Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Mwafrika,
Mkuu wangu samahani... hivi unatafuta cheo huko Chadema au?..maanake hatulali kila siku Zitto na Omar vipi mkuu wangu..mbona inakuwa kama hekaheka ya clouds halafu imekaa sana kijikoni!
 
Mwafrika, Mkuu wangu samahani... hivi unatafuta cheo huko Chadema au?..

No.

Sina mpango na sijawahi kuwa na mpango wa kuwa kiongozi wa chadema au wa chama chochote kile Tanzania. Kuna mengi tu kwa sasa yananizuia kufanya hivyo.
 
Mwafrika,
Mkuu wangu samahani... hivi unatafuta cheo huko Chadema au?..maanake hatulali kila siku Zitto na Omar vipi mkuu wangu..mbona inakuwa kama hekaheka ya clouds halafu imekaa sana kijikoni!

Hiyo ya habari za Zitto na wenzake, fuatilia kwa makini uone kuwa sio mimi ninazianzisha hapa. Most of the time, mimi ninachangia sana hiyo mijadala maana unakuta imejaa misinformation kibao.

Wanaozianzisha hizo habari wanajulikana, wengi wao ni wanaccm - mf habari ndiyo hiyo. Na nyingine nyingi zinaanzishwa na kambi ya zitto au wale wanaoonekana kama wanamtetea Zitto hapa jf - kina mkuyumkubwa, mbalamwezi na wenzao.

Ninachofanya hapa ni kujibu tu hoja zao ili kuweka record straight.
 
Mwafrika,
Mkuu wangu weee..tunakusoma sana lakini mengi unaanzisha wewe pia.. haya imekuwaje ukaleta haya hapa..

Na kisha mafisadi waende wamkolimbe Dada Halima buree kwa madai yasiyo na msingi kama haya. Zitto, Omar, Msafiri, Ndanda, Kafulila na wengineo wote kambi ya Zitto.
Mchawi wenu sio Halima Mdee, Mchawi wenu ni matendo yenu wenyewe na maneno yenu mnayoyatoa bila kuyapima. Eleweni kuwa Tanzania (na chadema in this case), ni kubwa zaidi kuliko Zitto Kabwe (bila kujali umaarufu ambao nyie mnadhani kuwa Zitto anao).
Hii inaonyesha chuki yako kwa Zitto na kusema kweli sijakusoma mahala popote ukizungumzia mapungufu ya Zitto kwa nia nzuri.. Inaonyesha wazi hata wewe uko kambi fulani ndani ya Chadema na unatazama tu upande wa pili pasipo nawe kujiuliza kwa nini upo kambi nyingine!
Hivi vita vyenu havina maana ya kuweka record straight isipokuwa kusodoana..
 
Mwafrika,
Mkuu wangu weee..tunakusoma sana lakini mengi unaanzisha wewe pia.. haya imekuwaje ukaleta haya hapa..

Hii inaonyesha chuki yako kwa Zitto na kusema kweli sijakusoma mahala popote ukizungumzia mapungufu ya Zitto kwa nia nzuri.. Inaonyesha wazi hata wewe uko kambi fulani ndani ya Chadema na unatazama tu upande wa pili pasipo nawe kujiuliza kwa nini upo kambi nyingine!
Hivi vita vyenu havina maana ya kuweka record straight isipokuwa kusodoana..

Mkandara,

Nitaenda taratibu kidogo ili uelewe nilichoandika.

Imewekwa habari hapo juu ikidai kuwa Halima Mdee ndiye anatumia jina la mwafrika. Mimi nikaonya kuwa, haya mambo ya kuweka habari za uongo na za kipuuzi kama hizi, zinaweza kupelekea mafisadi wakaamini kuwa mwafrika ndiye Halima Mdee na wakamtia dada wa watu matatizoni.

Ninahisi kuwa wewe pia umenunua hiyo propaganda kuwa Halima Mdee ni mwafrika (na wala sikulaumu kwa hili). Nilichoandika hapa ni specific toka kwa post ya habarindiyo hiyo ambaye kamkoti Omar Ilyasi kuhusu identity ya mwafrika.

Kuhusu kumpondea Zitto, inaonekana unataka kutojali miaka mitatu niliyotumia hapa nikiwa upande wa Zitto. Chukua muda usome maandishi yangu toka mwaka 2006 ugundue kuwa nimekuwa namtetea Zitto na kuwa upande wake mara kibao tu hapa.

