Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

Quote:-

"BODI ya Shirika la Ndege nchini (ATCL), imependekeza Mwenyekiti wake, Balozi Mustafa Nyang’anyi, awajibike kwa kuboronga safari ya Mahujaji ya mwaka huu."


With all due respect kwa mahujaji, ninauliza why only ishu hii tu? Maana kama ni kuboronga viongozi wetu si wanaboronga kila siku tena kwenye kila sekta, mbona hii ishu tu ndiyo inapewa umuhimu zaidi? Kwa nini hii tabia ya kushauri kuondolewa kwa viongozi wabovu isifanyike kwenye kila ishu?
 
Unajua kitu kinachoshangaza nadhani kuna kautamaduni ka "danganya toto". Mtu anasema anajiuzulu watu wanashangilia halafu kesho yake mnagundua kumbe hajajiuzulu. Mifano hai:

- Machunde - kajiuzulu kisha hakukubaliwa kujiuzulu
- Dr. Rashid - kajiuzulu kisha kaondoa kujiuzulu kwake
- Gav. Balali - kajiuzulu lakini hajajiuzulu kwani hajakubaliwa
- Mustafa Nyang'anyi - atajiuzulu halafu aombwe aendelee?
 
Sasa ndio nimeipata vizuri hii kadhia. Kumbe mwenyekiti wa bodi anasema mahujaji waliomba usafiri kwake, wakati menejimenti ya shirika inasema mweyekiti aliomba biashara kwa mahujaji. Kwa kuwa hawa mahujaji walikuwa na pesa zao na mashirika yenye uwezo wa kuwasafirisha yako mengi, hakukuwa na sababu wao "wakaombe" usafiri wakati pesa yao wanayo, hawahitaji msaada bali "wananunua" huduma, kwa hiyo the most plausible explanation ni kwamba huyu mwenyekiti aliitafuta hiyo "dili" kwa kuwaomba hao waislamu watumie shirika lake.

Sasa ona mwenyekiti wa bodi alivyoishughulikia hii ishu. "Anamkwepa" mkurugemzi mkuu, anakwenda kwa Mkurugenzi wa biashara na kumtaarifu juu ya biashara hiyo. Sasa ndio tuseme keshajipa pia ukurugenzi mkuu on top of uenyekiti wa bodi? Ni "ulevi" wa madaraka ama ni kumdharau mkurugenzi mkuu? Hapa kuna maelewano kweli?

Hatimaye Mkurugenzi Mkuu anapopata taarifa hiyo, anaandika barua kuiarifu Hajj Trust kwamba ATCL haina uwezo wa kufanya biashara hiyo. Mwenyekiti "anaiteka" barua hiyo ikiwa bado kwa Katibu Muhtasi na kuizuia isiwafikie walengwa, na mkurugenzi mkuu hataarifiwi juu ya hatua hiyo. Huu ni utawala gani wa mvurugano mtupu? Hivi kweli mahali kama hapo unaweza kufanya kazi kweli? Unatoa uamuzi, mtu anateka mawasiliano na kuyaficha, halafu anaendelea na mipango yake "behind the scenes"! Something is very very fishy here! Mwenyekiti wa bodi ameteka madaraka ya mkurugenzi mkuu, na kuanza kuendesha shirika! Hii ni fujo!

Kwa mujibu wa taarifa hii, huyu mwenyekiti ndie aliyekuwa analivuruga shirika na anastahili kutimuliwa na kushitakiwa! Mkurugenzi mkuu naye alikuwa na wakati mgumu sana kuendesha shirika huku kukiwa na mwenyekiti aliyeteka madaraka ya ukurugenzi mkuu, na hivyo kuwa na maamuzi antagonistic ambayo kwa makusudi kabisa alikuwa anamficha mkurugenzi mkuu asiyaone! Nashangaa mwenyekiti wa bodi anatoa maagizo ya kiutendaji kwa watumishi na kum-bypass mkurugenzi mkuu, kwa nini alikuwa anamtenga?

Huyu mkurugenzi mkuu kosa lake sijui ni nidhamu ya woga au ni nini. Baada ya kuona mwenyekiti anamvuruga katika utawala, kwa nini hakutoa taarifa mapema hili tatizo lao la kiutawala likashughulikiwa? Au pengine alitoa taarifa hizo "zikatekwa" kama ile barua yake ya kukataa biashara ya mahujaji? Namwonea huruma kwa mazingira aliyokuwa anafanyia kazi, lakini alipaswa kuwa imara kama Dr Rashid wa TANESCO, ambaye "alimtolea uvivu" mwenyekiti wake wa bodi. Kwa kuficha uozo huu na kuuvumilia, nae sasa anaonekana mshiriki wa uozo kama mwenzake. Nampa pole sana.
 
Hivi inaruhusiwa kutishia hivi? Hivi kweli hii ni hukumu ambayo imeainishwa na dini yeyote? Ni hukumu gani wanayoweza kuitoa nje ya mahakama?

Huyo aliyesema ni muilamu na dini ya kiislamu inaruhusu hivyo, kwa mujibu wa koran behading is acceptable, kwa hiyo alikuwa anaongea kwa misingi ya kidini, kwa msingi wa sheria za kidini ambazo Tanzania bado hazijaanza kutekelezwa.
 
Huyo aliyesema ni muilamu na dini ya kiislamu inaruhusu hivyo, kwa mujibu wa koran behading is acceptable, kwa hiyo alikuwa anaongea kwa misingi ya kidini, kwa msingi wa sheria za kidini ambazo Tanzania bado hazijaanza kutekelezwa.

Asante Mkuu kwa kunielimisha. Kwa hiyo huyu Bwana akirudi anaweza akakaa chini na wenzake na kupitisha hukumu juu ya muislamu mwenzao akatwe kichwa? Kama sivyo, nadhani serikali ilibidi kulikaripia tendo na vitisho kama hivi. Hili suala likiruhusiwa kugeuzwa la kidini na sio la kiutendaji litatufikisha pabaya. Kuna watu wanaweza kutaka kuingia peponi kwa nyofoa kichwa cha mtu. Si tendo la kufanyia mzaha. Bongolander ananistua anaposema kuwa sheria hizi hazijaanza kutekelezwa! Kwani ziko kwenye pipeline?
 
Fundi Mchundo! situpo kwenye mchakato wa kuanzisha mahakama ya kadhi, kwa kuwa alitamka waislamu wamuunge mkono basi wamhukumu huko kwa taratibu za kiislam, kama koran ilivyoandikwa.

