Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Wahenga hawakukosea waliposema "ukiona mwenzio ananyolewa nawe tia kichwa chako maji".....CHADEMA nayo hiyooooooo katika safari ya kuvurugana.
 
Dk Slaa awatimua maswahiba wa Zitto
KAKASLAA.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa ambaye jana alitangaza kuwavua uongozi viongozi wawili wa kitaifa,huku hatua hiyo ikipingwa na Naibu katibu mkuu wake Zitto Kabwe
broken-heart.jpg
NI VIONGOZI WAWILI WA KITAIFA. ZITTO APINGA VIKALI

Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe

HATIMAYE yule bundi wa kisiasa ambaye alikuwa akiinyemelea Chadema, sasa ametua rasmi baada ya chama hicho kutangaza kuwatimua maafisa waandamizi wawili ambao ni washirika wakubwa wa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ambaye ameeleza bayana kutofautiana na maamuzi hayo.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alitangaza jana kuwa kwa kutumia mamlaka yake amewavua nyadhifa zao David Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa chama hicho, na Danda Juju, ambaye alikuwa anahusika na mambo ya bunge.

"Tena andika mwandishi wala usiogope ni kwamba, leo (jana) kulikuwa na kikao, nimekiongoza mwenyewe na maamuzi nimeyatoa mwenyewe..., tumetengua uteuzi wao. Sasa ni wanachama wa kawaida," alisema Dk Slaa.

Uamuzi huo ambao unaonekana utagusa majeraha ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama hicho mwezi Septemba, umekuja siku chache baada ya kuvuja kwa taarifa za mkutano wa siri kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi, akiwemo Dk Slaa, ambao wanadaiwa kujadili nidhamu ya wanachama hao wawili pamoja na mama mzazi wa Zitto, Shida Salum.

Mbowe alikanusha kuwepo mkutano wenye ajenda hiyo ya kuwatimua wanachama hao akisema taarifa hizo ni "za kizushi", huku Dk Slaa akisema kuwa hakuna haja ya kuitisha kikao ili kuwashughulikia watendaji hao na kuwafananisha na sisimizi katika chama.

Jana Dk Slaa alisema kuwa ametengua ajira za watu hao wawili kwa maslahi ya chama na kuongeza:" Tunataka kusafisha chama..., maana tukiacha hali hii tunaweza kuingia Ikulu na mambo ya ajabu."

Kwa mujibu wa Dk Slaa, chama hicho kinaongozwa kwa taratibu na kwamba hakiongozwi na majungu hivyo anayekiuka lazima ashughulikiwe.

"Tuliwapa muda wa kutosha wa kujitetea," alisema mbunge huyo wa Karatu ambaye anatajwa kuwa atawania urais kwa tiketi ya Chadema.

Vyanzo vya habari vilidokeza kwamba wanachama hao walihojiwa kwa takriban saa tano katika mkutano uliofanyika makao makuu Kinondoni, Dar es Salaam kabla ya uamuzi wa kuwatimua.

Alipoulizwa sababu za kuwatimua, Dk Slaa alijibu: "Nimekwambia nimetumia mamlaka yangu, usiniulize vigezo au sababu.

"Kwani Rais Kikwete (Jakaya) akitengua ajira za watu mbona hamuulizi katumia vigezo gani... na mimi nina mamlaka ya kufanya hivyo bila kuulizwa."

Dk Slaa alifafanua kwamba, Chadema ni chama ambacho kina malengo hivyo lazima kijisafishe kwa kuweka misingi imara ya uongozi na si watu kufanya mambo bila taratibu.

Katibu huyo wa Chadema alisema haoni kama uamuzi huo unaweza kukiathiri chama hadi kikagawanyika, akisisitiza:"Nasema hakuna mpasuko wala kambi ndani ya Chadema mimi sioni mpasuko wowote.

"Lakini, pia ni bora mpasuko kuliko chama kufa, tukiachia mambo haya yakiendelea ya watu kujifanyia mambo bila taratibu, chama kitakufa... ninyi mnataka kife au?"