Baada ya kuona Zitto anachowafanyia viongozi wenzake, hasa baada ya issue ya Dowans, nilikuwa nimefikia kikomo cha utetezi wangu kwa Zitto. Yaliyofuata ni history.
 
Naomba niwathibitishie woote akina Omar(kama anafikiria hivyo) kua wewe sio Halima na wala huna cheo chadema na wala haupo Tanzania.

Jamni niaminini Mwafrika sio Halima Mdee!!!

Nadhani wataelewa sasa

FP
 
FP,

Hii issue hata Max (ambaye tunafahamiana vizuri sana) amejaribu kuipatia ufumbuzi behind the scene. Kwa sheria za JF, Invisible hawezi kutaja majina halisi ya members wa JF hapa ndio maana hajaweka mkono kwenye hili.

Sidhani kama watakuamini haraka hivyo. Wao wameamua kutafuta uchawi wa matatizo yao kwenye mtu (ndani ya chadema) badala ya kwenye vitendo na maneno yao.

Ninamuhurumia dada Halima kwa yatakayomkuta (GOD forbid) kama wajinga fulani kwenye team ufisadi wakiamini kuwa yeye ndiye mwafrika.
 
FP,

Hii issue hata (edited) (ambao tunafahamiana vizuri sana) wamejaribu kuipatia ufumbuzi behind the scene. Kwa sheria za JF, Invisible hawezi kutaja majina halisi ya members wa JF hapa ndio maana hajaweka mkono kwenye hili.

Sidhani kama watakuamini haraka hivyo. Wao wameamua kutafuta uchawi wa matatizo yao kwenye mtu (ndani ya chadema) badala ya kwenye vitendo na maneno yao.

Ninamuhurumia dada Halima kwa yatakayomkuta (GOD forbid) kama wajinga fulani kwenye team ufisadi wakiamini kuwa yeye ndiye mwafrika.

Mwanzoni nilifikiria wewe ni mbunge wa Chadema, Nikafanya homework yangu kama nilivyofanya kwa marafiki wa Zitto kisiasa nikagundua unaandikia ukiwa nje ya nchi na nikagundua mengine baadhi ni kuwa wewe wala sio mwanachama wala kiongozi wa Chadema labda mpo RELATED NA UONGOZI. Sina uhakika na relationship lakini

Hivyo nimeku CLEAR na hizo shutuma
 
Naomba ufanye editing, huyo uliyemtaja hajulikani .....

Hope umeelewa
 
Mwanzoni nilifikiria wewe ni mbunge wa Chadema, Nikafanya homework yangu kama nilivyofanya kwa marafiki wa Zitto kisiasa nikagundua unaandikia ukiwa nje ya nchi na nikagundua mengine baadhi ni kuwa wewe wala sio mwanachama wala kiongozi wa Chadema labda mpo RELATED NA UONGOZI. Sina uhakika na relationship lakini

Hivyo nimeku CLEAR na hizo shutuma
Wenye akili wameshaelewa, ndio maana kachagua upande!
 
Mwanzoni nilifikiria wewe ni mbunge wa Chadema, Nikafanya homework yangu kama nilivyofanya kwa marafiki wa Zitto kisiasa nikagundua unaandikia ukiwa nje ya nchi na nikagundua mengine baadhi ni kuwa wewe wala sio mwanachama wala kiongozi wa Chadema labda mpo RELATED NA UONGOZI. Sina uhakika na relationship lakini

Hivyo nimeku CLEAR na hizo shutuma

Hope that makes the issue clear.
 
Mwafrika,
Ninahisi kuwa wewe pia umenunua hiyo propaganda kuwa Halima Mdee ni mwafrika (na wala sikulaumu kwa hili). Nilichoandika hapa ni specific toka kwa post ya habarindiyo hiyo ambaye kamkoti Omar Ilyasi kuhusu identity ya mwafrika.
Mkuu wangu ktk hili umekosea sana kwa sababu mimi simjui huyo Halima Mdee ndiye nani! wala sina mazoea wala ukaribu naye iweje nianze kufikiria kwamba wewe Mwafrika ndiye Mndee.

