mstaafu akiuutumia uchaguzi wa Kenya kama kisingizio baada ya kuwapo kule kipindi chote cha uchaguzi akiufuatilia kwa makini.
 
Mkapa hakuwa na capacity ya Nyerere ndiyo maana alishindwa kupitisha watu wake kwenye kinyang'anyiro cha uraisi pamoja na kwamba alikuwa ameapa kuwa asingeachia kiti hicho kwa Kikwete.

1. Kikao kimoja cha CC under mkapa, siku moja kiliamua kuwa Idd Simba na Nchimbi, wafukuzwe uanachama CCM, kesho yake Mkapa kwa kutumia ubabe wake kama mwenyekiti akaandika memo kwa viongozi wote wa CCM kuwa wamepitishwa kugombea nafasi zao za Uv-CCM na Wazazi.

2. Kamati ya bunge ya ulinzi na usalama, ilimua kuwa Ulimwengu na Bandora, wavuliwe uraia moja kwa moja na wasipewe tena, kama kawaida ya ubabe wake mkapa akakataa kabisa na kuamuru wapewe.

Kwa hiyo kama Mwalimu na yeye alikwama kwenye urais, lakini sio huko chini hata siku moja.
 
Weakness ya Mkapa ni kuwa alikuwa hawezi kujenga hoja zenye nguvu kama alivyokuwa akifanya mwalimu. Kote huko aliko-override, alitumia mabavu tu bila ushawishi wowote. Katika maswala ya namna hii, Nyerere alikuwa akitumia ushawishi kwa nguvu ya hoja, na inaposhindikana ndipo anakata tamaa.
na kuachia ngazi. Mkapa alikuwa atumia hoja ya mabavu.
 
Urais wa Mkapa siku zote ulitegemea wakuu wa dola, hasa wa uwt kwa sababu according to the dataz hata uamuziw a kuwapiga kule Pemba hakuwa yeye aliyeamua, yeye alifahamishwa later tu huku wakuu wa dola wakiwa wameshahamisha askari wengi sana kutoka Bara kwenda Visiwani, tena walipelekwa wakiwa na nguo za kiraia kama watalii tu,

Infact hata wakati wa uchaguzi wa visiwani, wananchi wengi walipelekwa kutoka bara bila yeye kufahamishwa in advance, mauaji ya mwembechai yote hakuwa na any idea mpaka baadaye alipofahamishwa,

Uamuzi wa muungwana kuwa rais uliamuliwa na mstaafu wa uwt, sio yeye Mkapa, kwa sababu wakati wote huo mstaafu alikuwa kundi moja na Lowassa na Rostam, lakini kwa siri sana mpaka siku moja, Mkulu kaisi alipom-confront mkapa Chamwino kuhusu tetesi za muungwana kuwa rais, huku akifoka kwa hasira sana akayasema yote wazi kuwa ni mstaafu wa uwt ndiye aliyeamua sio yeye!

Ingawa ni kweli kama unavyosema kua angependa kumpitisha Kigoda, lakini the deal ilikuwa in the play kwa siku nyingi sana, yeye mkapa aliambiwa wiki nne kabla ya kwenda Chamwino kwenye mchakato wa CCM, huku mstaafu akiuutumia uchaguzi wa Kenya kama kisingizio baada ya kuwapo kule kipindi chote cha uchaguzi akiufuatilia kwa makini.

Mstaafu wa uwt ndio nani hapa? kumradhi umeniacha kidogo!
Data zako zinonekana makini ktk mtililiko mzima huu ila huu msamiati umeninyima raha ya hadithi hii.If you dont mind ,who is mstaafu?
 
Nchimbi: Hakuna fitina kupitisha majina UVCCM

Martha Mtangoo, Dodoma
HabariLeo
Monday,September 08, 2008

  • Asisitiza Baraza Kuu si la majungu
  • Makamba akemea kuisema CCM nje ya taratibu

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Emmanuel Nchimbi amesema hakuna majungu wala fitina zitakazotumika wakati wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi za uongozi katika umoja huo, kwa kuwa uchaguzi unazingatia misingi, sheria na Katiba ya CCM.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja huo mjini hapa jana, Nchimbi alisisitiza kuwa baraza hilo maalumu la UVCCM ambalo leo litatoa maoni yake kuhusu majina ya wagombea nafasi za uongozi ndani ya umoja huo, litaelekeza nguvu zake katika kusimamia kanuni za uchaguzi za umoja huo pamoja na kanuni za umoja wa vijana kutoa maoni yake ya majina ya wagombea.

