Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

kasana,lunyungu,GT,chuma,bubu,...

..Mahujaji waliingia mkataba na ATC siyo serikali.

..Kisheria/Kimahakama ATC na serikali ni vyombo viwili tofauti kabisa.

..Kwa mtizamo wangu Mahujaji wanaweza kupata haki yao Mahakamani toka kwa ATC lakini siyo serikali.

..Mtu akiwa na madai na ATC na akashinda, basi mali za ATC zinaweza kukamatwa. Kama ATC haina kitu nadhani ndiyo imetoka hiyo. Mahakama haiwezi kuamuru wizara ya mawasiliano, au Ikulu, iuzwe ili kufidia, kwasababu ati ATC ni mali ya serikali.

..Leo hii IPP ikishitakiwa haina maana kwamba mali zote za Reginald Mengi zipo mashakani. Ni mali zile zilizoko chini ya IPP ndiyo zinaweza kufidia kesi ya madai.

..Ukiona serikali imeingilia suala kama hili la Mahujaji basi ujue imefanya hivyo for HUMANITARIAN or POLITICAL reasons.
 
Jokakuu.. point nzuri... lakini uhusiano ulipo kati ya ATC na serikali na mikataba wanayoingia sio sawa na ule wa Tanesco, Richmond na serikali? Nani aliingia mkataba wa Richmond na Tanesco?
 
Jinsi watu tuchanganyavyo mambo?

Nakumbuka katuni moja miaka ya 90 walichora jamaa anapalilia shamba lenye Maharage na mahindi.
Alipoulizwa ni aina gani hiyo ya kilimo cha kuchnganya mahindi na Maharage alijibu kwamba ni kilimo cha makande.

Asijue kwamba Makande hutokea tu pale upikapo mahindi na mharage pamoja mekoni na siyo kuotesha pamoja shambani.
 
Chuma sijaona haja ya kuniita Bwege kama nimekugusa pabaya jitetee. Mimi sikuweza kuona hoja hiyo kabla maana mimi kila siku niko njiani . You that far ku guess niko wapi. Mimi sijawahi kutoke nje ya Afrika na sina mpango so huyo wa London sijui ni nani . Lakini bado naombab mwenye kuelewa kwa kuwa ATC na Serikali kuna utofauti na kuona uongozi sasa Vipi waziri Mkuu aache hata ziara kwa jambo hili . Wenye kuweza kunipa shule wanipe Chuma endelea na matusi .
 
kasana,lunyungu,GT,chuma,bubu,...

..Mahujaji waliingia mkataba na ATC siyo serikali.

..Kisheria/Kimahakama ATC na serikali ni vyombo viwili tofauti kabisa.

..Ukiona serikali imeingilia suala kama hili la Mahujaji basi ujue imefanya hivyo for HUMANITARIAN or POLITICAL reasons.

Who own ATC??
 
kasana,lunyungu,GT,chuma,bubu,...

..Mahujaji waliingia mkataba na ATC siyo serikali.

..Kisheria/Kimahakama ATC na serikali ni vyombo viwili tofauti kabisa.

..Kwa mtizamo wangu Mahujaji wanaweza kupata haki yao Mahakamani toka kwa ATC lakini siyo serikali.

..Mtu akiwa na madai na ATC na akashinda, basi mali za ATC zinaweza kukamatwa. Kama ATC haina kitu nadhani ndiyo imetoka hiyo. Mahakama haiwezi kuamuru wizara ya mawasiliano, au Ikulu, iuzwe ili kufidia, kwasababu ati ATC ni mali ya serikali.

..Leo hii IPP ikishitakiwa haina maana kwamba mali zote za Reginald Mengi zipo mashakani. Ni mali zile zilizoko chini ya IPP ndiyo zinaweza kufidia kesi ya madai.

..Ukiona serikali imeingilia suala kama hili la Mahujaji basi ujue imefanya hivyo for HUMANITARIAN or POLITICAL reasons.