Natizama hili mattaka taka inaonekana dubwana lipolipo tu, halina strategy zozote za kazi ndo maana mzee akaamua kumtumia capt Muze, mambo yaliharibika baada ya capt.muze kusafiri, je alisafiri kwenda wapi? kufanya nini? nani aliyemtuma? isijekuwa ilikuwa mbinu ya Mattaka kumkwamisha Mzee Nyang'anyi.

Hivi kweli angekuwa binti Fatma Karume, dr.idrisa, dr.kimei ndo ma-MD wa ATCL undondocha huu ungetokea?

Sasa tujiulize ATCL imekuwa commisioned 1st october 2007 kwa mtaji wa tshs 13bil (en.wikipedia.org), mahujaji waliokwama wako 1077 kila mmoja kalipa us$2400 na shirika limeongeza us$580, naona ATCL wameshapoteza tshs4bil tayari! ukiongeza deni la SAA la tshs 4.5bil, naona hili shirika limeshafirisika tayari! halafu walienda kuuliza bei ya airbus 320.
 
Kwa siku 12 Mahujaji wa Tanzania na baadhi ya wengine kutoka nchi jirani, walikwama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, baada ya taratibu za kuwasafirisha hadi Saudia kukwama. Hatimaye, walisafiri lakini baada ya Serikali kuingilia kati. Sasa jitihada zinafanyika waweze kurejea bila matatizo makubwa. Baada ya sakata hiyo, Serikali iliagiza ipewe taarifa ya hali ya mambo. Raia Mwema imefanikiwa kupata nakala ya taarifa hiyo ya Bodi ya ATCL na inaichapisha kwa faida ya wasomaji.

1.0 UTANGULIZI

Kuanzia Desemba 10 , 2007 hadi Desemba 14, 2007 Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lilikuwa katika msukosuko mkubwa. Hiyo ilitokana na matatizo ya kukwama kwa Mahujaji kwenda Hijja Saudi Arabia. Tatizo hilo lilianza kama tukio la kawaida la kiutendaji, lakini taratibu lilianza kuchukua sura mpya kiasi cha kuihusisha Serikali wakiwamo viongozi wa juu kabisa wa nchi.

Tatizo hilo kwa kiasi kikubwa limeleta usumbufu usio kifani kwa Mahujaji ikiwamo aibu na fedheha kwa shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Taifa kwa ujumla, Serikali na viongozi wake wakuu.

Kutokana na hayo, Mheshimiwa Andrew Chenge (Mb), Waziri wa Miundombinu, aliiagiza Bodi kwa kupitia barua yake Kumb. Na. MC 62/2270/01 ya Desemba 17, 2007, kwamba iundwe kamati ya Bodi ya ATCL kufanya uchunguzi juu ya suala la kukwama kwa Mahujaji, na kutoa taarifa yake siku ya Ijumaa, 21 Desemba, 2007.

1.1 UAANDAAJI WA TAARIFA

Kamati ya Bodi katika maandalizi ya taarifa yake ilizingatia yafuatayo:-

* Maelezo ya mdomo ya wahusika wakuu wakiwamo wafuatao:-

- Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL
- Mkurugenzi Mkuu, ATCL na
- Manager Flight Operations

maelezo yaliyotolewa katika kikao cha dharura cha 14 cha Bodi ya Wakurugenzi cha Desemba 17, 2007

* Maelezo ya maandishi ya wahusika muhimu katika suala hili yaliwahusu wafuatao:-

o Mwenyekiti wa Bodi – ATCL (Balozi M. Nyang’anyi)
o Mkurugenzi Mtendaji - ATCL (D. Mattaka)
o Manager, Flight Operations – (M. Manji)
o Kaimu Mkurugenzi wa Operations (Capt. S. Muze)
o Afisa Masoko - (J. Kagirwa)
o Katibu Muhtasi – (M. El-Hady)
o Mwanasheria wa Kampuni – (A. Mziray)

* Maoni ya Wajumbe wa Bodi ya ATCL

2.0 MAELEZO YA AWALI (BACK GROUND)

Kufuatana na maelezo ya Menejimenti ya ATCL, mnamo mwezi Julai, 2007, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, aliwaomba viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Kiislamu zinazoshughulika na safari za Mahujaji kulipatia shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) biashara ya kusafirisha Mahujaji kwenda Makka na Madina, Saudi Arabia (Lakini Mwenyekiti anasema ni viongozi wa Mahujaji ndio waliomfuata na kumuomba).

Mnamo Julai 19, 2007 Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL alimwita ofisini kwake Mkurugenzi wa Uendeshaji, Capt. Sadiki Muze, na kumtambulisha kwa viongozi mbalimbali wa Taasisi za Kiislamu, na kumueleza kwamba mwaka huu ATCL itaandaa safari za Mahujaji. Mkurugenzi huyo alitoa taarifa hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa ATCL kuhusu maongezi yake na Mwenyekiti wa Bodi. Baada ya majadiliano marefu na wataalamu wahusika kwenye Shirika ilionekana kuwa shirika halina uwezo (ndege) wa kuandaa safari hizo.

2.1 HATUA ZILIZOFUATIA

Mkurugenzi Mkuu aliandika barua kwa Mwenyekiti wa HAJJ Trust, ya Julai 26, 2007, ikimuelezea kuwa ATCL haina uwezo wa kuandaa safari za Hijja. Hata hivyo barua hiyo haikupelekwa kwa walengwa, kwani wakati Katibu Muhtasi anatafuta ofisi za Hajj Trust ili barua iwasilishwe huko, Mwenyekiti wa Bodi aliagiza kuwa barua hiyo isipelekwe mpaka afanye mawasiliano na Menejimenti. Katibu Muhtasi aliwajulisha Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Uendeshaji (Capt. Muze) kuwa barua haikupelekwa kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Bodi.

Mwenyekiti wa Bodi aliwasiliana na Mkurugenzi wa Uendeshaji na kumhakikishia kwamba ATCL ingeliweza kufanya safari hizo, kwani ndege zingeweza kupatikana, hususan kutoka katika kampuni ya RAK Leasing ya Dubai. Pia Mwenyekiti alimpatia Mkurugenzi wa Uendeshaji jina na namba ya simu za mhusika ili awasiliane naye kuhusu upatikanaji wa ndege.

Captain Muze aliwasiliana na kampuni ya RAK Leasing ambao walimwambia kuwa wanayo ndege aina ya Boeing 747-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 489, ambayo kwa wakati huo ilikuwa katika matengenezo ya Check “C” na kwamba ingekuwa tayari mwezi wa Septemba, 2007. Capt. Muze aliwaomba wamletee “Documents” za ndege hiyo ili aweze kufanya maandalizi ya kupata vibali muhimu, zikiwemo “slots”. Pia aliwasiliana na kampuni ya Al-Wassam ambao ni “Ground Handling Agent” wa Makka na Madina (ambao hapo zamani walikuwa wana “handle flights” za Hijja za Air Tanzania Corporation) ili wafanye matayarisho muhimu, ikiwamo utafutaji wa “slots”.