Dk Slaa pia alikanusha kuwa uamuzi huo ni kisasi cha mambo yaliyojitokeza katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa viongozi wa Chadema ambao ulitawaliwa na vurugu huku matokeo yakibatilishwa kwa kanuni kutofuatwa au rafu.

Lakini Zitto, ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi, alionekana kutofurahishwa na maamuzi hayo.

Katika ujumbe alioutuma kwa gazeti la Mwananchi jana, mbunge huyo wa Kigoma Mashariki alisema: "Ninasikitika kuwa tunachukua maamuzi kama haya kipindi hiki ambacho nchi inahitaji chama imara cha upinzani.

"Kafulila ni mgombea mtarajiwa wa ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini ambalo CCM wamefanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuliko majimbo yote nchini. Uamuzi huu unaweza kuwashtua sana wanachama wetu Kigoma Kusini na mkoa wa Kigoma kwa ujumla."

Zitto alikumbusha kuwa Kafulila aligombea uenyekiti wa jumuiya ya vijana ya Chadema na akashinda, lakini uchaguzi ulivurugwa na kufutwa na hivyo utarudiwa na hivyo uamuzi wa kumfukuza Kafulila ni dalili za wazi za watu waliofuta uchaguzi huo kuleta vurugu kwenye chama kwani wanachama hawatakubali uonevu.

"Kwangu mimi Kafulila ni kijana mahiri mwenye kukipenda chama chetu na ndio maana niliamua kumgroom (kumkuza) ili aje kuwa mgombea ubunge na baadaye mbunge katika Jimbo la Kigoma Kusini.

Anakipenda chama chake, ana akili nyingi na mjuzi wa kujenga hoja katika kutetea chama bila woga," ameandika Zitto katika ujumbe wake kwa Mwananchi.

Zitto aliwasihi viongozi wake kuwa makini katika maamuzi wanayochukua kwa kuwa yanaweza kuvunja moyo juhudi zote za ujenzi wa chama na kuwataka wanachama kutulia mpaka hapo taarifa rasmi za chama zitakapotolewa.

Naye Kafulila alisema: "Sina kinyongo na mtu yeyote ndani ya Chadema na nitagombea ubunge wa Kigoma Kusini kama kawaida.

"Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba nakipenda sana chama changu, namheshimu sana Dk Slaa, najua tatizo la msingi halijapatiwa ufumbuzi."

Naye Juju alihoji sababu za maamuzi hayo kuwalenga watu ambao wamekuwa wakionekana kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Zitto kwenye kampeni.
"Sasa angalia na jiulize mwenyewe kwanini sisi tuliokuwa kwa Zitto," alihoji.

Katika barua ya kumuita mbele ya mkutano huo kujieleza iliyoandikwa na kaimu katibu mkuu, Kafulila alitakiwa aeleze kuhusu matamshi yake kwenye magazeti na mengine anayoyafahamu kuhusu vyanzo vya habari hizo.

Habari zinasema kuwa Juju hakupewa barua ya kuitwa, lakini alipigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya mkutano huo saa 3:00 asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa. Imeelezwa kuwa mahojiano hayo yalifanyika hadi saa 9:00 alasiri Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, kikao hicho kilianza saa 3:00 asubuhi na kumalizika saa 9:00 alasiri, kisha kufikia maamuzi hayo ya kuvuliwa nyadhifa kwa Kafulila na Danda, ambao sasa ni wanachama wa kawaida.

source.gazeti la mwananchi la leo.

ninachojifunza hapa ni kuwa kumbe walipewa nafasi ya kujieleza na kujitetea.
pia kumbe walipewa barua rasmi siku moja kabla na hivyo walikuwa na muda mzuri wa kujiandaa na kuandaa utetezi wao wote.
 
Walisema wahenga
Kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo...

Naamini kabisa hawa vijana waliamua kuchomekea jina la Shida Salum ili wapate uungwaji mkono na Zitto katika Mipango yao Haramu kabisa
 
Waache na wao watoane macho kama wenzao wa CC em!! Majungu na kutoaminiana hakuko CC em tu jamani! Kujenga demokrasia si kazi ndogo!! Watanzania msihofu, tuko kwenye kipindi cha mpito.

nimeipenda hii observation yako....you have my big thank you
 
tusijaribu kuwekeza kwa mtu utakuja juta mbeleni pia huo nao ni ushauri.

hii ni sahihi kama historia ilivyotufundisha huko kenya....ODM waliwekeza kwa Samuel Kivuitu lakini D-Day ilipofika aliwaangusha.
 
