Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Kafulila ni nani hata awe na mgogoro na Mbowe?
Mbona kila mtu huko sasa hata mfagizi atasema kuwa naye ana mgogoro na Mbowe?
Kwa nini Mbowe kila issue wakati yeye sio mjumbe wa Secretariat?
Mbona Kafulila anajitafutia umaarufu kupitia mgongo wa Mbowe?
Kwa nini haya maswali yameulizwa hapa na leo?
Je? haya ndio yale aliyosema kafulila kwenye gazeti la Mwananchi jumapili kuwa mambo yote yatakuwa hadharani ndio hilo la disemba?
We are more than this, huyu anaonekana kuwa anachuki zake binafsi na Mbowe na wala sio kitu kingine.

Na wewe John Mrema , si utoke huko mbona kila siku lawama zinarushwa kwako tuu wewe na Mnyika?
Ama ninyi ndio nguzo ya hicho chama ama ni kikwazo ?

Jibuni haya maswali kwanza.
 
Unapenda pombe za bure kutoka kwa mbowe ndio maana mapofu yanakutoka akisemwa he! pole sana

Ha ha ha,

Kisha Tumaini akaendelea,

Ohsamdan,

Ule mpango wa kupiga pombe marufuku umeishia wapi

***mzee O --- Nilidhani tutaanza kuvunja mabucha ya nguruwe kwanza
Tumaini --- mabucha ya nguruwe mpaka mwakani wakati wa uchaguzi
***mzee O --- sema tu mullah, chochote utakachoamua
Tumaini --- mimi naona tuanze na hizi night clubs

Tumaini (huku akizuia mate kumdondoka) -- wakatoliki wanafaidi sana

--- Tuanze na Bilicanas.

*** mzee O --- lakini bilicanas kuna pombe za bure, tutazipata wapi?

Tumaini --- shhhhhh, sema taratibu maalimu Hashim wabiraho asikusikie
 
Mwafrika! pombe za bure mbaya....ok bilicanas haitafanywa kitu endelea kumtetea kihiyo wako hapa...maana dezo dezo..
 
Jibuni haya maswali kwanza.

Mkuu Haki Sawa katika Uchaguzi uliofanyika wa CHADEMA kulikuwa kuna watu wanamuunga mkono Mbowe na wengine walikuwa wanamuunga Mkono Zitto, Pamoja na kwamba wazee waliingilia kati na kumshauri Zitto ajitoe inaonekana Bado kuna watu katika hayo Makundi hawajirudhika na Uamuzi wa Zitto kumvaa Mbowe vile kuna wengine bado hawajaridhika na Uamuzi wa Zitto Kujitoa. Yawezekana kabisa Mbowe na Zitto walishamalizana baada ya Uchaguzi ila kuna Wapambe ( Wapambe kaka ni Nuksi). Sasa Mapambano bado yanaendelezwa na Hao Wapambe. Akina kafulila inaonekana bado Hawajaridhishwa na suluhu ya Mbowe na Zitto na Ndiyo maana wanapandikiza Chuki kwa Zitto hata Kumuhusisha Shida Salum ambaye kwa Mujibu wa Dr. Slaa hata Jina lake halikutajwa kwenye 'retreat' meeting yao kule Idodomya.

Ushauri wangu kwa CHADEMA hakuna aliye juu ya chama, kama kuna mtu anajaribu kutumia majeraha ya Uchaguzi kuzuia chama kisiende Mbele huyo hafai sio tu kuwa Kiongozi bali hata Mwanachama.
 
Mwafrika! pombe za bure mbaya....ok bilicanas haitafanywa kitu endelea kumtetea kihiyo wako hapa...maana dezo dezo..

Kisha Ohsamdan anakuja na idea mpya..