Hata hivyo, “documents” za ndege zilichelewa kufika na ilibainika kuwa zilikuwa zinaisha muda wake Novemba 30, 2007, na hivyo zisingefaa kutumika kuombea vibali pamoja na “slots”. Kampuni ya RAK Leasing iliahidi kuwa ingepata “documents” zingine na kuahidi kuitafutia ATCL kampuni nyingine za “ku-handle” ATCL. Pamoja na ahadi hizo kampuni hiyo haikufanya hivyo.

Wakati huo huo Capt. Muze alisafiri kikazi kwa muda mrefu na kumuachia shughuli hii Afisa Masoko, Josephat Kagirwa.

Kadiri muda ulivyopita, na safari za Mahujaji kukaribia ilidhihirika kuwa ndege isingepatikana kutoka kampuni ya RAK Leasing. Hii ilithibitika baada ya wafanyakazi wa ATCL, akiwamo mwanasheria wa ATCL Mziray kwenda Dubai, na kurudi mikono mitupu bila mikataba na au “documents” za ndege ya RAK Leasing na hiyo ilikuwa mwishoni mwa mwezi Novemba, 2007, zikiwa zimebakia siku chache mno kabla ya safari za Mahujaji kuanza.

Baada ya hapo Mwenyekiti wa Bodi na Capt. Muze walianza kufanya mipango mipya ya kutafuta ndege nyingine. Walifanikiwa kupata ndege kupitia msaada wa Al-Wassam, wa Jeddah. Ndege hiyo ni aina ya DC 10 inayomilikiwa na Global Aviation ya Afrika Kusini. Hata hivyo, ndege hiyo ilipatikana kupitia kwa wakala mwingine ambaye ni SAMEK Aviation Services wa Jeddah, (Ground Handling Agent).

Katika mikataba ATCL iliyoingia na SAMEK AVIATION ilijumuisha pia kuipatia ATCL “slots” za ndege hiyo. Mkataba huo ilibidi usainiwe Saudi Arabia na Balozi Hamis Msumi kwa niaba ya ATCL, kutokana na ucheleweshaji wa maandalizi na ufupi wa muda. Wakati haya yanakamilika ilikuwa 6/12/07 na tayari Mahujaji kutoka sehemu mbali mbali walikwisha kuwasili ikizingatiwa kuwa ratiba ya awali ya Mahujaji ingelikuwa 4/12/07.

SAMEK Aviation Services, waliahidi kuwa safari za Hijja zingeanza 8/12/07, na ahadi hii ilithibitishwa kwa Balozi wetu nchini Saudi Arabia, kwamba ndege husika ilikuwa inakuja. Kwa bahati mbaya haikufika kama ilivyoahidiwa, pamoja na ATCL kutimiza masharti yote, ikiwamo kulipa malipo ya awali ya Dola za Kimarekani 550,000.

Kufuatia kutowasili ndege hiyo kama ilivyokuwa imetarajiwa, na Mahujaji kuzidi kusongamana uwanja wa ndege wakati wanasubiri ndege ambayo haikuwa na uhakika, ndipo hali ya wasiwasi na mtafaruku kwa Mahujaji ilitanda na kuanza kuongelewa na vyombo mbalimbali vya habari, hadi Serikali kufahamu kuwa kulikuwa na tatizo.

Kuanzia 9/12/07 Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mtendaji, ilibidi wahamie uwanja wa ndege ili kuwafariji Mahujaji na kutafuta ufumbuzi kadri hali ilivyokuwa ikijitokeza. Hata hivyo, ndege haikufika kati ya tarehe 9 na 10/12/07 kama ilivyo ahidiwa na SAMEK Aviation Services kwa visingizio mbalimbali. Baadaye iligundulika kuwa sababu za ucheleweshaji wa ndege hii ni kwamba:-

* Ndege hiyo ilikuwa inaendelea kufanya kazi nyingine za kusafirisha Mahujaji kutoka Baghdad kwenda Saudi Arabia.

* Mawakala waliokodisha ndege hiyo walishindwa kupata “Slots”.

Hatimaye ndege hiyo ilifika nchini 11/12/2007 bila kuwa na “slots” kama ilivyotarajiwa.

3.0 UUZAJI WA TIKETI KWA MAHUJAJI

Mnamo 20/08/07 Capt. Muze kwa niaba ya Menejimenti aliwasiliana na Taasisi ya Waislam, Tanzania, akiwafahamisha upatikanani wa ndege aina ya Boeing 747-200 na nauli ya kiasi cha dola za Marekani 950 ambayo kila abiria angetakiwa kulipa.

Baada ya majadiliano baina ya ATCL na viongozi wa Taasisi ya Waislam Tanzania, mambo yafuatayo yaliendelea kufanyika:-

* Alichaguliwa Afisa Masoko ili ku-“coordinate” uuzaji wa tiketi kwa Mahujaji

* Viongozi wa Mahujaji walimchagua Wakala FAST TRACK kuwa wakala wao wa usafiri, hivyo fedha zote kwa mauzo ya Dar es Salaam zilipitia FAST TRACK.

* Afisa Masoko alipata kibali toka kwa Mkurugenzi wa Masoko, Ajay, kuingiza ratiba ya safari za Mahujaji kwenye mtandao (Reservation System).

* Afisa Masoko alipata kibali kingine kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Eliasaph, cha kuuza tiketi kwa Mahujaji.

* Nauli halisi iliyopokelewa na ATCL ilikuwa ni Dola za kimarekani 870 kwa kila Hujaji na pesa taslimu kwa Mahujaji wote ni Dola za Kimarekani 1,248,013 kiasi ambacho ni baada ya makato yote (commission).

* Kuweka ratiba ya Hajj Charters kwenye mtandao (Reservation System) ni kuwezesha safari hizi kuuzwa mahali popote ndani na nje ya nchi, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Comoro, Malawi na kadhalika.

3.1 MAPUNGUFU YA NAULI
* Baada ya kukosekana kwa ndege toka kampuni ya RAK Leasing, ndege ya DC10 ambayo ilisafirisha Mahujaji imegharimu dola za kimarekani, 1,450 kwa kila Hujaji, wakati nauli iliyotozwa na ATCL ilikuwa ni dola za Kimarekani 870 kwa kila Hujaji. Kwa sababu hiyo, ulitokea upungufu wa dola za Kimarekani 580 kwa kila Hujaji. Baada ya majadiliano kati ya Mwenyekiti wa Bodi na Viongozi wa Mahujaji walikubaliana kwamba Mahujaji walipie dola za Marekani 230 kila mmoja na zilizobaki zitafidiwa na ATCL. Hata hivyo, Mahujaji waliahidi kwamba fedha hizo watazilipa watakaporudi kutoka kwenye Hijja.