Naamini kabisa hawa vijana waliamua kuchomekea jina la Shida Salum ili wapate uungwaji mkono na Zitto katika Mipango yao Haramu kabisa

Basi Mh. Zitto ana marafiki ambao siyo waaminifu. Hivi huyu aliyevuliwa uongozi si ni yule niliyemusoma humu kuwa alikuwa anatumwa Habari Co. sijui kwa .........." anyway basi wabadilike sasa hivi ni watu wazima, jengeni chama chenu andoa makundi.
 
CHADEMA ni ya wanachama (Wanachadema) na si ya mtu binafsi au kundi fulani la viongozi. Ni vizuri migogoro inapojitokeza, viongozi wasichukue maamuzi kwa ajili ya kilinda maslahi yao binafsi, bali wachukue maamuzi kwa ajili ya wanachama wote.
Wasipokuwa makini, wapinzani wao hasa ccm wataitumia hiyo nafasi ili kuwasambaratisha zaidi.

MWISHO TUTAPA USEMI HUU "VITA VYA CHADEMA, NEEMA KWA CCM"
 
Mbowe is right....more than right!!!!
Fukuza mamluk Chair,hatuwezi kuwa na wanachama ambao wanavuruga chama afu tuwaache eti chama kitavurugika.
Uwepo wao ni matatizo kwa chama,so its better wafukuzwe.

tafadhali rejea italics hapo juu...chadema ina makundi kama CCM na wewe umechukua muelekeo fulani...assessment yako inaweza hata kuwa biased

Sina imani sana na Zito,huyu dogo anaonekana hayuko stable bado,though ni popular,but we should not trust him 100%.

hapa inabidi ueleze sababu na si hisia tu kuwa hayuko stable an pengine ufafanue kuwa stable maana yake nini..kuwa conservative au vipi maana hiyo nayo ni aina nyingine ya stability.


our chama.

wewe na akina mbowe siyo...watu wasio na mtazamo kama wako na wenzio hawatakiwi chadema?

CCM wanajaribu kutumia watu wenye ushawishi ndani ya chadema eg Zito kuvuruga chama chetu

sitaki kuamini kuwa chadema inamuogopa Zitto kwa kiwango hiki...


thats why Naungana na Absalom Kibanda katika usemi wake
"Tatizo ndani ya chama anaungwa mkono na vijana wajinga sana"

hili hakishangazi maana Kibanda ni mtu wa mbowe
 
KAKASLAA.jpg




Jana Dk Slaa alisema kuwa ametengua ajira za watu hao wawili kwa maslahi ya chama na kuongeza:" Tunataka kusafisha chama..., maana tukiacha hali hii tunaweza kuingia Ikulu na mambo ya ajabu."

"Tuliwapa muda wa kutosha wa kujitetea," alisema mbunge huyo wa Karatu ambaye anatajwa kuwa atawania urais kwa tiketi ya Chadema.
Muhimu kuwa na ndoto!
 
mhariri wa Mtanzania leo ameamua kuwavaa Mnyika na Mrema akiwahusisha na kutenguliwa uteuzi wa Kafulila na Danda. Mhariri huyo katika habari yake ya leo ya ukurasa wa mbele ameeleza kwamba vijana hawana walikuwa na uhusiano wa karibu na Zitto Kabwe lakini wamgeuka na kuwa karibu na Mbowe. Mhariri huyo ameeleza kwamba kugeuka kwao kumetokana na ukabila na maslahi binafsi. Mwandishi wa habari huyo amewataja wakurugenzi hawa wawili wa chama hicho kuwa wote ni wachagga. Habari hiyo imewahusisha wabunge wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kuwa wote wako kwenye mkakati wa kummaliza kisiasa Zitto Kabwe kwa ajili ya kuisaidia CCM.