Nchimbi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alieleza kuwa hakuna majungu wala fitina zitakazohusiana na namna ya kupitisha majina ya wagombea, kwani uchaguzi huo unazingatia misingi ya kisheria na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kuwa mkutano huo wa Baraza Kuu si wa fitina wala majungu kama baadhi ya watu wanavyofikiria, bali ni mkutano wenye maamuzi muhimu yanayozingatia kanuni na taratibu za umoja huo na CCM.

Aliwaomba wajumbe wa baraza hilo kuwa makini katika kupitia majina hayo ya wagombea, hasa kwa kuzingatia sifa za wagombea na kwa kuzingatia mustakabali wa jumuiya hiyo kwa miaka ijayo. Naye Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, Rashidi Kawawa alisisitiza umuhimu wa vijana kuendelea kukitumikia Chama Cha Mapinduzi kuboresha ustawi wake.

Kawawa alisema uhai na uimara wa CCM unatokana na vijana, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha siasa ya chama inalindwa, ikiwa ni pamoja na kutekeleza maagizo ya chama. Alisema madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa Umoja wa Vijana mwaka 1956, ilikuwa ni kutekeleza mwelekeo wa siasa za Chama cha TANU wakati huo na uimarishaji wa chama, hivyo misingi ya uanzishaji wa umoja huo ni vema ikaendelea.

Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alikemea tabia iliyoanza kujitokeza ya baadhi ya wanachama wa chama hicho na jumuiya zake ya kutoheshimu taratibu za chama na kukisema chama nje ya taratibu hizo, hasa kwa malengo binafsi. Alikiita kitendo hicho ni cha hatari kwa uhai wa chama, jumuiya na mtu binafsi kwani kinabomoa mshikamano na umoja uliopo ndani ya CCM.

Makamba aliwataka vijana wa CCM kuwa wavumilivu na kutokuwa na tamaa ya madaraka na kueleza kuwa hata viongozi waliopo, walianzia chini na baadaye wakapata madaraka ya juu kutokana na uvumilivu wao. Uchaguzi wa UVCCM hasa ule wa nafasi ya uenyekiti inayoshikiliwa na Nchimbi, umekuwa gumzo katika siku za karibuni huku yakitolewa madai ya baadhi ya wagombea kufanyiwa mizengwe.

Jina la kada wa umoja huo, Nape Nnauye ndilo limekuwa gumzo baada ya kudai katika mkutano wake wa kutangaza azma ya kuwania nafasi hiyo, kwamba kuna ukiukwaji wa taratibu katika uwekezaji wa Jengo la Kitegauchumi la UVCCM lililopo Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam.

Vijana 25 walijitokeza kuwania nafasi hiyo ya uenyekiti, lakini taarifa zinaeleza kuwa watano kati yao ndiyo ambao wamevuka katika vikao vya ngazi za chini na sasa wanaingizwa katika chekeche la Baraza Kuu na kisha Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya uteuzi wa mwisho katika vikao vyao vinavyoanza kesho mjini hapa.

Majina yanayodaiwa kupitishwa ni ya Zainab Kawawa, Hussein Bashe, Beno Malisa, Said Mtanda na Suleiman Haji. Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, walijitokeza wagombea tisa.
 
Nchimbi: Hakuna fitina kupitisha majina UVCCM

Martha Mtangoo, Dodoma
HabariLeo
Monday,September 08, 2008

  • Asisitiza Baraza Kuu si la majungu
  • Makamba akemea kuisema CCM nje ya taratibu

Ninaelekea kukubaliana na FMES kuwa Nchimbi alikuwa cornered; lakini ngoja tuone mwisho wa sakata lote.
 
Wakuu si mnakumbuka Nchimbi aliapa kwanza endapo nape atapitishwa basi yeye atajikata uume ili awe mwanamke! hiki ni kiapo kikubwa sana hasa kwa mbabe kama Nchimbi.
 
Nchimbi ametimiza ahadi yake. Kwa faida ya nani hasa lakini?
 
Hii inaonyesha kabisa MAFISADI wana nguvu kuliko kawaida EL na Nchimbi wanakenua meno kazi yao imefanyika..................hawa wazee wamemshambulia kijana kwa sababu lukuki,.
 
Back
Top Bottom