*** Mimi naona tuachane na hizi night clubs, tukizifunga tutaenda wapi?

Tumaini (kwa hasira kidogo) ---shhh nimekwambia upunguze Sauti

Maalimu Hashim atakusikia bureee

***mzee O --- tumwambie tu labda ataacha kwenda uwanja wa fisi

Tumaini --- yaani unataka maalimu aje na sisi bilicanas

*** mzee O --- nakwambia siku akienda huko ataachana na haya mambo yake

Tumaini --- wewe wakatoliki washakuharibu sasa

*** mzee O --- wewe mwenyewe si unaona wanavyofurahia maisha?

Tumaini --- shhhhh
 
mhariri wa Mtanzania leo ameamua kuwavaa Mnyika na Mrema akiwahusisha na kutenguliwa uteuzi wa Kafulila na Danda. Mhariri huyo katika habari yake ya leo ya ukurasa wa mbele ameeleza kwamba vijana hawana walikuwa na uhusiano wa karibu na Zitto Kabwe lakini wamgeuka na kuwa karibu na Mbowe. Mhariri huyo ameeleza kwamba kugeuka kwao kumetokana na ukabila na maslahi binafsi. Mwandishi wa habari huyo amewataja wakurugenzi hawa wawili wa chama hicho kuwa wote ni wachagga. Habari hiyo imewahusisha wabunge wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kuwa wote wako kwenye mkakati wa kummaliza kisiasa Zitto Kabwe kwa ajili ya kuisaidia CCM.

.......ndiyohiyo

Bahariri Bengine Vichwa ba Panzi kabisa, sasa hapa unatengenezwa Ugomvi kati ya Zitto na Mbowe, Hivi CCM wanamuhofia Zitto kama Zitto ( I mean Zitto individualy)? Hiki ni Kichekesho jamani

Ila Namsahuri Zitto akae na Hawa jamaa awashauri namna ya Kufanya Siasa, Hizi sio siasa za Daruso jamani, its all abouts maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Namuamini Dr. Slaa sana
 
mhariri wa Mtanzania leo ameamua kuwavaa Mnyika na Mrema akiwahusisha na kutenguliwa uteuzi wa Kafulila na Danda. Mhariri huyo katika habari yake ya leo ya ukurasa wa mbele ameeleza kwamba vijana hawana walikuwa na uhusiano wa karibu na Zitto Kabwe lakini wamgeuka na kuwa karibu na Mbowe. Mhariri huyo ameeleza kwamba kugeuka kwao kumetokana na ukabila na maslahi binafsi. Mwandishi wa habari huyo amewataja wakurugenzi hawa wawili wa chama hicho kuwa wote ni wachagga. Habari hiyo imewahusisha wabunge wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kuwa wote wako kwenye mkakati wa kummaliza kisiasa Zitto Kabwe kwa ajili ya kuisaidia CCM.

.......ndiyohiyo

Hivi CHADEMA kuna Maslahi ya kugombewa jamani? Kama mtu anataka Maslahi Binafsi Mbona nahisi CHADEMA siyo mahala pake. Anyway usilolijua ni kama usiku wa Giza
 
Hivi CHADEMA kuna Maslahi ya kugombewa jamani? Kama mtu anataka Maslahi Binafsi Mbona nahisi CHADEMA siyo mahala pake. Anyway usilolijua ni kama usiku wa Giza

Mkuu;

Kuna swali moja naliona kila mara kukiwa na ugomvi au vurugu Chadema.

Hili swali naomba Mwafika rafiki yangu pia anisaidie kupata majibu.

KWANINI MHESHMIWA MBOWE ANAHUSISHWA NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA CHAMA?

Sijawahi kusikia Maalim, Mrema, Mbatia, Profesa, au Makaidi kulalamikiwa kuhusu fedha za chama.

Nakubaliana na jamaa mmoja humu (jina nimelisahau), Chadema lina wasomi au wajuvi wengi ambao wanahoji sana na hao watu inaelekea ni tatizo kwa Mheshmiwa Mbowe. Hapendi kuhojiwa.

