Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

TUKO PAMOJA KAFULILA KATIKA HILI...kwani sio mtu ukienguliwa kwenye nafasi yako....basi unahama!...Mimi najua hunifahamu, lakini nimekuwa nikifuatilia makala zako mara kwa mara. usirudi nyuma...ni kweli CHADEMA inakabiliwa na changamoto nyingi lakini bado inahitaji vijana kama wenye upeo wa kafulila kwa kujenga na kubomoa hoja. najua umeonewa, lakini usimlaumu slaa...tatizo la chama chako ni mbowe na uchagga tu.....slaa anatumiwa...

Mkuyumkubwa

Hebu tuambie, ni kwa nini unasema Kafulila kaonewa? Kwa lipi? Je, CHADEMA kijana makini ni Kafulila tu? Maana sijakuona ukiwasifia wengine kina Zitto, Mnyika, Mrema nk

Kwa vipi unadhani Dr Slaa anatumiwa tu?

serayamajimbo
 
Siasa za minara ya simu kutafuta network kisha kubaki ilipo....
 
Mkuyumkubwa

Hebu tuambie, ni kwa nini unasema Kafulila kaonewa? Kwa lipi? Je, CHADEMA kijana makini ni Kafulila tu? Maana sijakuona ukiwasifia wengine kina Zitto, Mnyika, Mrema nk

Kwa vipi unadhani Dr Slaa anatumiwa tu?

serayamajimbo

Mkuyu mkubwa jana alisema kuwa kafulila sio mtu wa kuchezewa kwa vile alianguka ghorofa kumi na akapona kwa siku nane tu (akasisitiza kuwa usicheze na watu wa kigoma).

Mimi nitaanza kumuita mkuyumkubwa kama Dr Mkuyumkubwa.
 
Sisemi kwamba kijana makini ni kafulila tu. hapana. CHADEMa ina vijana wengi makini...wakiongozwa na zitto, mnyika, halima,nk....kila mmoja na mapungufu yake lakini wanaweza kufanya kitu kikubwa katika nchi yao..muhimu wajue tu kwamba tatizo la chama chao ni MBOWE.....Kafulila ni kijana mwenye uwezo mzuri wa kuchambua hoja kwa kadiri ya makala zake nilimsoma...lakini hata maoni anayotoa kwenye media naona upeo mzuri wa kijana huyu....hasa napotazama namna anavyopigania jimbo lake la Kigoma kusini kuhakikisha anashinda na kufanya mambo makubwa katika siasa za kigoma akiwa masikini kabisa...NADHANI ATAFIKA MBALI...MUHIMU AWE MVUMILIVU KWENYE CHAMA CHAKE...John Mrema sio miongoni mwa vijana wenye upeo kabisa...mimi nimesoma nae..na kuna wakati nimesoma maandiko yako kwenye magazeti....bado....NI UCHAGGGA TU!
 
Umesomea wapi wewe - kwa dr matungalehe wa kompelora?
 
utoto ukikutoka utaacha .
tulia kidogo ufikiri kwanini masanilo aliowataja kawaita mafisadi na je? nani kathibitisha?

Kujisaidia ajisaidie kuku tu bata eti kaharisha.

ee kwa heri
naaam nasusha pumzi afwadhali ujipotezee mkapam. matamshi yako yamejaa uchuro tepetepe maana unaloweka bila kupekshen mifuko. kanunue omo wasaa wa kufulia umefika
 
Nipo UDOM.....au hupendi kusikia chadema ikiambiwa ukweli? ndio maana kafulila anakataza vikao vya chadema kufanyika geto kweli.
 
mambo sasa yanabadilika hapa jf ,ukisoma pg nyingi hapa ni habari za propaganda ambanzo hazitusaidii sisi watanzania masikini.mwelekeo huu ukiendelea utaharibu hadhi ya jf.
 