* Imedhihirika kwamba upo utata katika mkataba kati ya SAMEK AVIATION SERVICES na ATCL kuhusu gharama za nauli. Upande wa ATCL imeeleweka kuwa gharama za nauli ni za kwenda na kurudi, japo katika mkataba suala hilo halijawekwa wazi. ATCL kwa ushirikiano na ubalozi wetu nchini Saudi Arabia wanawasiliana ili kuhakikisha swala hili linaeleweka vizuri kabla ya safari za kurudi kuanza.

4.0 SERIKALI KUINGILIA KATI

Baada ya ndege kuwasili 11/12/07, Manager Flight Operations, Mark Manji aliwasiliana na mwakilishi wa SAMEK AVIATION SERVICES kuhusu suala la “Slots” na alihakikishiwa kuwa “slots” zipo. Wakati wanatayarisha utaratibu wa ndege kuondoka Mark Manji vile vile aliwasiliana na kapteni wa ndege ambaye alimjulisha kuwa kila kitu kilikuwa tayari.

Mark Manji aliwajulisha viongozi wenzake wa ATCL kuwa ndege ilikuwa tayari na abiria waruhusiwe kupanda kwa ajili ya safari. Kabla ya hapo muwakilishi wa SAMEK AVIATION SERVICES, alidai na kukabidhiwa fedha kiasi cha dola za Marekani 160,000 kama malipo ya ziada ya safari ya kwanza.

Abiria walipopanda kwenye ndege uongozi wa ATCL uligundua kwamba ndege hiyo haikuwa na kibali “slots” cha kutua Saudi Arabia. Suala hili lilipojitokeza ungozi wa ATCL haukuwa na namna nyingine yeyote ila kuwashusha abiria waliokuwa wamepanda kwenye ndege. Itakumbukwa kwamba tukio hili lilitokea baada ya Rais na Waziri Mkuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuwaaga Mahujaji ambao tayari walikwisha hakikishiwa kuwa safari ingekuwapo.

Kadri muda ulivyopita ilidhihirika kuwa SAMEK AVIATION SERVICES walikuwa na mikakati ya ubabaishaji kuhusu upatikanaji wa “slots” na hivyo Serikali iliamua kuingilia kati suala hili. Hatimaye “slots” zilipatikana na ndege ya kwanza iliondoka na kundi la kwanza la Mahujai 11/12/2007.

Bahati mbaya kundi la pili halikuweza kuondoka kwa muda uliopangwa kutokana na ndege kuharibika ilipotokea Madina. Hata hivyo, kundi hilo liliondoka 12/12/2007 saa 11.30 jioni badala ya saa 1.30 asubuhi. Kundi la tatu lilisafiri 14/12/2007 mnamo saa 3.30 asubuhi.

5.0 USHIRIKI WA BODI

Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL ilipanga kuwa na kikao chake cha 16 cha kawaida kuanzia 9/12/07 huko Bagamoyo. Tarehe 10/12/07 asubuhi baadhi ya wajumbe walipokutana iligundulika kwamba Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji hawakuwapo. Wajumbe walifahamishwa kwamba kulikuwa na tatizo kubwa lililohusu kukwama kwa Mahujaji uwanja wa ndege, hivyo Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Menejimenti walikuwa uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere wakishughulikia suala hilo. Wajumbe walifanya kikao cha dharura chini ya uenyekiti wa Balozi (Ami) Mpungwe na kuamua yafuatayo:-

* Kuahirishwa kikao cha kawaida cha 16 kutokana na dharura hiyo na hivyo kurudi Dar es Salaam.

* Kuagiza Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mtendaji waitishe kikao cha dharura, siku iliyofuata yaani 11/12/2007 ili Bodi ipewe maelezo juu ya suala hilo, ambalo wajumbe wa Bodi walikuwa hawana taarifa yeyote; na

* Wajumbe walikubaliana kwa kuwa suala hili walikuwa hawalijui, wasiliongelee popote, hasa kwenye vyombo vya habari.

Kikao hicho cha dharura hakikuweza kuitishwa kutokana na hali halisi ilivyokuwa, hadi ilipofika 17/12/2007.

6.0 ATHARI ZA KIUTENDAJI KWA ATCL

* Kutokana na sakata hili la ATCL na Mahujaji, maneno mengi ya kejeli na kashfa dhidi ya Uongozi wa ATCL yamekuwa yakitolewa na baadhi ya Viongozi wa Mahujaji ambayo yanatia dosari kwa Shirika hili.

* Kuanzia 10/12/2007 vyombo vya habari vimekuwa vikitoa maoni na maneno yasemwayo na Mahujaji. Mifano michache ni pamoja na:-

- Katibu wa kundi la Mahujaji la AL-BIZ Abdallah Mohamed alikaririwa akisema “Safari hii imeandaliwa na kundi la kisanii – kisanii …. Tutadai haki na fidia kwa ATC”

- Kiongozi wa Taasisi ya MUSLIM Hajj Trust Juma Nchia alisema “watu waliotenda kosa kubwa wanapaswa kukatwa kichwa kwa mujibu wa Dini yao ……….. tutajadili hukumu yake baada ya safari hii kushidikana kabisa”.

- Katibu wa Taasisi ya Alh-Bir Abdallah Harith Mohamed alisema kuwa “waliingia mkataba na ATC baada ya Nyang’anyi ambaye ni Muislamu mwenzetu na mtu aliyewahi kuwa Balozi wa Saudia Arabia, ambaye aliwaomba Waislam wasafiri na ndege yao….”

* Aliendelea kusema “sisi tulikuwa tumeachana na Shirika hili kwa miaka 10 … Taasisi zote ziliambiwa kuwa ATC ina ndege ya kukodi Boeing 747-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 480”.

Akalalamika kuwa ATC imewatia hasara kubwa na lazima walipe gharama zote hizi pamoja na fidia ya usumbufu.

- Uzembe huu wa ATC ulitaka kuwasha moto wa hasira ya maandamano kwenye RUN WAY ya ndege ili kuzuia ndege zozote zisiondoke wala kutua uwanjani hapo.

* Yote haya yanaashiria kuwa bado Mahujaji kupitia viongozi wao wanatarajia kufanya mamabo yafuatayo:-

* Kudai fidia na gharama ya usumbufu.

` (ii) Kuishitaki ATCL kwa kukiuka mkataba.

* Kuitaka Serikali kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na kuvuruga safari yao ya Hijja.