Dr Slaa,

Najua upo hapa. Wewe kuwa Loyal kwa mwenyekiti sioni kama ni tatizo sana ingawa ni tatizo kidogo. Ninachoshauri ni kujaribu kujiweka katikati ujaribu kufanyia kazi hili la pesa. Jaribu kuwapatanisha hawa jamaa, na mshauri mwenyekiti kuhusu matumizi ya fedha za chama kama ni KWELI.

wasalaaam

FP
 
Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi Kafulila anasema "Ninakipenda sana chama changu, ninamheshimu sana Dr Slaa...najua tatizo la msingi halijapatiwa jibu..Ninatafakari! " .nikajiuliza kama tatizo la Kafulila ana mgogoro na Mbowe au CHADEMA? maana kafukuzwa na Slaa lakini bado anaonesha imani kubwa kwa slaa. tatizo ni nani? nini?....
1.Nimemsikia kijana aliyeshinda umakamu mwenyekiti wa BAVICHA akisema tatizo la kafulila ni misimamo...na mbowe anapenda vijana wa kuburuza....au wa kabila lake kama alivyo John Mrema
2.Kafulila amekuwa akidai vikao vya kujadili matumizi ya ruzuku ya chama kila mwezi pesa zinapoingia...ambazo ni zaidi ya milioni60..kitu ambacho mbowe hayuko tayari...Na huu ndio mgogoro mkubwa ndani ya CHADEMA.kwamba ni Mwenyekiti pekee katika vyama vya siasa vikubwa nchini ambae ni signatory wa chama ni yeye tu...Kikwete sio, Lupumba sio..
3.Inasemekana kafulila analalamika kuwa slaa anaburuzwa na mbowe, nakwamba slaa anafaa kabisa kuwa hata rais kwakuwa atakuwa juu ya wote...kwamba mwenyewe slaa hana hatia katika madili ya pesa...na kwamba hata kwenye viti maalumu, baada ya mbowe kubadilisha majini ya waliopendekezwa na baraza kuu kwa mujibu wa kanda zao, slaa aliagizwa akatetee kwenye kikao cha baraza kuu...wajumbe wakakataa....wakatishia kumfukuza, ndipo mbowe akaingilia kati kuomba radhi....ndipo slaa akasema "kama mwenyekiti aliyeagiza majina yabadilishwe amekiri kosa, basi na mimi nakiri kosa....
4.Nashukuru nimewahi kumwona kafulila akiwa na Dr Kitila Mkumbo nadhani ilikuwa mwezi wa nne kabla ya uchaguzi wa busanda. lakini anatisha...yani alianguka gorofa ya kumi lakini akapona kwa siku nane...na wala hakuwa amechubuka hata kidogo kicwani...isipokuwa miguuni..Du Kigoma????
5.Nimesikia alitakiwa kufukuzwa mara kwanza alipofuatilia sana matumizi ya milioni35 za desemba 2008, ambazo ni siri kubwa mpaka sasa...ila kesho ntaambiwa....maana jamaa anasema hiyo ni siri kubwa kwani vikao zaidi ya vinne vilikaa kutaka taarifa ya matumizi ya fedha hizo bila mafanikio...ndipo alipozidi kuhojiwa akatishiwa kufukuzwa.

NINAENDELEA KUCHUNGUZA MGOGORO HUU, NA NITAENDELEA KUTOA TAARIFA KILA NINAPO NUSA...HIZO NDIZO NIMENUSA LEO KUTOKA SAKATA HILO

ndugu yangu, acha propaganda za uongo.

Dr Slaa amesema wazi kuwa Kafulila ametenguliwa kutokana na kukiuka maadili, itifaki na taratibu za kawaida za utendaji. Na imeelezwa wazi kuwa ni kutokana na matamshi yake kwenye vyombo vya habari.

Matamshi hayo kwa aliyesoma gazeti la Majira Novemba 8 na Mwananchi Novemba 9 yanasema kuwa kikao kati ya Mbowe na Wabunge na Wakurugenzi wa chama kilikuwa kikao kisicho rasmi na amekiita kuwa ni kikao cha gheto. Amekwenda mbali zaidi kusema kuwa kikao hicho kilijadili kumfukuza uanachama. Jambo ambalo Slaa amesema halikujadiliwa kabisa Dodoma. Pia wamezusha kuwa kikao hicho cha Dodoma walikuwepo wakina Halima Mdee, Anna Komu na Lucy owenya wakati ambapo imebainika kuwa hawakuwepo kabisa bali walikuwepo Ndesa, Mwera, Arfi nk kujadili mwelekeo wa chama kwenda 2010.