Sisemi kwamba kijana makini ni kafulila tu. hapana. CHADEMa ina vijana wengi makini...wakiongozwa na zitto, mnyika, halima,nk....kila mmoja na mapungufu yake lakini wanaweza kufanya kitu kikubwa katika nchi yao..muhimu wajue tu kwamba tatizo la chama chao ni MBOWE.....Kafulila ni kijana mwenye uwezo mzuri wa kuchambua hoja kwa kadiri ya makala zake nilimsoma...lakini hata maoni anayotoa kwenye media naona upeo mzuri wa kijana huyu....hasa napotazama namna anavyopigania jimbo lake la Kigoma kusini kuhakikisha anashinda na kufanya mambo makubwa katika siasa za kigoma akiwa masikini kabisa...NADHANI ATAFIKA MBALI...MUHIMU AWE MVUMILIVU KWENYE CHAMA CHAKE...John Mrema sio miongoni mwa vijana wenye upeo kabisa...mimi nimesoma nae..na kuna wakati nimesoma maandiko yako kwenye magazeti....bado....NI UCHAGGGA TU!

Mkuyumkubwa

Naona unamsifu Kafulila na kumbeza Mbowe lakini mbona Kafulila anamsifu sana Mbowe?

Halafu kule Kigoma Kusini, unaonaje kati ya Kafulila na kijana mwenzake Muslim Hassanali ambaye ni mmoja wa wadhamini wa CHADEMA, cheo cha juu zaidi na aligombea ubunge jimbo hilo mwaka 2005?

Kwanini unasema Mrema hana upeo? Yeye si Mkurugenzi wa Bunge na halmashauri, ina maana ameteuliwa mtu ovyo ovyo?

Serayamajimbo
 
Nipo UDOM.....au hupendi kusikia chadema ikiambiwa ukweli? ndio maana kafulila anakataza vikao vya chadema kufanyika geto kweli.

Ukweli ndio upi kwa tafsiri yako? Kujua afya ya mtu kwa kumuangalia?

Yaani Kafulila kaanguka ghorofa kumi na kubonda kichwa chake, kisha wewe unakutana naye (kwa Dr Kitila Mkumbo) na kujua kuwa jamaa yuko fit kabisa kwa kumuangalia tu!

Mwl wako UDom ni nani? inafaa acharazwe bakora kwa anachokifanya.
 
Wakuu zangu huyu kafulila ndiye yule aliyekuwa chaguo la Zitto ktk Uongozi wa vijana ama mimi ndio nimechanganya!
Isije kuwa ugonvi ule umechukua hatua nyingine ndani ya chama...
 
NDUGU zanguni, mniwie radhi, ni naivety tu yangu kwenye hii siasa yetu; alichofanya kafulila si ndio inavyotakiwa?? yaani hakujiunga CHADEMA kwa ajili tu ya uongozi au??

Hivi CHADEMA ina wanachama wangapi hadi tujadili hayohayo tu!?
 
Huyu Kafulila (Kafulia) hana professional nyingine zaidi ya kuwa mwanasiasa? Atumie elimu yake kufanya mambo mengine kusaidia jamii!
 
Bundi ameanza kunyemelea familia ya Zitto Kabwe. Mama Mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ameitisha kikao juzi kujadili mustakabali wa familia. Mtoa habari wetu ambaye ni mmoja wa wanafamilia aliyehudhuria kikao hicho anaeleza kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na wanafamilia wa karibu akiwemo kaka wa Zitto anayejulikana kwa jina moja la Salum. Kikao hicho cha kifamilia kilijadili mustakabali wa kisiasa wa Zitto Kabwe na mambo yanayojitikeza ya chama chao cha CHADEMA. Baadhi ya watu wa karibu na familia walioalikwa kwenye kikao hicho ni pamoja na David Kafulila, ambaye Zitto amemtangaza hivi karibuni kuwa kijana mwenye akili anayemuandaa kuwa mbunge wa jimbo la jirani yake la Kigoma Kaskazini.

Kikao hicho cha kifamilia kimeazimia kuwa Zitto ajiuzulu na nafasi ya unaibu Katibu Mkuu CHADEMA ili asipoteze maisha kama Chacha Wangwe. Mama Mzazi wa Zitto Kabwe, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amethibitisha familia kuamua Zitto ajiondoe kwa ajili ya kulinda maisha yake. Mama huyo amenukuliwa na Gazeti la RAI akieleza kwamba familia inamtegemea sana Zitto na ameisadia kwa mengi hivyo wamemuandikia barua akiwa ujerumani kumweleza msimamo wao wa kutaka ajitoe.