* Serikali kuwaomba radhi Hadharani kwa usumbufu wowote ule uliotokea.

* Kuitaka ATCL kupitia Serikali kuwahakikishia kuwa kosa hili halitarudiwa tena wakati wa kuwarejesha nyumbani Mahujaji.

7.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA BODI

Katika kikao cha dharura kilichofanyika 10/12/2007 huko Bagamoyo na baadaye kuhitimishwa kwa pamoja 17/12/2007 katika Ofisi za ATCL Dar es Salaam, Wajumbe wa Bodi walimtaka Mwenyekiti na Menejimenti ya ATC itoe maelezo ya kina kuhusiana na sakata lote hili kuanzia mwanzo lilipojitokeza hadi tarehe ya kikao hicho. Pia Bodi ilitakiwa kutoa majibu ya masuala yaliyojitokeza kama barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu ilivyokuwa imeelekeza Menejimenti na Bodi kufuatilia kwa undani nini kiliathiri mpango mzima wa safari za Hijja.

7.1 MAELEZO YA MWENYEKITI WA BODI

Bodi ilipata maelezo ya kina toka kwa Mwenyekiti wa Bodi Balozi Mustafa Nyang’anyi na baadaye akayaweka kwenye maandishi.

7.2 MAONI YA BODI

Wajumbe pamoja na kukubaliana na Mwenyekiti kukubali kuwajibika kwa kushawishi Menejimenti kuidhinisha kuingia Mkataba wa ukodishaji wa ndege; Wajumbe waliona kuwa ilikuwa ni kosa kwa kuwaingiza watendaji katika mikataba mizito kama hii, bila Bodi kuhusishwa.

Pamoja na nia nzuri ya Mwenyekiti kutaka kufanikisha safari hii, lakini wasiwasi wa kuwatumia mawakala wa ndege za kukodi bila kutumia taratibu zetu za nchi na Sheria za manunuzi n.k. zinatia dosari utendaji wa Bodi katika kusimamia taratibu hizi.

Ni kutokana na hilo Bodi inaona kuwa Mwenyekiti anastahili kuwajibika na kutoa maelezo hayo kwa chombo cha uteuzi wake ili kusisafisha Bodi na Wajumbe wake ambao hawakuhusika kabisa katika sakata zima la ukiukaji wa taratibu zote za maandalizi ya safari za Hijja.

7.3 MAELEZO YA MKURUGENZI MTENDAJI

Pamoja na maelezo ya kina yaliyojitokeza kama ilivyoainishwa kwenye taarifa yake, kama Mtendaji Mkuu wa Shirika na Mshauri Mkuu wa Bodi, angeweza kukataa ushauri wa Mwenyekiti na kuleta suala hili kwenye Bodi kwa maamuzi. Inaonekana hakufanya hilo na badala yake alikubaliana waendelee na utekelezaji wa ushauri huo kinyume cha sheria, kanuni na maelekezo ya Bodi.

o Tatizo hili lilichukua sura mbaya baada ya ATCL kuendelea kuvurugwa na ratiba za ndege hizo za kukodi hata bila Bodi kuwa na taarifa.. Maji yalikuwa yamefika shingoni, hakukuwa na nafasi ya kukwepa mzigo huu.
o Mkurugenzi Mtendaji kwa hili, pamoja na barua ya awali ya kutaka kupinga ATCL isijihusishe katika ukodishaji wa ndege za Mahujaji, hawezi kukataa kuwajibika kwa kuwa alikuwa na kila sababu ya kuwajulisha Wajumbe wa Bodi kuhusu mapatano hayo ambayo kiutaratibu yalitakiwa yapate kibali cha Bodi.

Pamoja na uwezo wake mzuri wa kikazi lakini kwa hili anastahili kukiri kosa kwa tabia kama hii.

8.0 MAJUKUMU YA BODI

Kwa mujibu wa majukumu ya Bodi kama yalivyoainishwa kwenye Waraka wenye Kumb. Na. SHC/B.40/6/21 imedhihirika kuwa Menejimenti imesahau na pengine haikufuatilia maelekezo kwenye waraka huo ambao ulifafanua yafuatayo:-

* Majukumu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi

* Majukumu ya Wakurugenzi wa Bodi

* Majukumu ya Watendaji Wakuu



Imedhihirika kuwa, wajumbe wamesahau na pengine hawakuyafuatilia maelekezo yaliyomo katika waraka huo. Matukio ya hivi karibuni ya SAKATA la ATCL na Mahujaji, yamedhihirisha udhaifu huo kwa kutozingatia maelekezo na utendaji wa kazi za kila siku.

Bado hatujachelewa, hili ni fundisho kubwa kwa Shirika letu la ATCL katika kusimamia maelekezo yale yote yaliyomo kwenye waraka huo.

9.0 MAJUMUISHO

Katika sakata hili, Bodi imebaini kuwa:-

* Utaratibu mzima wa kushughulikia suala hili ulikosewa baada ya Mwenyekiti kuanza kujiingiza kwenye utendaji.

* Mkurugenzi Mtendaji hakuwajibika ipasavyo baada ya kuandika barua ya kutoridhia maombi ya Mahujaji na kushindwa kuhakikisha kwamba maamuzi yake ya awali ya kukataa yanatekelezwa.

* Uongozi wa ATCL haukuwajibika ipasavyo kwa kuliacha suala hili liwe “one man show” badala ya kushughulikiwa na kamati maalum ya Hijja, yaani “Hijja Committee” ambayo ingehusisha idara ya Masoko, Uendeshaji, (Operations) Fedha na Mwanasheria wa Shirika. Kamati hii ingesaidia sana kugundua mapema kasoro za upatikanaji wa ndege “slots” na vibali vingine na kutafuta mipango mbadala ya kuokoa hali hiyo.

* Makabidhiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa Uendeshaji na Afisa Masoko hayakuzingatia taratibu za kiutawala. Kazi hii muhimu ilipaswa ikabidhiwe kwa Mkurugenzi Masoko, ambaye angeweza yeye kwa wadhifa wake kutumia maafisa wengine waliochini yao.

* Mwenyekiti wa Bodi alikosea kukutana na Mahujaji na kuwaahidi kuwa ATCL itabeba mzigo wa kutoa ruzuku bila kibali cha Bodi ya Wakurugenzi. Jambo hili lina athari ya kifedha na Bodi ndiyo yenye maamuzi ya mwisho juu ya masuala ya fedha na haswa ambayo hayamo kwenye Bajeti ya Shirika.