Kumhusisha Dr Kitila na mambo hayo ni kumvunjia hadhi; Dr Kitila ni mjumbe hapa JF aingie na kueleza ukweli kwamba anakubaliana na kauli hizo za kihuni.

Dr Kitila anajua kabisa kuwa Sekretariati ya CHADEMA hukaa mara kwa mara na vikao vya bajeti hufanyika kila mwezi.

Kijana gani aliyeshinda umakamu Mwenyekiti BAVICHA wakati ambapo ilielezwa wazi kwenye vyombo vya habari kuwa uchaguzi wote wa vijana ulifutwa, na hayo ndio maamuzi ya Kamati Kuu?

serayamajimbo
 
Mkuu;

Kuna swali moja naliona kila mara kukiwa na ugomvi au vurugu Chadema.

Hili swali naomba Mwafika rafiki yangu pia anisaidie kupata majibu.

KWANINI MHESHMIWA MBOWE ANAHUSISHWA NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA CHAMA?

Sijawahi kusikia Maalim, Mrema, Mbatia, Profesa, au Makaidi kulalamikiwa kuhusu fedha za chama.

Nakubaliana na jamaa mmoja humu (jina nimelisahau), Chadema lina wasomi au wajuvi wengi ambao wanahoji sana na hao watu inaelekea ni tatizo kwa Mheshmiwa Mbowe. Hapendi kuhojiwa.

Dr Slaa,

Najua upo hapa. Wewe kuwa Loyal kwa mwenyekiti sioni kama ni tatizo sana ingawa ni tatizo kidogo. Ninachoshauri ni kujaribu kujiweka katikati ujaribu kufanyia kazi hili la pesa. Jaribu kuwapatanisha hawa jamaa, na mshauri mwenyekiti kuhusu matumizi ya fedha za chama kama ni KWELI.

wasalaaam

FP

FP

Mbowe anashambuliwa zaidi kwa maoni yangu, kwa kuwa unapozungumza masuala ya fedha huku mzungumzwa ni mchagga. Ni mkakati wa kumvika beji ya ubadhirifu, kwa kuwa wafanya propaganda hizo wanajua wazi kuwa jamii ya watanzania ina mtazamo tofauti kuhusu wachagga. Mbowe anashambuliwa zaidi kwa kuwa ni Mwenyekiti wa chama, ni mkakati tu wa mpige Mchungaji na kondoo watatawanyika. Kumwangusha Mbowe Mwenyekiti, ni kuiangusha CHADEMA. Hivyo, wote mnapenda CHADEMA iendelee kudumu mnawajibu wa kumlinda Mwenyekiti wa CHADEMA. Nafurahi kama Dr Slaa analitambua hilo

Mbowe ni tofauti kabisa na Wenyeviti wote; halipwi mshahara na CHADEMA kama Lipumba anavyolipwa na CUF. Hapewi Posho za vikao. Anajiweka mbali na fedha za CHADEMA. Kosa lake kubwa ni kuwa mwaka 2005; alitoa kiwango kikubwa cha fedha kukupesha kampeni za CHADEMA. Zaidi ya milioni 300 kwa baraka za Kamati Kuu ya Chama. Baada ya uchaguzi huo akaseme zaidi ya nusu ya fedha hizo kama mchango wake kwa chama. Sasa wakina Mrema,Mbatia nk; hakuna aliyefanya hivyo. Ndio maana anatajwa kwenye masuala ya fedha. masuala yote haya ya fedha CHADEMA iliyaweka hadharani. Wenyeviti wengine wote na vyama vyao hawajawa transparent kwa kiwango hicho

Asha
 
ndugu yangu, acha propaganda za uongo.

Dr Slaa amesema wazi kuwa Kafulila ametenguliwa kutokana na kukiuka maadili, itifaki na taratibu za kawaida za utendaji. Na imeelezwa wazi kuwa ni kutokana na matamshi yake kwenye vyombo vya habari.

