FP
Mbowe anashambuliwa zaidi kwa maoni yangu, kwa kuwa unapozungumza masuala ya fedha huku mzungumzwa ni mchagga. Ni mkakati wa kumvika beji ya ubadhirifu, kwa kuwa wafanya propaganda hizo wanajua wazi kuwa jamii ya watanzania ina mtazamo tofauti kuhusu wachagga. Mbowe anashambuliwa zaidi kwa kuwa ni Mwenyekiti wa chama, ni mkakati tu wa mpige Mchungaji na kondoo watatawanyika. Kumwangusha Mbowe Mwenyekiti, ni kuiangusha CHADEMA. Hivyo, wote mnapenda CHADEMA iendelee kudumu mnawajibu wa kumlinda Mwenyekiti wa CHADEMA. Nafurahi kama Dr Slaa analitambua hilo
Mbowe ni tofauti kabisa na Wenyeviti wote; halipwi mshahara na CHADEMA kama Lipumba anavyolipwa na CUF. Hapewi Posho za vikao. Anajiweka mbali na fedha za CHADEMA. Kosa lake kubwa ni kuwa mwaka 2005; alitoa kiwango kikubwa cha fedha kukupesha kampeni za CHADEMA. Zaidi ya milioni 300 kwa baraka za Kamati Kuu ya Chama. Baada ya uchaguzi huo akaseme zaidi ya nusu ya fedha hizo kama mchango wake kwa chama. Sasa wakina Mrema,Mbatia nk; hakuna aliyefanya hivyo. Ndio maana anatajwa kwenye masuala ya fedha. masuala yote haya ya fedha CHADEMA iliyaweka hadharani. Wenyeviti wengine wote na vyama vyao hawajawa transparent kwa kiwango hicho
Asha