10.0 MAPENDEKEZO

* Bodi inasisitiza kuwa mamlaka yake ya kiutendaji yasiingilie kamwe shughuli za uendeshaji wa Shirika kama ilivyoainishwa katika Waraka wenye Kumb. Na. SHC/B.40/6/21 wa tarehe 28/3/1994.

Vile vile na Menejimenti isijichukulie mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba ya Bodi.

* Kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa Shirika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria (kushitakiwa) na Mahujaji ni vyema ifanywe mikakati ya kukutana na uongozi wa Mahujaji walioko nchini ili kutafuta muafaka mapema kabla Mahujaji hawajarudi nchini.

* Shirika lisijihusishe tena na usafirishaji wa Mahujaji hadi hapo litakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo baada ya kupata idhini ya Bodi ya ATCL na Serikali.

* Kutokana na uzito wa suala lenyewe lilivyojitokeza kwa umma wa Tanzania na ulimwengu kwa ujumla Bodi inapendekeza kuwa Mwenyekiti alitolee maelezo bayana kwa umma kwa jinsi alivyohusika.

* Kutokana na kutosimamia kikamilifu suala hili Bodi inapendekeza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL apewe karipio ili iwe fundisho kwake.

* Bodi itachukua hatua itakazoona zinafaa kwa kuwawajibisha waliohusika katika Menejimenti.

11.0 MWISHO

Bodi ya ATCL inaishukuru Serikali ambayo ndiye mwenye hisa zote za Shirika hili kwa jinsi walivyoingilia kati.

Shukurani ziende kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa Kamati rasmi ya Komandi ya kuokoa ATCL, Dr. Enos Bukuku kwa kazi nzuri sana waliyoifanya kupunguza aibu ambayo ingetupata.

Tunawapongeza na kuwashukuru Viongozi wa dini ya Kiislamu na Mahujaji wote kwa utulivu na uelewa waliouonyesha wakati wote huu wa usumbufu wa safari yao ya Hijja. Tunaiomba Serikali kwa wakati huu ambao Bodi inajaribu kusawazisha athari hizi mbele ya watumishi na mbele ya Umma wote wa Tanzania, iendelee na Kamati yake (Command Post) hadi Mahujaji watakaporejea.

Ni ukweli usiopingika kuwa Bodi nzima imechafuliwa mbele ya uso wa Watanzania; ni kweli pia Mwenyekiti wa Bodi aliwatenga wajumbe wa Bodi kutowahusisha katika maamuzi makubwa kama haya. Ni kweli pia Mkurugenzi Mtendaji alishindwa kumkatalia Mwenyekiti wa Bodi juu ya ATCL kutokuwa na uwezo wa kuingia katika mikataba ya ukodishaji wa ndege kwa ajili ya Mahujaji.

Lakini ni kweli pia katika hali hii wajumbe wamesononeshwa na kitendo hiki cha Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji kwa kutokutoa taarifa yeyote hata sakata lilipoanza hadi lilipotolewa na vyombo vya habari. Ni matarajio yetu kuwa Serikali italifafanua suala hili vizuri ili UKUNGU uliotanda mbele ya uso wa ATCL uondolewe.

http://www.raiamwema.co.tz/07/12/26/5.php
 
Hivi bodi ya ATCL inaundwa na akina nani? sababu inaonekana mwenyekiti anaweza kufanya analotaka bila kizuizi chochote. Lakini hizi bodi kwani zina ulazima kuwepo kwenye haya mashirika ya umma? au ndo zinarudisha nyuma ufanisi wa haya mashirika?

Tatizo naona kuna conflict of interest hapa -- nafikiri ATCL inabidi iwe makini sana kwani biashara ya airline inahitaji clear strategy sio kwa kuwa Mattaka alikuwa PPF akajenga maghorofa basi anaweza kuendesha ATCL kama kujenga maghorofa.
 
..hii sakata ina harufu ya UDINI-UDINI.

..Mwenyekiti wa Bodi inaigawa menejiment kwa kutumia Dini.

..Kama ni kulazimisha maamuzi yake, basi Mwenyekiti angefanya hivyo kwa management nzima, na siyo kwa watendaji Waislamu, huku akimtenga Mkurugenzi Mkuu Mkristo.

..Yuko Imamu aliyedai anakwenda kumsomea ITIKAFU David Mattaka kwa kuhujumu safari ya Hijja.

..Namfahamu Mzee Nyanganyi na nimesikitishwa sana kwa maamuzi yake haya. Naamini alikuwa na nia nzuri kabisa ila njia alizozitumia hazikuwa nzuri. Anapaswa kuwajibika.
 
Serikali mtegoni sakata la mahujaji

na Tamali Vullu
Tanzania Daima

SERIKALI sasa inaonekana kuingia katika mtego mwingine kuhusu safari ya mahujaji walioko Saudia, ambao wanakaribia kukamilisha ibada ya hijja.
Hali hiyo inajitokeza hasa baada ya Serikali ya Saudia nayo kuanza kuonyesha hofu dhidi ya mahujaji wa Tanzania, ikidhani kuwa wanaweza kuzamia nchini humo na hivyo kuwabana katika taratibu za safari.

Kwa upande mwingine, serikali imekiri kuwa haina uhakika wa safari ya mahujaji hao kurejea nchini.

Hadi jana mchana, serikali ilikuwa haifahamu siku ya kurejea nchini kwa mahujaji hao waliokwenda kwa ajili ya ibada ya hija, Makka, Saudi Arabia.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, mpaka jana mchana, kamati ya inayoshughulikia safari ya mahujaji hao ilikuwa ikiendelea na vikao vyake kujadiliana na kupanga tarehe ya kuwarejesha mahujaji hao nchini na ndege watakayotumia.

Hayo yalithibitishwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, alipozungumza na gazeti hili, kutoa ufafanuzi wa safari hiyo ya mahujaji.

Hata hivyo, Chambo, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, alisema kuwa kutokana na unyeti wa suala hilo, ndiyo maana jana kamati hiyo ililazimika kukutana kujadili suala hilo, licha ya kuwa ni siku ya mapumziko.

"Mpaka sasa sijafahamu mahujaji hao watarejea lini, hivyo tumekutana hapa na kujadili ili kupanga siku ya kurejea kwa mahujaji hao… si unaona tupo hapa leo ingawa si sikukuu?" alisema Chambo.

Alipotakiwa aeleze ni mashirika gani ya ndege ambayo tayari serikali imewasiliana nayo kwa ajili ya safari ya mahujaji hao, Chambo alikataa kulizungumzia suala hilo akidai kuwa ni la kibiashara.

Hata hivyo, alilihakikishia gazeti hili kuwa, kulikuwa na uwezekano baada ya kikao cha jana, masuala mengi kuhusu safari hiyo ya mahujaji kurejea nchini, yakafahamika.