SERIKALI kama kawaida yake inacheza mchezo wa CHESS na waislam kama kweli ina nia ya kuwasaidia waislam ingeachana na kuwa:

KIMBELE MBELE KUTWACHAGULIA WAISLAM VIONGOZI

INGEACHA KUWAPENDELEA BAKWATA ambao waislam wengi hawaitambui

INGEWAPA ZANZIBAR REFERENDUM KAMA WAJIUNGE NA OIC

INGEACHANA NA UPUUZI WA KUJIDAI INAWAPENDA SANA WAISLAM KULIKO WASIO WAISLAM

INGWAACHIE WAISLAM WAAMUE KAMA WANATAKA KADHI AU LA

NA KAMA WANAMTAKA THEN IT SHOULD BE LEFT UP TO THEM
 
kasana,

..mimi nafikiri suala hili liamuliwe nje ya mahakama.

..Mahujaji waliingia mkataba na ATC, hawakuingia mkataba na serikali.

..mara nyingi tu wasafiri walikuwa wakikwama pale Railway station au bandarini. hatukusikia serikali ikiwakodishia mabasi au ndege.

..kitendo cha serikali kushughulikia suala hili kilitokana na msukumo wa KISIASA na KIBINADAMU.

GAME THEORY,

..umetoka nje ya mada, pamoja na kwamba madai yako ni ya msingi.

..kwanza, mahujaji waliokwama siyo wafuasi wa BAKWATA.

..napinga Zenj kujiunga na OIC. Lakini naunga mkono Tanzania kama Jamhuri kujiunga na OIC.

..Waislamu wangechagua tu Kadhi wao mkuu kwa utaratibu ambao hauhusishi katiba ya nchi.

..Waanglikana, Walutheri,Ismailia,Bohora,Maasai,Nyamwezi, wote wana viongozi wao wakuu na utaratibu wao wa kuwachagua bila kuhusisha katiba ya nchi.

..hivi hakuna KIONGOZI wa KIISLAMU ambaye ni PRAGMATIC wa kuwaunganisha Waislamu wote bila kujali kama wanaunga mkono BAKWATA or not?
 
Mimi nadhani haya yote ni matatizo yanayotokana na kushindwa kutenganua majukumu ya watendaji na wanasiasa.Imekuwa kawaida sasa mawaziri kuwa wasemaji wakuu wa mashirika yaliyochini yao badala ya viongozi wa hayo mashirika. Mfano wa hivi karibuni ni Mheshimiwa Kapuya akizungumzia mradi wa Bio-gas wa NYUMBU, Mheshimiwa Magufuli akizungumzia mradi wa nyumba za NHC n.k. Tumeshindwa kuyaichia haya mashirika uhuru na responsibility ya kufanya maamuzi yao. Kwenye hili vile vile, mkataba ulikuwa kati wa wasafiri na msafirishaji. Wangeachwa wamaliziane hata kama ingebidi msafirishaji apelekwe mahakamani na kufilisiwa. Hii ingetoa fundisho kwa pande zote mbili, kwa msafiri kujua kwamba ni jukumu lake kutafuta msafirishaji wa UHAKIKA atakayemfikisha anakotaka kufika katika wakati muafaka na bei nafuu bila kuangalia uzalendo au huyu ni wa kwetu na msafirishaji kujua kuwa akivunja mkataba atatoswa, pure and simple. Kwa kufanya ilivyofanywa inaweka precedent kuwa hapo baadaye wengine walio katika hali (mahujaji wengine-waislamu,wakristu,wahindi n.k, timu zetu za michezo, wasafiri wa treni n.k.) kama hii wataona ni haki yao serikali kuwakwamua na juu ya yote kuwapa kifuta jasho. Haikutakiwa kufika hapa. Kama serikali ingeona ni muhimu kuingilia, ingemsukuma msafirishaji kwa chini na kumwacha awe ndiye mhusika mkuu. Msaada wowote ambao angepewa ingejulikana kwamba ni mkopo. Msafirishaji ndiye angewajibika na kuwasafirisha mahujaji na kulipia gharama za ziada zinazotokana na kucheleweshwa kwao ( malazi ya hoteli, usafiri, chakula n.k.).Makubaliano ya kitu kama kifuta jasho kingewekwa wazi katika makubaliano kati ya waliohusika na mkataba.Huu ungebaki mkataba wa kibiashara bila kuingiza maswala ya ubinadamu. Tusiuangalie kupitia darubini la imani, uzalendo au ubinadamu.
 
GAME THEORY,

..umetoka nje ya mada, pamoja na kwamba madai yako ni ya msingi.

..kwanza, mahujaji waliokwama siyo wafuasi wa BAKWATA.