Matamshi hayo kwa aliyesoma gazeti la Majira Novemba 8 na Mwananchi Novemba 9 yanasema kuwa kikao kati ya Mbowe na Wabunge na Wakurugenzi wa chama kilikuwa kikao kisicho rasmi na amekiita kuwa ni kikao cha gheto. Amekwenda mbali zaidi kusema kuwa kikao hicho kilijadili kumfukuza uanachama. Jambo ambalo Slaa amesema halikujadiliwa kabisa Dodoma. Pia wamezusha kuwa kikao hicho cha Dodoma walikuwepo wakina Halima Mdee, Anna Komu na Lucy owenya wakati ambapo imebainika kuwa hawakuwepo kabisa bali walikuwepo Ndesa, Mwera, Arfi nk kujadili mwelekeo wa chama kwenda 2010.

Kumhusisha Dr Kitila na mambo hayo ni kumvunjia hadhi; Dr Kitila ni mjumbe hapa JF aingie na kueleza ukweli kwamba anakubaliana na kauli hizo za kihuni.

Dr Kitila anajua kabisa kuwa Sekretariati ya CHADEMA hukaa mara kwa mara na vikao vya bajeti hufanyika kila mwezi.

Kijana gani aliyeshinda umakamu Mwenyekiti BAVICHA wakati ambapo ilielezwa wazi kwenye vyombo vya habari kuwa uchaguzi wote wa vijana ulifutwa, na hayo ndio maamuzi ya Kamati Kuu?

serayamajimbo

Nawaambieni Hakuna mtu anayetea maslahi ya Taifa akatetea CCM na akatetea CHADEMA .

CHADEMA ni kihiyo cha ajabu sana , hakuna hata mjinga mmoja atakaye kubaliana na maneno eti amesema vibaya ktk vyombo vya habari ihiali kila mmoja anatambua bayana ni vita ile ile .

Hapa hakuna cha Slaa wala nini Slaa naye ni kihiyo tu kama vihiyo vingine.NUKTA
anaendeshwa na fisadi Mbowe kama karagosi lilokosa mwelekeo.
 
Waliomuona na kumsikia Dr Slaa pale TBC1 jana walielewa. Vinginevyo ambao hamkumwelewa mtafuteni kwa wakati wenu atawaelewesha zaidi. Uzuri wa Mzee huyu huwa anasema analoliamini kuwa ni sahihi na hajing'ati ulimi anapoongea.
 
Wawe makini katika maamuzi kwa kweli wasije wakavunja umoja ndani ya chama.
 
Upinzani bongo unajukumu moja tu!
kupigana kufa na kupona ili cc em! iendelee na ibakie madarakani kwa miongo mingi ijayo. Nina uhakika na hilo.
 
Waliomuona na kumsikia Dr Slaa pale TBC1 jana walielewa. Vinginevyo ambao hamkumwelewa mtafuteni kwa wakati wenu atawaelewesha zaidi. Uzuri wa Mzee huyu huwa anasema analoliamini kuwa ni sahihi na hajing'ati ulimi anapoongea.

Kweli kabisa mimi nilipomsikiliza kwa makini huyu jamaa anauhakika na ukweli wa anachokisema! He is great kusema kweli! Mungu amzidishie hekima na busara nyingi
 
FP

Mbowe anashambuliwa zaidi kwa maoni yangu, kwa kuwa unapozungumza masuala ya fedha huku mzungumzwa ni mchagga. Ni mkakati wa kumvika beji ya ubadhirifu, kwa kuwa wafanya propaganda hizo wanajua wazi kuwa jamii ya watanzania ina mtazamo tofauti kuhusu wachagga. Mbowe anashambuliwa zaidi kwa kuwa ni Mwenyekiti wa chama, ni mkakati tu wa mpige Mchungaji na kondoo watatawanyika. Kumwangusha Mbowe Mwenyekiti, ni kuiangusha CHADEMA. Hivyo, wote mnapenda CHADEMA iendelee kudumu mnawajibu wa kumlinda Mwenyekiti wa CHADEMA. Nafurahi kama Dr Slaa analitambua hilo