Aidha, akifafanua kukwama kwa mahujaji hao katika mji wa Makka, Chambo alieleza kuwa walichelewa kutoka katika mji huo kwenda Madina baada ya kuzuiliwa na serikali ya Saudia.

Alisema kuwa serikali hiyo iliwazuia kwa hofu kuwa baadhi yao wanaweza 'kuzamia' au kuzidisha siku za kukaa kinyume cha taratibu za viza zao.

Hata hivyo, alisema mahujaji hao wameruhusiwa kwenda Madina baada ya Balozi wa Tanzania nchini Saudia kuihakikishia serikali ya nchi hiyo kwamba hakuna hujaji atakayezamia wala kuzidisha siku za kukaa huko. Alisema kwa kawaida ibada hiyo hufanyika si zaidi ya siku nane.

"Balozi wetu nchini Saudia amenipigia simu na kunieleza kuwa mahujaji hao hawakuweza kwenda Madina kutokana na serikali ya nchi hiyo kuhofu kwamba wanaweza kuzidisha siku za kukaa huko ama kuzamia.

"Lakini Balozi ameihakikisha serikali ya nchi hiyo kuwa hakuna hujaji atakayezamia, hivyo wameruhusiwa kwenda Madina," alisema Chambo na kuongeza kuwa mahujaji hao wanakwenda Madina kumalizia ibada hiyo kwa kuwa walichelewa kwenda Makka na kwamba wakimaliza ibada hiyo watawapelekea ndege ya kuwarejesha nchini.

Wakati serikali ikieleza hayo, habari kutoka Makka zinaeleza kuwa hadi jana mchana, mahujaji hao walikuwa hawajui lini wataondoka Makka kwenda Madina.

Habari hizo zinaeleza kuwa, mpaka jana vikao vya ujumbe kutoka Tanzania na Balozi vilikuwa vikiendea, lakini hakuna mafaniko yaliyopatikana.

Mmoja wa mahujaji alilitumia gazeti hili ujumbe wa simu ya mkononi (SMS) akieleza kuwa hawana uhakika wa safari ya kutoka Makka kwenda Madina, achilia mbali safari ya kurejea nchini.

"A alaykum. Habari za huku ni kwamba vikao vinazidi kuendelea kila siku pamoja na ujumbe kutoka Tanzania na balozi. Lakini mafanikio mpaka jana ni mabaya.

"Barua waliyopewa viongozi wa mahujaji haikukubaliwa na wizara ya usimamizi wa mahujaji ya Saudia, kwa hiyo bado tupo Makka na hatujui lini tutakwenda madina…" alisema hujaji huyo kupitia sms.

Juzi kulikuwa na taarifa kwamba huenda mahujaji hao wakarejea nchini Januari 17, mwakani kutokana na kukosa usafiri wa ndege ya kuwarejesha nchini mapema.

Taarifa hizo zilitolewa na mmoja wa hujaji aliyeko Makka, ambaye alieleza taarifa hizo walizipata baada ya ujumbe kutoka Tanzania na viongozi wa jumuiya ya kiislamu kufanya kikao.

Hata hivyo, mahujaji hao hawakukubaliana na majibu hayo na kwamba waliendelea kusisitiza kurudi nchini Desemba 29 au 30, mwaka huu kama walivyokubaliana awali na kwamba kikao kingine kilipangwa kufanyika juzi, ili kutoa hatma ya safari yao ya kurejea nchini.

Awali, ilielezwa kuwa mahujaji hao walikwama kuondoka Makka kwenda Madina kutokana na kutokuwa na vithibitisho kamili vya ratiba ya safari zao, ambavyo mamlaka ya usafiri ya huko inatakiwa ivithibitishe kabla ya kuondoka.

Mahujaji hao, pamoja na wengine kutoka nchi jirani, walisota katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwa siku kadhaa kutokana na kutopatikana kwa ndege ya kuwasafirisha kwenda Saudia.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kushindwa kuileta ndege iliyodai kuwa iliikodi kwa ajili ya kuwasafirisha mahujaji hao.
 
Wazee akina Nyang'anyi walitaka kupiga bao la mwishomwisho ktk maisha.Lakini sioni tatizo kwa Serikali ambayo yenye kampuni ya ATC kuchukua lawama na mzigo wote kwani ni watu wao wenyewe.Nyang'anyi kama jina lake linavyosomeka ni mnyang'anyi kwelikweli.
Siwezi kujua alifanya kwa nia mbaya au nia njema ili awasaidie Waislamu kwenda Hijja lakini matokeo yake yakawa haya.
Kama alifanya kwa nia mzuri nampa pole na Mumgu anajua na atamlipa ila kama alifanya kwa nia mbaya hiyo ni miongoni mwa good days ambapo yamemtokea puani na wazee wenzake wa Bodi wanamkana ilihali wanajuana.
Kuleana na kujuana.Sasa tuone nini kitatokea.Wote Mataka na Mnyang'anyi watafanywa nini?
Ili ni jambo la kuvuta Subira.
 
Pilgrims coming back on Jan 6, govt assures

By Mnaku Mbani
THE CITIZEN

The news comes amid worries that over 1000 pilgrims have been stranded again in Saudi Arabia after the government failed to secure the plane to carry them back home. Mr Omar Chambo, the deputy permanent secretary at the Ministry of Infrastructure Development, who chairs a task force to coordinate the pilgrims return, says that all the pilgrims will return home as scheduled.

After finishing their Hajj in Mecca, the pilgrims were expected to fly to Medina starting yesterday for final rituals, which they failed to attend after being stranded at the Julius Nyerere International Airport before departing, he elaborated. We have asked the Saudi government to authorize our pilgrims to stay there for some days to finalise the remaining rituals, the official noted yesterday.

The pilgrims were supposed to attend the Hajj ritual event by December 22 but lacked authorization documents to enter Medina, he said.
They are expected to stay in Medina for eight days before boarding a return flight with the Air Tanzania Co. Ltd (ATCL), he further noted.

Three ATCL officials were in Saudi Arabia to liaise with the pilgrims committee on how to smoothen arrangements for the return flight, he said. Some pilgrims who have finished their pilgrimage in Mecca say their journey is still on the crossroads, reports indicated.

Certain sources said that there was no possibility of the pilgrims flying to Medina despite that their hotel accommodation booking ends today.

We are frustrated here because accommodation booking is ending and the hotel�s authority will simply order us to pack our bags, said Sheikh Aksabat Said, a pilgrim. Reports from Saudia say pilgrims from other countries have already left after performing Hajj rituals.