Kikao hicho kilijadili misaada ya magari ambayo Zitto ametoa kwa baadhi ya vijana wanasiasa ndani ya CHADEMA kwa ajili ya kuwasaidia washinde katika majimbo yao ya uchaguzi. Mmoja kati ya watu hao anatajwa kuwa ni Msafiri Mtemelwa ambaye wakati wa uchaguzi wa ndani ya CHADEMA alikuwa Kampeni Meneja wa Zitto Kabwe kwenye kugombea nafasi ya uenyekiti na hata katika kupanga safu za viongozi wa ngazi zingine ndani ya CHADEMA. Familia ilielezwa kwamba hivi karibuni Msafiri alionekana akiongea na Katibu Mkuu Dr Slaa ofisini. Familia ikaelezwa kuwa alipigiwa simu hivi karibuni na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. Kutokana na mambo hayo, kikao hicho kilianza kumtilia mashaka kuwa amemgeuka Zitto Kabwe.

Mtoa habari wetu anafafanua kuwa David Kafulila alikieleza kikao kuwa Msafiri Mtemelwa alichangia uteuzi wake kama Afisa utenguliwe kwa kuwa alikuwa mjumbe wa Kikao cha Sekretariati kilichokaa chini ya uenyekiti wa Dr Slaa lakini hakumtetea. Kafulila aliendelea zaidi kukieleza kikao kuwa badala ya kupingana na wajumbe wengine wa sekretariati ili kumnusuru, Msafiri alitoa hoja kwamba atolewe nje ya kikao baada ya kujieleza kwa masaa manne ili maamuzi yaweze kufikiwa. Hivyo, wanafamilia walichukua uamuzi wa kumnyang'anya gari aliyopewa na Zitto Kabwe aina ya Prado. Uamuzi huu umeshatekelezwa kwa Msafiri Mtemelwa kunyang'anywa gari hiyo.

Mtoa habari wetu ameeleza kwamba maamuzi hayo na mambo mengine ya zamani yanaelekea kuigawa familia katika makundi mawili. Kundi moja likiwa ni lile linalolaumu urafiki na Zitto na baadhi ya marafiki wapya ambao wanaelekea kumweka mtoto wao mbali na viongozi wa chama chake na marafiki zake wa zamani na kumzushia migogoro yenye kutishia mustakabali wake wa kisiasa. Kundi lingine ni lile linaloamini kwamba viongozi wote wa kitaifa wa CHADEMA na marafiki wa zamani wanamchukia Zitto hivyo mustakabali wake wa kisiasa utategemea kuwashambulia na kuwamaliza viongozi hao na watu wanaotofautiana na Zitto; kundi hili linamsimamo kwamba kama mpango huu hautawezekana basi ni vizuri Zitto aache siasa kunusuru maisha yake.

Juzi gazeti la Alasiri limeandika ukurasa wa mbele habari ya kwamba Zitto ametangaza tena kuacha kugombea ubunge 2010 na badala yake anataka kuwa Mwalimu wa chuo Kikuu. Habari hiyo imefuatiwa na habari ya jana katika Gazeti la Rai ikimnukuu Mama Zitto akieleza kwamba mwanae ni msomi, afadhali afanye kazi zingine ili aendelee kuisaidia familia badala ya kubaki katika chama na kupoteza maisha yake.

Mwanafamilia huyo anaendelea kudodosa kuwa maadui wa Zitto wanatajwa kuwa ni Freeman Mbowe, Dr Slaa na wakurugenzi wote wa makao makuu ya CHADEMA isipokuwa Msafiri Mtemelwa. Katika orodha hiyo anatajwa pia mfanyabiashara mmoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari. Pia wabunge wote wa CHADEMA isipokuwa wawili. Gazeti la jana la Rai limeeleza pia katika kundi la wabunge anayeongoza kwa uadui na Zitto ni Halima Mdee ambaye anatajwa kuwa amewasilisha nyaraka ya tuhumu 22 dhidi ya Zitto Kabwe kwa chama hicho ikiwemo tuhuma zinazohusiana na masuala ya kampuni ya Dowans. Kutajwa kwa jina la Halima Mdee kumethibitisha maelezo ambayo Msaidizi wa Karibu wa Zitto Kabwe, Omar Ilyas aliwahi kuyatoa katika Mtandao wa Jamii Forums, akieleza kwamba yupo mbunge mmoja kijana ambaye alikuwa karibu na Zitto ambaye amemgeuka na kumtuhumu kwa mambo mbalimbali. Omar amekuwa akihusisha mbunge huyo, na jina la Mwafrika katika mtandao huo.

