Bundi ameanza kunyemelea familia ya Zitto Kabwe. Mama Mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ameitisha kikao juzi kujadili mustakabali wa familia. Mtoa habari wetu ambaye ni mmoja wa wanafamilia aliyehudhuria kikao hicho anaeleza kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na wanafamilia wa karibu akiwemo kaka wa Zitto anayejulikana kwa jina moja la Salum. Kikao hicho cha kifamilia kilijadili mustakabali wa kisiasa wa Zitto Kabwe na mambo yanayojitikeza ya chama chao cha CHADEMA. Baadhi ya watu wa karibu na familia walioalikwa kwenye kikao hicho ni pamoja na David Kafulila, ambaye Zitto amemtangaza hivi karibuni kuwa kijana mwenye akili anayemuandaa kuwa mbunge wa jimbo la jirani yake la Kigoma Kaskazini.
Kikao hicho cha kifamilia kimeazimia kuwa Zitto ajiuzulu na nafasi ya unaibu Katibu Mkuu CHADEMA ili asipoteze maisha kama Chacha Wangwe. Mama Mzazi wa Zitto Kabwe, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amethibitisha familia kuamua Zitto ajiondoe kwa ajili ya kulinda maisha yake. Mama huyo amenukuliwa na Gazeti la RAI akieleza kwamba familia inamtegemea sana Zitto na ameisadia kwa mengi hivyo wamemuandikia barua akiwa ujerumani kumweleza msimamo wao wa kutaka ajitoe.
Kikao hicho kilijadili misaada ya magari ambayo Zitto ametoa kwa baadhi ya vijana wanasiasa ndani ya CHADEMA kwa ajili ya kuwasaidia washinde katika majimbo yao ya uchaguzi. Mmoja kati ya watu hao anatajwa kuwa ni Msafiri Mtemelwa ambaye wakati wa uchaguzi wa ndani ya CHADEMA alikuwa Kampeni Meneja wa Zitto Kabwe kwenye kugombea nafasi ya uenyekiti na hata katika kupanga safu za viongozi wa ngazi zingine ndani ya CHADEMA. Familia ilielezwa kwamba hivi karibuni Msafiri alionekana akiongea na Katibu Mkuu Dr Slaa ofisini. Familia ikaelezwa kuwa alipigiwa simu hivi karibuni na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. Kutokana na mambo hayo, kikao hicho kilianza kumtilia mashaka kuwa amemgeuka Zitto Kabwe.
Mtoa habari wetu anafafanua kuwa David Kafulila alikieleza kikao kuwa Msafiri Mtemelwa alichangia uteuzi wake kama Afisa utenguliwe kwa kuwa alikuwa mjumbe wa Kikao cha Sekretariati kilichokaa chini ya uenyekiti wa Dr Slaa lakini hakumtetea. Kafulila aliendelea zaidi kukieleza kikao kuwa badala ya kupingana na wajumbe wengine wa sekretariati ili kumnusuru, Msafiri alitoa hoja kwamba atolewe nje ya kikao baada ya kujieleza kwa masaa manne ili maamuzi yaweze kufikiwa. Hivyo, wanafamilia walichukua uamuzi wa kumnyang'anya gari aliyopewa na Zitto Kabwe aina ya Prado. Uamuzi huu umeshatekelezwa kwa Msafiri Mtemelwa kunyang'anywa gari hiyo.
Mtoa habari wetu ameeleza kwamba maamuzi hayo na mambo mengine ya zamani yanaelekea kuigawa familia katika makundi mawili. Kundi moja likiwa ni lile linalolaumu urafiki na Zitto na baadhi ya marafiki wapya ambao wanaelekea kumweka mtoto wao mbali na viongozi wa chama chake na marafiki zake wa zamani na kumzushia migogoro yenye kutishia mustakabali wake wa kisiasa. Kundi lingine ni lile linaloamini kwamba viongozi wote wa kitaifa wa CHADEMA na marafiki wa zamani wanamchukia Zitto hivyo mustakabali wake wa kisiasa utategemea kuwashambulia na kuwamaliza viongozi hao na watu wanaotofautiana na Zitto; kundi hili linamsimamo kwamba kama mpango huu hautawezekana basi ni vizuri Zitto aache siasa kunusuru maisha yake.
Juzi gazeti la Alasiri limeandika ukurasa wa mbele habari ya kwamba Zitto ametangaza tena kuacha kugombea ubunge 2010 na badala yake anataka kuwa Mwalimu wa chuo Kikuu. Habari hiyo imefuatiwa na habari ya jana katika Gazeti la Rai ikimnukuu Mama Zitto akieleza kwamba mwanae ni msomi, afadhali afanye kazi zingine ili aendelee kuisaidia familia badala ya kubaki katika chama na kupoteza maisha yake.
Mwanafamilia huyo anaendelea kudodosa kuwa maadui wa Zitto wanatajwa kuwa ni Freeman Mbowe, Dr Slaa na wakurugenzi wote wa makao makuu ya CHADEMA isipokuwa Msafiri Mtemelwa. Katika orodha hiyo anatajwa pia mfanyabiashara mmoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari. Pia wabunge wote wa CHADEMA isipokuwa wawili. Gazeti la jana la Rai limeeleza pia katika kundi la wabunge anayeongoza kwa uadui na Zitto ni Halima Mdee ambaye anatajwa kuwa amewasilisha nyaraka ya tuhumu 22 dhidi ya Zitto Kabwe kwa chama hicho ikiwemo tuhuma zinazohusiana na masuala ya kampuni ya Dowans. Kutajwa kwa jina la Halima Mdee kumethibitisha maelezo ambayo Msaidizi wa Karibu wa Zitto Kabwe, Omar Ilyas aliwahi kuyatoa katika Mtandao wa Jamii Forums, akieleza kwamba yupo mbunge mmoja kijana ambaye alikuwa karibu na Zitto ambaye amemgeuka na kumtuhumu kwa mambo mbalimbali. Omar amekuwa akihusisha mbunge huyo, na jina la Mwafrika katika mtandao huo.
..........ndiyohiyo