..napinga Zenj kujiunga na OIC. Lakini naunga mkono Tanzania kama Jamhuri kujiunga na OIC.

..Waislamu wangechagua tu Kadhi wao mkuu kwa utaratibu ambao hauhusishi katiba ya nchi.

..Waanglikana, Walutheri,Ismailia,Bohora,Maasai,Nyamwezi, wote wana viongozi wao wakuu na utaratibu wao wa kuwachagua bila kuhusisha katiba ya nchi.

..hivi hakuna KIONGOZI wa KIISLAMU ambaye ni PRAGMATIC wa kuwaunganisha Waislamu wote bila kujali kama wanaunga mkono BAKWATA or not?

kwa hiyo unabisha serikali haiwachaguliii waislam viongozi wao?

mzee hapa kila kitu kiko connected

Huwezi kuongelea waislam Tanzania bila kuwaingiza BAKWATA na serikali

kwa taarifa yako waislam hawaoni tofauti kati ya BAKWATA na serikali na wao wanaamini kuwa vyombo hivyo viwili huwa wanaconspire dhidi ya waislam

ZANZIBAR kujiunga na OIC ni haki yao na kama issue ni kubadilisha katiba ya ZNZ then let it be...after all ile ni nchi yao

Upuuzi ninaokataa mimi ni pale serikali kuingiilia mambo ya kidini kuwaonyesha waumini waswali lini iddi, kuwabagua kwa kuwaweka close BAKWATA na zaidi ya yote serikali kuwahudumua mahujaji as if hiyo ndio itakuwa ni solution ya malalamiko ya waislam serikalini

What you see now ni ile mbegu iliyopandwa ya kuwaambia watu eti serikali haina dini lakini wananchi wanzo dini...ile nyimbo ya taifa kwa nini imekaa kama dua ? Mungu anafanya nini kwenye nyimbo ya taifa?
 
GT,

..kama Waislamu hawapendi kuchaguliwa viongozi wao na serikali basi wasingependekeza Mahakama ya Kadhi iundwe kwa sheria ya Bunge.

..unazungumza as if BAKWATA siyo WAISLAMU.

..hii vita dhidi ya BAKWATA inawezekana ni ya kugombea ulaji tu.

..kuna watu wamekosa ulaji kwa kuanzishwa kwa BAKWATA, and they havent gotten over it.

..Kikatiba Zenj haina haki kujiunga na OIC. Kinachotakiwa kufanyika ni Tanzania ijiunge na OIC.

..Zenj siyo dola. umeshasahau hukumu ya mahakama ya Rufaa kuhusu kesi ya uhaini Zenj. I guess tulikuwa excited with the decision and never thought about the implications.
 
Salamu kwenu Mwenyekiti Bodi ya ATCL na TANESCO.

Mwenyekiti wa ATCL......

Ukiona mwenzako ameshanyoLEWA basi na wewe TIA MAJI,unafikiri MUUNGWANA atakuwacha.umeitia serikali HASARA mabilioni ya pesa kwa kushindwa kuwapeleka MAHUJAJI kwa muda uliokubaliana nao,matokeo yake JK na EL ikabidi waliingilie kati suala hilo.zaidi alivyofika uwanja wa ndege mkawachukua mahujaji na kupakia ktk ndege,alivyoondoka tu mkawashusha........KWA HIYO NA WEWE JITAYARISHE AMA ZAKO ama za MUUNGWANA LAZIMA ALE SAMBAMBA NA WEWE.

Mwenyekiti wa TANESCO........

duh wewe ndio husemeki,manake JK kila akivuta PUMZI anahasira na RICHMONDS.jitayarishe na wewe.

KULA 5 Mkulu Mheshimiwa Muungwana JK kuanza kuwaFANYIA kweli MAFISADI WA NCHI YETU.
 
You must not be serious guy, hivi wewe kwa akili yako unamwona JK ni mtu serious wa kuweza kushughulikia suala la Tanesco na ATCL? Wewe kwa akili yako unadhani suala la Ubadhilifu BOT alikuwa halifahamu? Amechukua hatua na kumtoa sadaka Balali kwa sababu tu ya kuwafumba macho waTZ na kuwafurahisha Wazungu. Dont expect anything from the Kamati Ya IGP na AG iliyoundwa. Is just to buy time Wabongo lala mlaze bongo zenu wenzenu waendelee kutanua.JK is not serious, this is terrible thing to this country, tunabahati Mbaya sana.