..........ndiyohiyo
 
Nadhani Kuna utoto kwa BAADHI ya marafiki wa Zitto wa kisiasa.

Nipo tayari kumuelezea Zitto ni kivipi kuna utoto. Kibanda alisema ni wajinga mimi nasema ni WATOTO.

Halafu Kama Halima Mdee anamshutumu Zitto mbona naye sio msafi tena sana!!!
 
hii chadema karibu nitashindwa kuanza kukielewa maana mara utasikia sijui mtei anamsaport mbowe kwavile na baba mke wake mara zito na familia sasa hichi ni cha cha siasa au ni chama cha mambo ya familia? upuuzi mtupu watu wanashindwa kutenganisha mambo na ndivyo watu wengi walivyo hata kwenye biashara kwenye utasikia mabo ya kifamilia kwa sana
 
Kati ya habari ambazo zimenifungia wiki hii vibaya ni hizi za mparaganyiko ndani ya CHADEMA. Sikuwahi kuzifikiria. Niko kwenye maombi yasifikie pabaya zaidi ya hapa walipo. Kama naiona NCCR Mageuzi ya 1997 ilivoanza kumeguka! Naikumbuka vizuri timu nzima ya NCCR Mageuzi ilipotua Magu - Mwanza kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Magu(tena enzi hizo hata jimbo la busega halijazaliwa) kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge enzi hizo marehemu Lupondije. Naikumbuka timu iliongozwa na Mrema, akifuiatiwa na Marando, alikuja kijana wa mwalimu(simkumbuki jina ila aliporudi ccm alipewa ubunge wa kuteuliwa), alikuepo masumbuko lamwai na wengine wengi. Timu ile ilikuwa imekamilika. Nilikuwa naipenda sana ingawa mzee wa mapesa aliwapiga bao na kuchukua ubunge. Wakati wa kampeni zilishasikika tetesi kuwa makao makuu ncc mageuzi hakukaliki. Lakini jamaa walikuja na mshikamano mzuri sana. Baada ya wa uchaguzi mdogo, Mrema aliwekwa kitimoto na wananchama wa magu katika ukumbi wa Tujengane. Ndipo Mrema alipowaambia kuwa mnavyosikia kwenye vyombo vya habari ni ya kweli. Baada tu ya kurudi Dar ndipo anguko kuu la NCCR lilitokea!! Nisingependa kusikia haya ndani ya Chadema. Ikitokea basi mnatupa nafasi nzuri sana CCM kuendeleza ujinga kwa Watanzania. Chadema muelewe nyie ni chama na ni zaidi ya chama. Zitto aliwahi kusema kule kwao Kigoma Chadema ni kama 'Movement' fulani. Natamani spirit hii ya wanakigoma iwe kwa Watanzania wote kuwa ChADEMA ni kama movement ili kuleta changamoto kwa CCM viongozi wawe macho. Mkiendelea kujichanganya hivi sijui.....
 
Zitto needs coaching.

Hawa marafiki zake yaani sijui niwaweke kundi gani, Naombeni elimu za hawa marafiki zake wa karibu kisiasa, yaani kuropoka hovyo hovyo tu magazetini, habari za nyumbani zinavujishwa hovyohovyo. The look like some wahuni wasio na strategies wale vision!

Sorry, lakini baada ya kusoma sana sehemu nyingi na kuulizia around nakubaliana na Absalom Kibanda na pia kwa sasa nipo na Dr Slaa, huyu David Kafulila HAFAI na marafiki wa Zitto kisiasa ni WATOTO.
 
Hii ni habari iliyonukuliwa kutoka katika gazeti au ni maoni yako habarindiohiyo? anyways hii ni siHasa kwa hiyo i dont expect better than this.
 
Sina hakika kama gazeti linalonukuriwa la RAI linaripoti kile kilichotokea, lakini kama kilichoandikwa ni kweli, ni vema Zitto amshauri mama mzazi wake aachane na active politics. Si jambo baya akibakia mwanachama wa CHADEMA bila kuwa kiongozi. Nina hofu mafisadi wanaweza kumtumikisha bila yeye kujua kuwa anawatumikia.
 
Back
Top Bottom