Mbowe ni tofauti kabisa na Wenyeviti wote; halipwi mshahara na CHADEMA kama Lipumba anavyolipwa na CUF. Hapewi Posho za vikao. Anajiweka mbali na fedha za CHADEMA. Kosa lake kubwa ni kuwa mwaka 2005; alitoa kiwango kikubwa cha fedha kukupesha kampeni za CHADEMA. Zaidi ya milioni 300 kwa baraka za Kamati Kuu ya Chama. Baada ya uchaguzi huo akaseme zaidi ya nusu ya fedha hizo kama mchango wake kwa chama. Sasa wakina Mrema,Mbatia nk; hakuna aliyefanya hivyo. Ndio maana anatajwa kwenye masuala ya fedha. masuala yote haya ya fedha CHADEMA iliyaweka hadharani. Wenyeviti wengine wote na vyama vyao hawajawa transparent kwa kiwango hicho

Asha

Asha;

Umejibu very professional. I liked your response. Nimeridhika.

Swali la ziada ni kuwa je hao wanaomtuhumu Mbowe na ufujaji wa pesa za chama wanalitambua hilo?, kwanini hawalikubali kama wanalitambua?. Naomba usitumie hoja ya "wametumwa" maana ni too general.

Halafu, mmewahi kuwa na vikao vya usuluhishi?, yaani tume ya maridhiano ambapo yatakayozungumzwa yabakie humo na wasamehane?. Wasiwasi wangu ni kuwa Kama binadamu wengine Mbowe anaweza kuwawekea bifu wanaompinga, hilo halijengi, inatakiwa kama mwenyekiti awasaidie kimawazo na kuwarudisha kundini.

Waweke maadui wako karibu zaidi....
 
Waliomuona na kumsikia Dr Slaa pale TBC1 jana walielewa. Vinginevyo ambao hamkumwelewa mtafuteni kwa wakati wenu atawaelewesha zaidi. Uzuri wa Mzee huyu huwa anasema analoliamini kuwa ni sahihi na hajing'ati ulimi anapoongea.

Wewe unaweza mtafuta Lowasa ama RA kukuelewesha juu ya Ricmond? kama ndiyo kawatafute uache kulalamika hapa jf.
 
Asha;

Umejibu very professional. I liked your response. Nimeridhika.

Swali la ziada ni kuwa je hao wanaomtuhumu Mbowe na ufujaji wa pesa za chama wanalitambua hilo?, kwanini hawalikubali kama wanalitambua?. Naomba usitumie hoja ya "wametumwa" maana ni too general.

Halafu, mmewahi kuwa na vikao vya usuluhishi?, yaani tume ya maridhiano ambapo yatakayozungumzwa yabakie humo na wasamehane?. Wasiwasi wangu ni kuwa Kama binadamu wengine Mbowe anaweza kuwawekea bifu wanaompinga, hilo halijengi, inatakiwa kama mwenyekiti awasaidie kimawazo na kuwarudisha kundini.

Waweke maadui wako karibu zaidi....

Naamini wanalijua sana, lakini wanafanya makusudi. Suala la kujiuliza ni kwanini?

Kuhusu maridhiano, mambo yote haya ikiwemo taarifa za fedha yanajadiliwa kwa uwazi kwenye vikao vya CHADEMA kama ambavyo Dr Slaa ameeleza. Swali la kujiuliza; kwanini badala ya kwenda kuyajadili kwenye vikao vya chama watu hao kazi yao ni kuzungumza uongo kwenye vyombo vya habari?

Hata Zitto aliwahi kuandika hapa kwa kirefu JF kuhusu uadilifu wa Mbowe na kujitolea kwake kukisaidia chama kifedha; sasa huyo Kafulila anaposema kwamba ameondolewa kwa kuhoji masuala ya fedha kwenye sekretariati anaanzia wapi?

Atoe mtu maelezo au vielelezo kuwa Mbowe anaiba ruzuku ya CHADEMA basi! Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.

Asha
 
Back
Top Bottom