.......ndiyohiyo
 
Jamani tukubaliane na ukweli kwamba, mtu asipoonyesha tabia njema kama kiongozi ktk chama au kikundi chochote makini anatakiwa ama kujiuzuru au kuachishwa madaraka. Wala tusijenge woga na ugumu wa kuwajibika. Mbona siku zote tunapiga kelele Kikwete na CCM wawafukuze akina Rostam? hata akina Makamba kwani mzee Makamba ana nini cha ajabu hadi awe tofauti na Danda?

Umakini katika chama ni pamoja na kuwajibisha wanaofanya makosa. Ukisoma vizuri hapo utatambua kwamba Kufulila anaakili nzuri (kama mwandishi alinukuu sahihi). Lakini Danda bado anamatatizo, anadai kwanini wawili, wafuasi wa Zitto wanaandamwa. Huyu anataka kutuambia kwamba kuna kambi au kndi la Zitto lenye maslahi na style yake ya uongozi ndani ya chadema. Zitto naye anawatetea tu bila kujua nini kinatokea.

Naomba kumuuliza Mhe. Zitto, hivi mkuu wewe ungekuwa umepata umwenyekiti wa chama ungemzuia Katibu kufukuza kazi Afisa mwenye makosa? au ungekuwa Katibu Mkuu usingemfukuza kazi Afisa mwenye makosa? Tena kwasasa wewe ni msaidizi wa Dr. Slaa, unataka kuniambia hujui kazi ya Katibu Mkuu? au unataka kuniambia watu wanaokuunga mkono wewe huwa hawafanyi makosa? Mbona wewe ni mmoja wa walalamikaji kumtaka Rais awajibishe mawaziri na watendaji wabovu!

Tuache taratibu na majukumu yachukue mkondo wake na siyo hisia na urafiki.
 
Wewe ni mzushi tu, Mnyika sio Mchaga Ni Msukuma na ni mzaliwa wa Mwanza acha mambo yako ya ukabila na kutunga uongo usio na maana. uliza kabla hujatoa shutuma au fanya kwanza utafiti, hapa si mahala pa udaku, hii ni Forum ya watu makini Mkuu kuwa na adabu
 
Dr Slaa, Zitto watofautiana na viongozi wenzao




Kikao hicho kilihusisha pia wabunge wote wa CHADEMA waliokuwepo Dodoma wakati huo wakiwemo Ndesamburo, Charles Mwera, Susan Lyimo na Grace Kiwelu. Wabunge Halima Mdee, Lucy Owenya na Ana Komu ambao wametajwa na magazeti yote mawili kuwa walihudhuria kikao hicho Dodoma hawakuwepo Dodoma wala kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa safari nje ya nchi.
”.

Naona leo Majira, Mtanzania na Mwananchi wamerudia tena kuandika kwamba wabunge waliokuwepo Dodoma ni Halima, Owenya na Anna Komu. Mbona ushahidi wote unaonyesha kwamba walikuwa nje ya Dodoma, na kwamba walioshiriki kikao ni Ndesamburo, Mwera, Arfi, Slaa, Lyimo na Kiwelu?
 
Wewe ni mzushi tu, Mnyika sio Mchaga Ni Msukuma na ni mzaliwa wa Mwanza acha mambo yako ya ukabila na kutunga uongo usio na maana. uliza kabla hujatoa shutuma au fanya kwanza utafiti, hapa si mahala pa udaku, hii ni Forum ya watu makini Mkuu kuwa na adabu

Si maneno yangu, ni habari ya leo ya ukurasa wa mbele ya Mtanzania yenye kichwa Zitto ahujumiwa. Habari imeandikwa na Sarah Mosi

....ndiyohiyo
 
Mkuu ukikuta utumbo nje ukauchukua na ukaja kuuweka kwenye JF na wewe ni mmoja wao, ukileta jambo zuri tutakupongeza na ukileta baya lawama lazima upokee mkuu, hata mimi nimesoma hiyo habari nikaipuuza maana ina uongo mwingi kuliko ukweli
 
Kwani Zitto na Mbowe walianza kutofautiana lini? Huu upuuzi kabisa, kitengo cha Tabwe Hiza kipo kazini sasa.
 
Back
Top Bottom