Mnafikiri Makachero wa nchi hii hawakumpa issue kwamba wajanja wanachota hazina yetu pale BoT? Kwanini haku react mpaka asubiri Wazungu wamsukume? Report ya CAG hakuiona? Mitandao alikopata Slaa habari hizi makachero wake hawaichungulii? Tusidanganyane, hakuna kinachofanyika and I say the only serious president of this country was Nyerere and Mwinyi, Hawakuwa mafisadi kabisa
 
Salamu kwenu Mwenyekiti Bodi ya ATCL na TANESCO.

Mwenyekiti wa ATCL......

Ukiona mwenzako ameshanyoLEWA basi na wewe TIA MAJI,unafikiri MUUNGWANA atakuwacha.umeitia serikali HASARA mabilioni ya pesa kwa kushindwa kuwapeleka MAHUJAJI kwa muda uliokubaliana nao,matokeo yake JK na EL ikabidi waliingilie kati suala hilo.zaidi alivyofika uwanja wa ndege mkawachukua mahujaji na kupakia ktk ndege,alivyoondoka tu mkawashusha........KWA HIYO NA WEWE JITAYARISHE AMA ZAKO ama za MUUNGWANA LAZIMA ALE SAMBAMBA NA WEWE.

Mwenyekiti wa TANESCO........

duh wewe ndio husemeki,manake JK kila akivuta PUMZI anahasira na RICHMONDS.jitayarishe na wewe.

KULA 5 Mkulu Mheshimiwa Muungwana JK kuanza kuwaFANYIA kweli MAFISADI WA NCHI YETU.

It does not take much to win Tanzanians. Kama wananchi ndio wanamtazamo huu kweli tutafika???

Watawala nao wanajua namna ya kuwadanganya waTZ. Haya ngoja tuone
 
Nimesoma na kufuatilia suala la 'sakata la mahujaji' toka mwanzo hadi mwisho. Nimekuwa ninamuomba mungu wakati wa kipindi chote hicho niendelee kuwa na moyo wa subira wakati suala hilo lilipokuwa linashughulikiwa na vyombo mbalimbali ikiwemo serikali.
Hakika wanadamu tunapopewa uhai basi huambatana na mitihani / majaribu. Safari ya kwenda Makka kuhiji kwa mahujaji wetu ilipangwa na Mwenyezi Mungu tangu siku waja hawa walipozaliwa na tayari alishaelekeza jinsi watakavyo safiri kufika huko. Kilichotokea hapa ni mchakato mzima wa mipango yake Mwenyezi Mungu.
Kama binadamu, viumbe wake, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo analotupatia kwani kila jambo lina sababu zake.
Hakuna haja ya kunyoosheana vidole katika hili tena kwani ni jambo ambalo liko wazi kabisa.
Mungu ameleta mtihani kwa waja wake wanaokwenda hija kuanzia kwenye nia zao, kufanya maamuzi ya kwenda au kutokwenda (kwa maana ya kutumia mali zao kugharimia safari)na mambo mengine kadhaa hapahapa kabla hawajaondoka na ameweza kuona imani zao.
Napenda kuchukua nafasi kuwashukuru wale wote waliojitokeza kushughulikia suala hili kuanzia kwa Mh. Rais, Mh. Waziri Mkuu, Waziri wa Miundo Mbinu, pamoja na vyombo vingine vyote ya serikali na visivyo vya kiserikali.
Napenda pia kuchukua fursa hii kuwapa pole mahujaji wote waliokumbwa na kadhia hii kwa moyo wao subira na kushilikia mafunzo na maelekezo ya dini yao.
Pia napenda kuwapa pole wale wote kwa nia njema kabisa walikuwa wanataka kufanikisha safari hizi za mahujaji lakini baada ya kutokea kadhia hii wakajikuta wakiwa katika matatizo haya au yale waelewe kuwa jitihada zao hazishindi kudra za Mwenyezi Mungu nina hakika walikuwa na nia njema na safi.
Kwa upande wa Kampuni ya Ndege (ATCL), tumieni wakati huu adhimu kusahihisha makosa ya kimaamuzi na kiutendaji, mimi binafsi bado nina imani na Bodi na Menejimenti ya ATCL katika kutekeleza majukumu yake, isipokuwa inatakiwa ijipange vizuri zaidi. Ikumbukwe kuwa kunapotokea crisis jambo muhimu ni kutulia na kufanya kazi kwa kufuata maelekezo bila ya kutetereka.
Mwisho suala la mahujaji limekwisha tuachie serikali na watendaji wengine wapate muda wa kupitia yaliyotokea.
 