Sheikh Azeberth Said, another pilgrim, said in a telephone interview yesterday that the Tanzania's embassy in Saudia was unclear about their travel arrangements but they were promised to leave Mecca for Medina yesterday. What government authorities here told us is that the plane has been obtained, he said.

Sheikh Said said the pilgrims were supposed to leave three days ago but embassy officials were still struggling to process travel documents.

The embassy gave them documents for the Medina trip, but when they arrived at the airport, the scheduled airline officials disputed the documents they were carrying. We didn't believe what we were told by the airline official," he aid, noting that the flight indicated in their travel documents was deemed not schedule on that day.

The pilgrims' hijja mission developed difficulties at the point of departure at the local international airport after ATCL failed to produce a plane to ferry them to Saudia. ATCL later explained that it had agreed with a Ras Al-Khaimah RAS leasing company to furnish the plane, "but the deal later fell apart." RAS leasing was supposed to bring a Boeing 747 Jumbo jet to carry more than 450 passengers.

ATCL then contacted Alwasam Co., a Jeddah-based firm, which leased a DC 10 plane from Global Leasing PLC of South Africa, which flew all pilgrims in three trips.
 
Nadhani tumeelewa kwanini Mkapa aliweka wageni katika Board za NMB, NBC na CRDB. Tunamwona Dr.Kimei kama mtu mwenye mafanikio lakini tukumbuke danida wana hisa mle, tunaona exim kuwa benk yenye mafanikio tukumbuke IFC wanahisa zao pale.
 
Nadhani tumeelewa kwanini Mkapa aliweka wageni katika Board za NMB, NBC na CRDB. Tunamwona Dr.Kimei kama mtu mwenye mafanikio lakini tukumbuke danida wana hisa mle, tunaona exim kuwa benk yenye mafanikio tukumbuke IFC wanahisa zao pale.

Usituchefue na habari za Mwizi Mkapa na NET GROUP je??; NA TTCL??
 
Katika kufuatilia sakata hili habari nyeti ambazo zimefika studio ni kuwa hadi hivi sasa hakuna slots za ndege zitakazochukua mahujaji kuwarudisha nyumbani wiki ijayo. Habari hizo nyeti ambazo KLH imeziona zinaeleza wazi kuwa uwezekano wa kupata slots za kuchukua mahujaji wetu kuwarudisha nyumani zitaanza kupatikana kuanzia tarehe ya 17 Januari. Maofisa wa ATC waliofuatilia kupata nafasi ili kutimiza ahadi yao kwa Watanzania kuwa mahujaji watarudi nyumbani wiki ijayo juhudi zao zimegonga mwamba.

Shirika la ndege lililotumika kuwachukua mahujaji ndilo lilitakiwa liwarudishe pia lakini tatizo ni kuwa kwa utaratibu wao waliotangulia kufika ndio wanatangulia kuondoka na kwa vile mahujaji wetu walichelewa kufika basi watachelewa kuondoka kwani ndege iliyotumika inatakiwa kutumika kuwarudisha mahujaji wa Iraq kwanza.

Katika waraka wake wenye tarehe ya leo (ambao KLHN Imepata nakala yake) Katibu Mkuu wa Miundo mbinu wamewataka ATC kufanya kila wanaloweza ili mahujaji warudi kama ilivyopangwa ukizingatia kuwa Rais alipozungumza na waandihi wa habari wiki moja kidogo iliyopita aliwahakikishia Watanzania kuwa mahujaji hawatapa matatizo wakati wa kurudi. Katibu huyo amewataka ATC kuibembeleza kampuni hiyo ili angalau wakubali kutoa slot moja ya Wairaq kwa Watanzania.

Kwa kifupi ni kuwa ndugu zetu watakwama tena Saudia unless Rais Kikwete atume Gulfstream yake na hata hapo tatizo bado litakuwa ni slots!

Mnaweza kunikuu.
 
tuombe mungu wafrudi salama waislamu wenzangu hiyo ndio hali halisi natoka wizarani kuulizia hili swala nkapewa hiyo

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT

Telegrams: "MIUNDOMBINU", Dar es Salaam
Telephone: 2114425/2112858 P.O. BOX 9144,
Fax: 255 022 2112751/2116032 DAR ES SALAAM.


Ref: ATCL/HIJA/07 29th Desemba, 2007


Mark Manji
Mwakilishi wa ATCL Saudi Arabia,


Yah: KURUDI KWA MAHUJAJI

Kamati iliyoundwa kusimamia kurudi kwa mahujaji imepitia ripoti yako na kuwa na wasiwasi juu ya lini hasa mahujaji wa Tanzania wataanza kurudi hasa kwa kuzingatia kuwa shughuli za Irak zinaweza zikaendelea hata baada ya tarehe 1 Januari 2008 na hivyo tukawa hatuna uhakika wa slots ifikapo tarehe 2 Januari 2008.

Rais amekwisha taarifiwa kuwa mahujaji wataanza kurudi tarehe 31 Desemba 07 hadi tarehe 2 Januari 08. Tarehe hizi haziwezi kubadilishwa na hivyo Serikali imeingilia kati suala la upatikanaji wa slots na ndege nyingine ili safari zianze kama ilivyopangwa. Ndege ya Global Aviation itatumika kubeba mahujaji ambao watakuwa wamebaki wakati itakapomaliza shughuli ya Irak.

Hivyo unaagizwa ufanye yafuatayo:

1. Ongea na uongozi wa SAMEK ili kutumia angalau slot moja kati ya kumi walizopewa Irak.
2. Ongea na uongozi wa SAMEK ili kuwaarifu kuwa Serikali inaandaa ndege nyingine kuanza safari za kuwarejesha mahujaji wa Tanzania tarehe 31 Desemba 2007. Ndege DC10 ya Global aviation itatumika kumalizia mahujaji watakaokuwa wamebaki. Kapteni Muze atakutumia taarifa za ndege hii nyingine. Suala la malipo ya ndege nyingine tutalijadili ili faida waliyopanga katika biashara hii isibadilike.

Fanyeni kila linalowezekana ili mahujaji waanze kurudi tarehe 31 Desemba 2007.

Wako,



O. Chambo
NAIBU KATIBU MKUU
 
Tumerogwa au tumelaaniwa, kwani kurogwa kunaweza kuganguliwa ila kulaaniwa ni mpaka aliyeacha laana aintengue mwenyewe kama keshakufa ndo inakuwa imetoka hiyo!!! Sasa ndo kama Tz yetu, likitoka hili linaingia lile alimradi vurugu tu! Sijui siye tumekosa nini.
 
Je wanaweza kuondokea mji mwingine? maana ukiangalia gharama za kubakia mpaka 17th Jan na kusafiri kwenda mji mwingine zinaweza kuwa sawa au pungufu.
 
Back
Top Bottom