Mkuu utanisamehe lakini nakuomba sana unisikie hapa.. Tatizo la hoja zako nyingi zinahusu WATU yaani unatumia muda mwingi kuchambua na kufikiria watu wakati sisi tunazungumzia issues. Sijali wewe ni nani uwe Mbowe, Dr.Slaa au Mndee mimi sina mshirika katika habari yoyote zaidi ya kusoma hoja na kuzichanganua ktk mtazamo wangu. Mara kibao nimemkorofisha Zitto humu, nimezungumza mambo mengine kinyume cha ustaarabu pasipo kufikiria huyu ni nani isipokuwa maadishi ya mhusika.. That's me kwa hiyo unapohisi ama kudhani kwamba hata mimi nimenunua hiyo propaganda mkuu wangu inaonyesha wazi jinsi unavyojikisia mwenyewe.
Mimi nipo kwa jina langu, Zitto yupo kwa jina la ke huyo Omar nasikia pia yupo kwa jina lake isipokuwa wewe tu.

Na kama sikosei ni wewe uliyetufahamisha kuhusu huyo Omar ni nani na wana uhusiano gani na Zitto, kulikuwa na haja au sababu ya kufanya hivyo!..Pengine hufahamu kwamba sisi wengine tunapenda sana kuyaona hayo majina bandia kwani unaweza kurusha madongo pasipo kuonea aibu mtu, Nitakushauri tu mkuu wangu hizi habari za kutoa ID ya mtu achana nazo kwani wewe mwenyewe unaelewa vizuri hasara zake..
Halafu huu ubishi wenu mkuu wangu wala hauna maana hata kidogo, yaani tunakusomeni kama vile tunatazama horror movie - Inatisha.
 
Bila shaka atakusoma na kumaliza mjadala. Umeeleza vizuri sana na kwa muungwana hana haja ya kuendeleza mjadala huu. Ni vizuri tuamie mjadala mwingine.
Asanteni.
 
Mwasisi wa Chadema abariki Kafulila kuvuliwa uongozi
broken-heart.jpg
Na Hemed Kivuyo, Arusha

MUASISI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema anakubaliana na uongozi wa chama hicho kuwavua vyeo baadhi ya viongozi wake akiwamo Ofisa Habari, David Kafulila.

Mtei alitaka hatua hiyo isifananishwe na mgogoro ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao umesababishwa na maslahi binafsi.

Alisema baada ya Chadema kusitisha ajira za waajiriwa kadhaa baadhi ya watu wamepinga hatua hiyo na kuielezea kuwa ni mgogoro ndani ya chama hicho jambo ambalo sio kweli.

Alisema aliyewaondoa maafisa hao madarakani ni mwajiri halali mwenye mamlaka kisheria kusitisha ajira hizo.

Mtei aliongeza kuwa kilichopo ndani ya Chadema ni baadhi ya watu wasiofuata kanuni na misingi inayoongoza chama hicho ambao haoni sababu ya watu hao kuendelea kuwepo.

“Hao wanaosema kuwa Chadema ama katibu mkuu amekosea kuwaondoa kazini baadhi ya watu,hawapo sahihi,wale ni waajiriwa na ajira zao zinaweza kukoma wakati wowote kama ilivyofanywa na sioni sababu ya chadema kuendelea kuwa na watu wasiofuata misingi ya chama, alisema Mtei.

Alipoulizwa kama chama hicho kinaweza kutumia nafasi ya udhaifu uliopo ndani ya CCM kuchukua madaraka, alisisitiza kuwa ndani ya Chadema hakuna mgogoro na kwamba mgogoro upo ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema ndani ya CCM kuna mgogoro mkubwa ambao husababishwa na chama hicho kukosa mwelekeo kitu ambacho hakipo Chadema.

Aliongeza katika chama chochote cha siasa kuna utaratibu wa vikao na kwamba vikao hivyo vinakuwepo kutokana na misingi ya kukiweka chama katika hali nzuri.

Aliongeza Chadema ama chama kingine cha siasa kisifananishwe na taasisi ya kidini ambayo huimba wimbo mmoja mara kwa mara na kwamba pamoja na kuwepo kwa tofauti ya mawazo, kuna baadhi ya viongozi ambao huenda kinyume na misingi ya vyama.