Nilipokuwa mdogo kitu kimoja kilikuwa kinanisumbua kuhusu nafasi ya Mwenyezi Mungu katika maisha ya binadamu. Nilifundishwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupangia maisha yetu na ni yeye ndiye anayejua siku na namna ambavyo kila mmoja wetu atakavyoondoka hapa duniani. Nilichokuwa najiuliza ni kuwa: kama ni hivi, basi kwa nini tunamhukumu yule ambaye atatimiza hili kwa kumchoma kisu mwenzake? Si alikuwa anatimiza mapenzi/mipango ya Mwenyezi?Huyu mtu, si alistahili kuzawadiwa na kupongezwa? Badala ya hivyo, huyu mtu hasira za jamii na dola zitamwangukia. Tusitumie kisingizio cha mapenzi/mipango ya Mungu kutetea uzembe na udhaifu wetu wa kibinadamu. Si amini kuwa Mwenyezi alikusudia waja wake wateseke vile uwanjani. Tunatakiwa kama jamii kudai kuwa wale ambao wanapewa dhamana katika jamii wanaitekeleza inavyopaswa na si vinginevyo. Ndiyo maana ya responsibility. Au utu uzima.
 
Tatizo la watanzania ni kuongea bila vigezo, nyie wadau mnaozungumza maneno ya kashfa kuhusu Balozi nyanganyi na kusema yeye ni mbomoaji nadhani hamna vigezo. Kama unataka kujua mambo aliyoyafanya siyo Tanzania tu bali dunia nzima unaweza kwenda kwenye mtandao na kusearch by his name na utaona kazi kubwa aliyoifanya Marekani kuitangaza Tanzania na kujenga Umoja baina ya Watanzania wanaoishi huku, nenda World Bank na IMF na uone kiasi gani cha fedha alileta nyumbani kwa projects na misaada mbali mbali kipindi alichokuwa Balozi, namba ya watalii iliongezeka mara dufu kwa kipindi hicho. Alikwenda Uarabuni na akaendelea na hilo hilo. Hotel ya Kilimanjaro ilikuwa gofu na akaitangaza Tanzania na waarabu wakaja kufanya vitu vyao, akaanzisha umoja wa Watanzania wanaoishi huko UAE na kuunda katiba. Ukiacha haya yote ya nje ya nchi, aliicha wizara ya Mawasiliano ikiwa imesheehena ndege zikiruka Uarabuni, Uingereza na bara lot ela Afrika akiwa waziri wa Mawasiliano na uchukuzi.Mbona hamuongelei kilichotokea ni nini? Na ndege hizo zilienda wapi? Kakabidhiwa shirika halina hata helicopter ya kupaa!Sasa JAKAYA kumrudisha hapo kuwa mwenyekiti wa bodi haikuwa kwa sababu ya kujuana bali ni kwa ajili ya uzoefu alionao. Makosa hutokea lakini si vizuri watu kukashifu mtu kama hakufanya chochote katika nchi hii. Hawa ni viongozi wachache ambao wameitumikia nchi kwa uaminifu kwa kufanya kazi karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hadi alipostaafu! Tuwe wakweli na tujifunze kukumbuka Historia, na siyo kuendeleza gumzo lisilo na maaana.
 
Heshima mbele..... Duh naona mambo yanakuwa moto kwelikweli, kajiswali kangu ni kadogo sna kwa kweli, "Hivi lile dege letu la eabasi lilikuwa lije kama wiki chache zilizopita mbona haliji na badala yake tunaambiwa kwenye "press conference" kwamba litakuja litakuja, sasa kuchelewa kwake kimkataba hakuna vijisenti wanatakiwa kutulipa (liquidated damages)??".... Kama mkataba unasema vilipwe, wameshaanza kuvilipa??

Mwisho ni kurudia tu, "Je huu mkataba ukoje?" au nao ni siri ya Taifa kama ilivyokuwa Richmon.....

Naomba kuwakilisha.................
 
Back
Top Bottom