Alisema kutokana na Chadema kuongozwa kwa vikao halali anaamini maamuzi yanayotolewa ni sahihi na kwamba chama hicho hakitasita kumwajibisha yeyote atakayeonekana kwenda kinyume na kanuni zake.

Mtei aliongeza kuwa anaamini kuwa ndani ya chama hicho alichoshiriki kukiasisi hakuna mpasuko zaidi ya kuzidi kukiimarisha. Juzi chama hicho kilitangaza kuwaondosha katika nyadhifa zao viongozi wawili ambao ni David Kafulila na Danda Juju aliyekuwa akishughulikia mambo ya Bunge katika chama hicho.
 
wacha wafukuzwe..hakuna aliye mkubwa zaidi ya chama kama wao waliona ni maarufu kuliko chama wakaanzishe chama chao waone kama ni rahisi..let them go..simple
 
Mtei alitaka hatua hiyo isifananishwe na mgogoro ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao umesababishwa na maslahi binafsi.

Mzee Mtei heshima yako,
Waliotimuliwa hapa ni wale wale waliokuwa wanampinga Mbowe kwenye uchaguzi uliopita. Hebu tupe ushahidi kuonyesha kuwa hawakufukuzwa kwa maslahi binafsi ya Mbowe ambaye sasa inaonekana anamburuza Dr. Slaa kama mtumishi wake binafsi?

Alisema baada ya Chadema kusitisha ajira za waajiriwa kadhaa baadhi ya watu wamepinga hatua hiyo na kuielezea kuwa ni mgogoro ndani ya chama hicho jambo ambalo sio kweli.

Mzee Mtei,
Kama haya ni kweli umeyasema, hebu tufahamishe tokea lini msuguano wa uongozi wa juu chamani kiasi cha kufukuzana sio mgogoro ndani ya chama?

Mtei aliongeza kuwa kilichopo ndani ya Chadema ni baadhi ya watu wasiofuata kanuni na misingi inayoongoza chama hicho ambao haoni sababu ya watu hao kuendelea kuwepo.

Hao wanaosema kuwa Chadema ama katibu mkuu amekosea kuwaondoa kazini baadhi ya watu,hawapo sahihi,wale ni waajiriwa na ajira zao zinaweza kukoma wakati wowote kama ilivyofanywa na sioni sababu ya chadema kuendelea kuwa na watu wasiofuata misingi ya chama, alisema Mtei.

Kanuni na misingi ipi iliyovunjwa? Kama ipo kwa nini wanachama hawataarifiwi hizo kanuni na misingi ili isionekane kuwa watu wanafukuzwa bila sababu?

Mzee Mtei, kwa kuwapiga vita wale wote wasiomuunga mkono Mbowe, nafikiri huko ni kukibomoa chama. Tutafukuza wangapi kwenye uongozi ili tu Mbowe abakie na Uenyekiti?
 
Nashangaa kuwa pamoja na ubakaji wa demokrasia walioufanya chadema, mtei kusema CCM walipenyeza fedha bila kuwataja wanachama waliokamatwa, na hili la sasa nachelea kusema huyu mzee anakiharibu chama hiki.

Sitasita kusema kuwa Chadema wakishika nchi wanaweza wakafanya kama yaliyotokea kenya-kung'ang'ania madaraka!

Tunaweza kutukananana humu, lakini athari zake ni kubwa kwa vizazi vyote vijavyo,VIJANA WANATAKA KUJIUNGA NA CHADEMA WAKIWA NA AMBITION TOFAUTI, WENGINE WANATAKA KUWA MARAIS, inakuwaje mtu kama hana hakika akienda chadema atakuja kupata nafasi anayoiota?

Please ushabiki pembeni hapa tuangalie kulia na kushoto, I love chadema

ukweli ndiyo huo
 
Waberoya,
Kwa ajili ya Tanzania njema usijiunge na Chadema kutafuta cheo. Jiunge na Chadema kama njia ya uhakika ya kuleta mabadiliko yanayohitajika Tanzania. Ni ushauri tu.
 
Jasusi,
Pamoja na yote hayo nyie wanachama (wajumbe) mnayajua yaliyotokea hadi viongozi hawa kunyang'anywa maradaka yao? kama hamjui huoni kuna umuhimu wa nyie kuelezwa ikiwa nyie dio mlowachagua watu hao..
 
Back
Top Bottom